Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Kinachonishangaza kwa herufi kubwa ni kwanini huyu mama anakubalika kwa kiwango hiki

na hawa wapinzani waliokua wanaichukia ccm kwa kiasi kile? kwanini? na kila hatua anayopiga

wapinzani wanapiga makofi na kufurahia,yani ni rahisi wa kwanza ambae wana ccm ndio tunamkosoa

na ni rais wa kwanza kutoka ccm ambae ni chaguo la upinzani,eti leo hii Mbowe ana hashtag #Samia2021-2030 kweliiiii?!!!?!?

natamani yote haya yawe ni ndoto,matamanio yangu ni mtu aniamshe aniambie Amka wewe,halafu nimsimulie nilichokua naota...
 
Inashangaza Sana[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Dunia haiishi maajabu.
 
Inashangaza Sana[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Dunia haiishi maajabu.
Anayeshangaaa atakua ana matatizo au ni ile hali ya kuona MPINZANI ni adui au kila anayekosa baya la ccm basi ni mpinzani.kiukweli mama ameanza vizuri...katika maisha kila mtu anapenda UTU wake uthaminiwa kwa rais aliyepita yy aliamini kwenye VITU zaidi na siyo ,Utu sasa mama Samia amekuja tofauti ndiyo maaana hata uwe mpinzani utafurahi tu.
 
Msibani kwa mwenda zake,mbona hawakuzuia watu kukusanyika?
Wale wa msibani hawakuwahi kulalamika kwamba kuna corona? Lkn hao wanaoomba kufanya mikutano wameshasema sio zaidi ya mara moja kwamba nchini kuna corona, na kuna kipindi waliwahi kutoka bungeni ili wakakae lockdown majumbani kwao. Sasa inakuaje waombe tena mkusanyiko wa mikutano? Lisu alisema mlinzi wa hayati Magufuli alikufa kwa corona, Mbowe nae alidai kuwa yeye ashapata chanjo ya corona. Sasa wanaomba mikusanyiko ya nini, kuuwa watu na hiyo corona yao au? Muda mungine unapoandika kitu jaribu kwanz kutumia akili yako kufikiri kuhusu swali lako sio unakuja na maswali kwa lengo la kutaka kumuonesha mwenyekiti kuwa unajua kuuliza na wakati ki uhalisia swali lako linakubana mwenyew kama hivi?
 
Hawa Wanaomsifia sasa ndo hao hao Watakaomnanga........Kama Enzi za Mzee Wa Msoga...! Tunaikumbuka ile Kauli Ya ' Raisi Dhaifu' ilitokea Wapi....!
Ety wamesahau , walikua wanamnanga haswa na walisema mzee wa angani na wakapiga hesabu za siku alizokaa angani , walimwita vascodagama, mara marcopolo..
 
Kama bado anacheka na Hamis basi ujue hamna kitu... mwizi hana maana
 
Jamani msilazimishe mawazo ya Rais aliyetutoka yafuatwe na Rais wetu Samia Suluhu. WaTanzania tutamsupport Rais huyu hata kama ni sisi upinzani au wana CCM ili nchi yetu ipate maendeleo ya wananchi wote!! wakulima, makuli, walimu, bodaboda, wafanya biashara kubwa na ndogo, wafanya kazi serikalini na binafsi!

Wapinzani na wana CCM wanaruhusiwa kukosoa na kushauri pale inapobidi ili inchi yetu ipige hatua na kapata mafanikio na maendeleo kwetu sote tulio WaTanzania.

Hebu tumsaidie Rais wetu tufaidike wote kama waTanzania !!!
 
Huu uzi mbona ni kama ule wa jpm anatupeleka wapi???
 
Unaweza ukawa sawa, lkn Rais has never raised that issue!
 



Ni mengi ameyasema lakini asipoweza kuondoa udhaifu huu wa kusema tu kwa maneno bila vitendo basi ataishia kuumia nafsi yake na wengine wataendelea kuumia pia.


Ipo siku wote tutakufa na tutaacha yote tulioyapigania, hivyo tupiganie kuwaachia watoto wetu na kizazi chetu kwa ujumla mambo mema na yenye kuwapa baraka na sio laana. Afrika kwa ujumla mengi tunayowaachia watoto wetu ni laana tupu
 
Reactions: Ame
Ipo siku wote tutakufa na tutaacha yote tulioyapigania, hivyo tupiganie kuwaachia watoto wetu na kizazi chetu kwa ujumla mambo mema na yenye kuwapa baraka na sio laana. Afrika kwa ujumla mengi tunayowaachia watoto wetu ni laana tupu
Kila mtu amejaa ubinafsi...Judgmental na full of hutred...Mama anajitahidi kuleta umoja tayari makundi yanayotaka upendeleo na uhakika wa interests zao zina mvuta huku na kule...Mpeni basi nafasi, atendee kwa kadri ya ufahamu wake. Weakness kila mtu anayo, ziacheni kwanza weakness zake kuzeni talents zake ili apate confidence ya kuongoza nchi kwa amani na upendo
 
Too early to pass judgement on Samia Leadership! Tumpe muda angalau hta siku mia moja za mwanzo ni bora zaidi kuliko mwezi mmoja wakati hata muundo wa serikali yake haujakamilika!
 
Reactions: Ame
Umeongea kwa point sana lakini, natamani kama point yako ingekuwa validi lakini naomba urejee clip ya siku mama anaapishwa uitizame mwanzo mpaka mwisho kisha angalia na clip ya siku za usoni ulinganishe je, anaelekea kwema ama kubaya? Akina majaliwa, mpango, kabudi, mwigulu, umi mwalimu, jafo, na wote wengine wameshambadilishia gia zake alizokuwa ameingiza tayari kuanza safari na sasa anaenda safari yao na sio yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…