Ndugu yangu ni mapema mno kuweza kumuhukumu Raisi aliyekuwepo madarakani kama anafaa au hafai. Kwa maoni yangu mama Samia anatosha kabisa kuwa mkuu wa nchi, kwanza mama Samia alikuwa makamo wa raisi hivyo ni tosha kuwa uraisi kwake si kitu cha kujaribu kwani amekuwa makamo wa raisi kwa miaka mitano ya mwanzo na sasa amekuwa raisi kamili. Mama Samia ni mstaarabu, muungwana na mwenye khofu na Mungu hivyo usidhani atakuwa anatoa maamuzi ya haraka haraka, hao wenye kugombana ndiyo hao watakaopatana kwani wana kamati zao za maadili hivyo wamalizane wenyewe, raisi ana mengi ya kufanya siyo huo ugomvi wa watendaji wa serikali.Huo ni ukweli ulio bayana.
Ukiangalia na kusikia ya hapa na pale ndani ya muda ambao Rais Samia amechukua madaraka hakika magomvi, dharau na kutuhumiana waziwazi kwenye kada mbalimbali kumetamalaki.
Mfano ni katika Idara mbalimbali za Serikali Viongozi wengi kwa muda mfupi baada ya kifo cha Magufuli waziwazi ama wanatishana kuuana kwa sababu ya maslahi ama wanadharauliana na kuchongeana ili tu mmoja wao aonekane bora dhidi ya mwingine.
Kinachosikitisha hayupo yeyote anayewakemea ama kuwaadhibu. Mamlaka za wagomvi wale zipo kimya jambo ambalo katika Utawala uliopita kamwe wajinga wale wasingevumiliwa.
Kwa muktadha huo naliona mapema sana anguko la Samia.