Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Sasa na wewe umeona umeandika kibwengo mkubwa ww. Uenda hata wewe ukosewa huyo si baba yako mzazi. Mbona mnapenda kuhangaika na makosa madogo? Vipi aliyesema Sadaam Hussein ni wa Kuwait.
 
Katika kila uongozi wowote watu wakubweka bweka ovyo hamkosekani hata kama ni mnafiki there is absolutely nothing unawza fanya.
Just sit back and relaxx jiangalie wee na tumbo lako
 
Tengua teua zipi zipi hizo ambazo hazikuwahi kuwepo kabla yake ? Amebadili kila kitu ? Ni vitu gani alivyobadili ? Kipimo cha watu makini ni kipi ? Maana ukisema mama hakuzungukwa na watu wakini, hasa watu makini ni kina nani ?

Mawaziri, manaibu na makatibu wakuu ni wale wale, waliobadilika ni kina nani ?? Kuna jitihada kubwa sana za kumpa sifa mbaya mama na bahati mbaya sana inafanywa na MATAGA
 
Tulikuwa tunaongozwa na Rais asiyejua hata kuongea kiswahili fasaha..
 
Eti imani kwa Marehemu..Mataga bana..upuuzi wote wa awamu iliyopita inapaswa ufumuliwe na Mama kashaanza kazi
 
Kwani nchi za nje zinatumia katiba ya Tanzania linapokuja suala la misiba ya viongozi ambao sio wa kwao?..Tungesema tunaomboleza miaka kumi bendera nusu mlingoti,hizo nchi za nje zingetufwata na sisi kama unavodai?
 
Rais ni Samia Suluhu Hassan..

Mengineyo yoote ni maoni tu
Na utofauti na wengine waliopita, yeye "maumbile yake ni mwanamke"

Kwa mara ya kwanza naona CCM wanapigana vijembe wao kwa wao
 
Hio ni aina ya mtu (ingawa sisemi kama huyu yupo hivyo) mfano Biden huwa anachanganya maneno akiwa anaongea... (Kwa Biden nadhani ni sababu ya kigugumizi chake)

Kwa huyu mama so long as dhamira yake ni nzuri na sio mnafiki wa kupitiliza, basi I will take the rough with the smooth... (nasema kupitiliza sababu wanasiasa na unafiki ni kama Kulwa na Dotto)
 
Hakuokoa jahazi alilizamisha
Bisha kwa hoja! Ni uamuzi gani mgumu hawa wengine wamewahi kufanya?

Hata 2015 NEC meeting kwa ajili ya nomination ya CCM presidential candidate tu JKM ilimshinda mpaka BWM akalazimika kuokoa jahazi!
 
Meko Mwendazake alishawahi weka Microphone sikioni akidhani simu
na simu akaweka mdomoni akijua ni Microphone
mbona tulikatazwa tusizitumie picha hizo
sasa kwa Mama mnaona ajabu gani?
 
Aya sasa wewe siku 31 umezitoa wapi? Kama wewe unakosea ukiwa peke yako iweje yeye aliyekuwa kazungukwa na wanafiki?
 
Jiwe amekinga bakuli kwa mabeberu miaka yote 5 ya utawala wake. Deni la Taifa limeongezeka kwa Trilliini 18 Tshs kwa kipindi hicho, amechukua hela za korosho, bureau de changes na mifuko ya jamii lakini bado maji yalikuwa yanazidi unga
Bila kukinga bakuli kwa mabeberu, huyu hana ujanja wa kuendesha hii nchi. Kwa hiyo, atalazimika kufuata masharti yote ya mabeberu!
 
Ninawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano
Na hilo Jina la Jamhuri ndio salamu yenyewe.

Na mnayemtazama mbele yenu mwanamke ndio Rais mwenyewe.

Naomba sana msiwape mdomo mdomo wa kusema tunawabinya.

Na ninaposema "naomba" sio kwa udhalili.

Manake we kijana mi ni mama, ukizingua tutazinguana.

Na wewe Mwambe wewe ndio ulitengeneza uozo wa pale Uwekezaji, sasa nakurudisha ukafanye kazi. Mwekezaji akija si lazima kuajiri Watanzania. Na wachimbaji wa madini sisi tunawahitaji wao zaidi ya wao wanavyotuhitaji, acha wachimbe.

Na wewe Mulamula ukarekebishe mahusiano yetu na dunia.

Mwisho kabisa lazima tumuenzi Marehemu mzee wetu katika miradi yake miwili!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…