Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Bisha kwa hoja! Ni uamuzi gani mgumu hawa wengine wamewahi kufanya?

Hata 2015 NEC meeting kwa ajili ya nomination ya CCM presidential candidate tu JKM ilimshinda mpaka BWM akalazimika kuokoa jahazi!
Acha kulisha watu Matangopori kenge wewe kwa mahaba yako binafsi na jiwe
 
Wacha kulisha watu machicha serikali iliyopo madarakani haikuchaguliwa na wananchi,sema hawana nidhamu kwa Tume ya Uchaguzi iliyowaweka madarakani.hao viongozi wake wote waliwajibika kumtii Mkuu na sio kutatua matatizo ya wananchi,walimtii na kufuata aliyowakingia kifua kuwepo hapo.
 
ID ya ole sabaya au rc chalamila hii.Mungu wenu kafa,mtajiju
 
Mama yuko kwenye system zaidi ya miaka kumi kuna kamtu kako nyuma ya keyboard ya tecno kanasema mama hajui nchi inataka nini [emoji86][emoji86]
 
Wasukuma watu wanaofanya kz kwa kutotegemea ajira wala teuzi serikalini kukaa unawataja kwenye ujingaujinga wa kibaguzi ni kupoteza muda wako
Ndo acheni kumsakama madam President, zama zenu zishapita,mshukuru mmepata mbuga ya wanyama uko kwenu
 
naona unalalamikia vitu vya ajabu ww. kuna protocol za kiusalama.
wanaomtibu rais ni madkatari wa usalama, wanamlinda ni usalama. wana protocol zao.

waziri mkuu mwenyewe alikuwa hajui, vp mwenyewe alifichwa hali ya rais. kila kiongoiz alikuwa anakuja na lake.

unataka ujue identity zao ili iweje? ulitaka watangaze ili iwe vip?

they did their best but wakaishia hapo.
 
Nyie MATAGA mmefilisika akili.

Mama Samia is the BEST PRESIDENT since Nyerere. Ameanza vizuri na maneno yake yanaonyesha atapaisha uchumi wa nchi yetu fasta.

Mama Samia anajua anachokifanya. Hayati Magu alifanya wafanyabiashara wanyanyaswe hadi wengi wakafunga biashara makusanyo ya kodi yakapungua Ni maendeleo hayo?

Kwa miaka mitano tu ya Magu deni la taiifa lililoongezeka kwa kiasi kikubwa kuliko lilivyoongezeka kwa miaka thelathini kuanzia Mwinyi hadi Kikwete. Hiyo mikopo ilitumikaje wakati kila siku Magu alikuwa anasema pesa za kununua ndege, kujenga SGR, na Bwawa la Nyerere zote zilikuwa pesa za ndani?

Na hiyo miradi iliyoanzishwa "hewani" bila kupitia bungeni mnajua hasara zake? Abiria wa kutua uwanja wa kimataifa wa Chato wapo? Na hiyo hasara ya bilioni 600 iliyotokana na kufufua shirika letu la ndege kwa kukurupuka hamuioni? Kwa nini Hayati Magu aling'ang'ania kununua ndege cash wakati ulimwenguni kote hata mashirika makubwa kabisa ya ndege yananunua ndege zao kwa mikopo?

Kama hamjui jinsi uchumi wa nchi hii ulivyoharibika tangu Kikwete aondoke kaeni kimya.
 
Sukuma gang au ?
 
Waislamu... mtume amesemaje juu ya swala la uongozi.

Juu ya mwanamke kuwa kiongozi Mtume Muhammad S.A.W alisemaje?
 
Kuna watu hasa Wapinzani wameanza kumshangilia mama kwa nguvu sana wakina Zitto wanashingilia Mbaya, CDM wanashangilia mbaya.

Kitu kinacho nipa ukakasi kuamini kwamba hakuna Mageuzi ya maana kwa huyu mama ni pamoja na yafuatayo.

1. Timu yake asilimia 100 kwenye baraza la mawaziri ni ile ya Mwendazake, hawa kwanza ni ant Democracy wakubwa sana.

Huwezi kuchukua asilimia 100 ya timu ya mtangulizi wako then useme unafanya magezui.

2. Vinara wa sheria mbovu ni wale wale wakina Kabudi na wamerudishwa pale pale unategemea nini?

3. Waziri wa Pesa alikuwa Naibi awamu ya JK awamu ya Upigaji na anajua upigaji sana, Hana Miujiza hapo Wizarani.

4. Katibu mkuu wizara ya Habari Michezo na Utamaduni ndo alikuwa kinara wa kufungia vyombo vya habari na bado yuko pale pale unazani kwa nini kaachwa pale pale?

Mama kwa sasa anacheza na akili zs Wadanganyika kama mambo ya Data na kadhalika ila hakuna Mabadiliko alio fanya.

Lisu aliwahi sema huyu mama Mhafidhina hivyo watu wasitarajie mageuzi yoyote ya maana.
 
Kwa msio jua huyu mama alishataka kujiuzuru mara kadhaa kwakutokubaliana na mambo ya hayati cha roho mbaya Ila kilicho mbakiza ni busara za kina mzee wa msoga tu hivyo wasukuma tulieni dawa iwaingie.

