Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Siku waTanzania watakapoanza kutumia akili zao na kuachana na matumizi ya mihemko....ndipo yatakapoanza mageuzi ya kweli kwenye taifa hili.

Ndio siku ambayo watapata kuziona bayana rangi za wanasiasa wao.

Na vugu vugu hilo halihitaji hata tamko la wanasiasa maana kila mmoja atajikuta ni muhanga wa utawala mbovu.......na hapo ndipo itakapozaliwa Tanzania mpya.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Kama vyama vya siasa bado vinakatazwa kufanya mikutano ya hadhara ambayo ipo kikatiba, na wewe hujaingilia kati kwa ishu ndogo kama hii ambayo hutapata lawama maana kipo kikatiba, Basi naanza kuwa na mashaka utawala wako.

Najua umezungukwa na wahafidhina wa CCM, lkn Kama dhamira yako, sheria na Katiba vinakupa haki katika kufanya lolote, waambie kuwa kwa hili niacheni.
Muacheni mama aendelee na kazi Imani itajijenga yenyewe
 
Mimi sijawahi kuwa na imani na CCM...

Na bi mkubwa si ndie alisema "hata tusiposhinda CCM ndio tutaunda serikali"

Huyu aliubariki udhalimu wa October kwa moyo mkunjufu kabisa! CCM ni ile ile..
 
Ongezea na issue ya vifurushi vya simu, waliotumbua pesa kwenye report ya CAG, uthubutu ni jambo gumu sana anaogopa kutengeneza maadui huko CCM.
Kwa habari ya ViFURUSHI vya smu, it seems VODACOM ama wameitia TCRA mfukoni, au ndo wanaendesha serikali hii ya awamu ya 6!

Maana, ingawa matamko yalitolewa na serikali kurejesha vifurushi vyote kwenye viwango vya awali, VODACOM wametulia kwa viwango vya ndugulile na genge lake ndani ya TCRA 🙄
 
Kama vyama vya siasa bado vinakatazwa kufanya mikutano ya hadhara ambayo ipo kikatiba, na wewe hujaingilia kati kwa ishu ndogo kama hii ambayo hutapata lawama maana kipo kikatiba, Basi naanza kuwa na mashaka utawala wako.

Najua umezungukwa na wahafidhina wa CCM, lkn Kama dhamira yako, sheria na Katiba vinakupa haki katika kufanya lolote, waambie kuwa kwa hili niacheni.

Nimesikia habari Kama hiyo bado sija ithibitisha. If that is true then lazima tuanze ku- doubt huu utawala wake pamoja na maneno mazuri aloanza nayo!!! Kwamba Watz tunatakiwa KUONDOA TOFAUTI ZETU NA KUONESHA MSHIKAMANO!!
Yawezekana WAHIFIDHINA wa CCM wameshaanza kumchanganya Mama....!!! Tunarudi kwene ule mse mo wa Kizaramo...ZILONGWA MBALI NA ZITENDWA MBALI!!!!
 
Kwa habari ya ViFURUSHI vya smu, it seems VODACOM ama wameitia TCRA mfukoni, au ndo wanaendesha serikali hii ya awamu ya 6!

Maana, ingawa matamko yalitolewa na serikali kurejesha vifurushi vyote kwenye viwango vya awali, VODACOM wametulia kwa viwango vya ndugulile na genge lake ndani ya TCRA [emoji849]
Hamna kitu hapo nimemsikia naibu waziri kama sijakosea akitolea hilo suala ufafanuzi bungeni akasema wao kama serikali lazima waangalie na wateja wao (makampuni ya simu) yanayowalipa kodi pia yaweze kupata faida.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Mama yuko sahihi,huu sio muda wa vimikutano vya hapa na pale ili kueneza propaganda na DJ Mbowe,na baba,mvinyo ni uleule ndani ya chupa tofauti.
 
Mama akituzingua na sisi tutamzingua kweli
Sisi hatutaki maneno matamu tunataa vitendo

1. Tunataka katiba mpya
2. Tunataka haki za kikatiba za watu na makundi yote ya kijamii ziheshimiwe
3.Tunataka sheria zote za kuminya uhuru wa habari ziondolewe
4. Tunataka freedom of speech
5. Tunataka tume huru ya uchaguzi
6. Tunataka marejesho bodi ya mikopo yashuke kutoka 15%
7. Tunataka magazeti yaliyofungiwa yafunguliwe
8.Tunataka sheria ya KIKOKOTOO ifutwe siyo kuipiga kalenda
9. Tunataka bei za vifurushi zishuke maramoja
 
Hamna kitu hapo nimemsikia naibu waziri kama sijakosea akitolea hilo suala ufafanuzi bungeni akasema wao kama serikali lazima waangalie na wateja wao (makampuni ya simu) yanayowalipa kodi pia yaweze kupata faida.
Mbona mitandao mingine wamerejea kwny viwango vya mwanzo?!
 
