Hizo ni porojo za vijiweni. JPM hakuwa mtu wa kubembeleza mtu mwingine. Hata uchaguzi wa term ya pili ilikuwa fursa nzuri ya Samia kujiengua, kama angetaka!
Mbona JPM hakujitenga na BM au JK , badala yake alipokuwa Rais ndo akaanza kutenda tofauti na kuwananga watangulizi wake?
Najua wewe ni pro Magu, lakini tambua kila kiongozi ana muono au utaratibu wake, ambao atapenda wasaidizi wake wa cope hivyo. Haiwezekani hata Siku moja SSH, kuwaza na kutenda kama JPM, eti kwakuwa walikuwa serikali moja. Vivyo JPM hakutenda au kukopy na kupaste ya JK na BM.
Mkosoe au umnange pale serikali yake itakaposhindwa, kuiimarisha nchi kiuchumi, uzalishaji kuwa chini, utendaji serikalini kuzorota na huduma kwa jamii kuwa mbovu na kushinda kumalizia miradi ya kimkakati iliyo achwa na mtangulizi wake, pamoja na kushindwa kujenga miradi mipya.
Kwahiyo usitake SSH kuwa blend ya JPM, kama ambavyo wewe huendeshi familia in similar fashion ya wazazi wako. Kuna baadhi ulichukua na mengine ukayaacha na kubuni ya kwako.
Kuhusu kusahaulika kwa JPM, si rahisi kama ambavyo hatujamsahau Nyerere. Na wala si kwasababu hawakuwa na madhaifu, la hasha! Tunawakumbuka na kuwaenzi kwa mazuri waliyoitendea nchi. Lakini pia tambua hata JPM alipokuwa madarakani pamoja na mazuri yake, bado kulikuwa na mapungufu kadhaa yaliyo tufanya tumu miss JK.