Ninyi wasukuma rudini nyumbani mkachunge ng'ombe zamu yenu imeshapita,hivi unadhani mama alijisikiaje wakati mnafanya ya hovyo?Wakati mnaforce kila kitu kipelekwe chato mnadhani Mama alikuwa sambamba na hayati cha roho mbaya kwani yeye nae mchunga ng'ombe?

Mlisafirisha wanyama kuwapeleka chato kisha mkaanza na ile propaganda kwamba hifadhi ya burigi ndio kitovu cha utalii huko wakati mkijua kabisa watalii wengi huja Tanzania kwasababu ya mbuga ya serengeti.

Kwa ubinafsi wa hayati akajenga uwanja mkubwa wa ndege chato ambao hata Shinyanga haupo.Hivi unafikiri huyu mama yeye alikiwa anajisikiaje?

Mkaanza na mchakato wa kujenga uwanja mkubwa wa mpira Chato sehemu ambayo kwa idadi ya watu wake simba na yanga wakicheza hawawezi kujaza uwanja,huu ni wendawazimu.

Unatumbua watu wa vyeti feki kisha unambakiza bashite kwasababu ni sukuma mbele mwenzako watu wakipiga kelele unauliza "kwani vyeti ndio vinafanya kazi?".Mlifikiri huyu mama aliumia kiasi gani?

Mkawekana kindugu huko maofisini kila mahali palijaa wachunga ng'ombe,yani kwa muda mfupi Sana kuna baadhi ya ofisi hata vikao vingeweza fanyika kwa lugha ya wachunga ng'ombe.

Tunawataka mkae kimya mkiendelea na hizi chokochoko tutaendelea kuwachomoa mmojammoja huko maofisini mpaka muishe wote mrudi nyumbani mkachunge ng'ombe.

Kwa ujumla mama ni mvumilivu sana kwasababu kufanya kazi na mwenda zake aliejiona yeye ndio kila kitu,hapangiwi na mtu ilikiwa inahitaji roho ya chuma.
 
Hizo ni porojo za vijiweni. JPM hakuwa mtu wa kubembeleza mtu mwingine. Hata uchaguzi wa term ya pili ilikuwa fursa nzuri ya Samia kujiengua, kama angetaka!
Mbona JPM hakujitenga na BM au JK , badala yake alipokuwa Rais ndo akaanza kutenda tofauti na kuwananga watangulizi wake?

Najua wewe ni pro Magu, lakini tambua kila kiongozi ana muono au utaratibu wake, ambao atapenda wasaidizi wake wa cope hivyo. Haiwezekani hata Siku moja SSH, kuwaza na kutenda kama JPM, eti kwakuwa walikuwa serikali moja. Vivyo JPM hakutenda au kukopy na kupaste ya JK na BM.

Mkosoe au umnange pale serikali yake itakaposhindwa, kuiimarisha nchi kiuchumi, uzalishaji kuwa chini, utendaji serikalini kuzorota na huduma kwa jamii kuwa mbovu na kushinda kumalizia miradi ya kimkakati iliyo achwa na mtangulizi wake, pamoja na kushindwa kujenga miradi mipya.

Kwahiyo usitake SSH kuwa blend ya JPM, kama ambavyo wewe huendeshi familia in similar fashion ya wazazi wako. Kuna baadhi ulichukua na mengine ukayaacha na kubuni ya kwako.

Kuhusu kusahaulika kwa JPM, si rahisi kama ambavyo hatujamsahau Nyerere. Na wala si kwasababu hawakuwa na madhaifu, la hasha! Tunawakumbuka na kuwaenzi kwa mazuri waliyoitendea nchi. Lakini pia tambua hata JPM alipokuwa madarakani pamoja na mazuri yake, bado kulikuwa na mapungufu kadhaa yaliyo tufanya tumu miss JK.
 
Haya hapa makosa ya umakini ya Rais Samia Suluhu Hassan ambayo nimeya-notice tangu maandalizi mpaka muda alipoingia ofisini. Kama yapo mengine maGT mtaonngezea:

Siku anatangaza taarifa ya msiba wa JPM alifanya makosa mawili:

1. Mapumziko siku 14 badala ya 21

2. Kifo cha JPM kilisababishwa na tatizo la mfumo wa umeme, baadaye akajirudi akasema tatizo la moyo wa mfumo wa umeme.

Siku anafanya kikao cha kwanza cha Baraza la Mawaziri...

3. alichanganya kalamu ya wino mweusi badala ya mwekundu

Siku anateua Wakurugenzi...

4. Aliteua Mkurugenzi asiye na sifa na kumuacha mwenye sifa na baadaye kutengua uteuzi wa asiye na sifa na kumrejesha mwenye sifa.

Bunge la Jamhuri/Bunge la Katiba...

5. Mara moja au mara mbili amekuwa akitaja Bunge la Katiba wakati anapashwa kusema Bunge la Jamhuri.

Vyombo vya habari vilivyofungiwa.

6. Alisikika akisema vyombo vya habari vilivyofungiwa (akitolea mfano online tv na vingine) vifunguliwe lakini badae kauli ile ikahitaji kutolewa ufafanuzi na wasaidizi wake kuwa alimaanisha online tv pekee.

Mpaka sasa nimeona kuna hizo makosa 6 ambazo kwa maoni yangu ni nyingi mno kwa muda ambao amekuwa ofisini.

ushauri rahisi: ajitahidi akiwa kwenye mimbari awe na glass ya maji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…