Hao waliorejea nao siwaamini, baada ya muda watashusha data taratibu, hiki unachokiona kwa voda ujue ndio benchmark na serikali iko upande wao.
 
Kama vyama vya siasa bado vinakatazwa kufanya mikutano ya hadhara ambayo ipo kikatiba, na wewe hujaingilia kati kwa ishu ndogo kama hii ambayo hutapata lawama maana kipo kikatiba, Basi naanza kuwa na mashaka utawala wako.

Najua umezungukwa na wahafidhina wa CCM, lkn Kama dhamira yako, sheria na Katiba vinakupa haki katika kufanya lolote, waambie kuwa kwa hili niacheni.
Hivyo vyama vyenu vyenyewe mnataka kuongelea nini hasa huko mikutanoni kama si matusi tu na kejeli!!? Kamq ataruhusu makelele yenu itakua ni ajabu kabisa, ngojeni wakati wa kampeni, msimchoshe Amir jeshi wetu ana mambo mengi ya muhimu kuliko nyie wachumia tumbo
 
Kama vyama vya siasa bado vinakatazwa kufanya mikutano ya hadhara ambayo ipo kikatiba, na wewe hujaingilia kati kwa ishu ndogo kama hii ambayo hutapata lawama maana kipo kikatiba, Basi naanza kuwa na mashaka utawala wako.

Najua umezungukwa na wahafidhina wa CCM, lkn Kama dhamira yako, sheria na Katiba vinakupa haki katika kufanya lolote, waambie kuwa kwa hili niacheni.

Rais ana haki ya kufanya kazi vile anavyoona inafaa . Sasa afanye kama wewe kwani wewe ni Rais?
 
Mama Samia achana na cheap popularity haitakusaidia lolote unatakiwa usiwe muongeaji sana maana naona unaanza kutoboa matundu ya hela wakati huo ukiwa umewekwa kwenye mtego mgumu na mzito sana wa ilani yenye kurasa 300 ya kutekeleza miradi yote iliyoko kwenye ilani.

Yaani kumbuka sasa hivi hauko kwenye meli mpya uko kwenye meli ileile sema tu imepata mawimbi katikati ya safari.

Mama nimekushangaa sana unaposema kuna miradi mingine iko kwenye makaratasi wakati wewe na Hayati Magufuli ndio mliotembea nchi nzima kuinadi kwa hiyo tunataka ahadi zilizoko kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Tofauti na hapo hatutakuelewa tutanyima kura 2025 kama ukitaka kuomba ridhaa ya kugombea tena.

Jitahidi sana kwenye suala la kodi usiwalaumu tu TRA waonye hata wafanyabiashara pia maana ni wakorofi.

Mama shikilia hapo hapo:

1. Kodi za dhuluma NO!
2. Miradi isiyo na faida tupa kule.
3. Mafisadi bila kujali sura zao, sukuma ndani.
4. Haki huinua taifa.
5. Hii ni awamu ya sita na dereva ni wewe.

Hiiiiii bagosha!
 
Mama Samia achana na cheap popularity haitakusaidia lolote unatakiwa usiwe muongeaji sana maana naona unaanza kutoboa matundu ya hela wakati huo ukiwa umewekwa kwenye mtego mgumu na mzito sana wa ilani yenye kurasa 300 ya kutekeleza miradi yote iliyoko kwenye ilani.

Yaani kumbuka sasa hivi hauko kwenye meli mpya uko kwenye meli ileile sema tu imepata mawimbi katikati ya safari.

Mama nimekushangaa sana unaposema kuna miradi mingine iko kwenye makaratasi wakati wewe na Hayati Magufuli ndio mliotembea nchi nzima kuinadi kwa hiyo tunataka ahadi zilizoko kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Tofauti na hapo hatutakuelewa tutanyima kura 2025 kama ukitaka kuomba ridhaa ya kugombea tena.

Jitahidi sana kwenye suala la kodi usiwalaumu tu TRA waonye hata wafanyabiashara pia maana ni wakorofi.
Pole sana ni kweli miradi mingine haikuepo kwenye budget mfano chato airport, manunuzi ya ndege
 
Back
Top Bottom