Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Nilidhani mimi tu sielewi, kumbe tuko kadhaa. Mama wa mipasho ni anaimba halafu haijulikani anaimba nini. Tumepatwa.

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Nilidhani mimi tu sielewi, kumbe tuko kadhaa. Mama wa mipasho ni anaimba halafu haijulikani anaimba nini. Tumepatwa.

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
Mkishaongozwa na wala pweza sijui ngisi wa nazi.. Mnaishi kiswahili swahili tu kujifanya wastaarabuuu... wajanja wa mjini.. but nothing will be serious zaidi ya maneno mdomoni.
 
Mwenye post 348 na 1210 sijui kama alisahau kubadilisha simu akajikuta anatumia ID moja au ni purposely?
 
Utamnyima kura peke yako lakini Watanzania halali watampa,vitisho vya nini??
 
Wale tuliokua tunawaita nyumbu naona sasa ndo wako na mama. Maneno yao ya kejeli na ushabiki tu. Kinachonisikitisha hakuna chama cha upinzani serious ila kama kitakuja kuwepo ntakupigia kura za hasiraaaa
Usukuma usukuma sasa basi.
 
 
Nimeanza kupata wasiwasi haswa pale anaposoma hotuba, hotuba zake, tones ya sauti yake inaonekana kama inayovizia wasikilizaji, inaonekana ya mtu aliechooka na kama haitoshi ina kapresha fulani hivi, kapumzi cha kuhema, pengine ni unene alionao au hofu.

Japo anajisifu kuwa anafuata nyayo za Rais aliefariki Marehemu Magufuli na kuyatekeleza yale yote aliyoyaacha Marehemu, nakaribia kuapa kwamba hilo haliwezi hata azikiri...!

Magufuli alikuwa na uthubutu wa papo kwa papo na hata akiwa mbali, halazi damu kwa wazembe wa mchana kweupe. (Alikuwa na kasoro zake nyingi tu, ila alikuwa anajua kusimamia uchapa kazi).

Huyu Bikashoo nahisi anaona watu wako poa na kila akiitwa mama ,anasahau kama anavishwa kilemba cha ukoka. Mpaka sasa kuna mambo yameshaanza kupwaya, bado nasubiri kuona uchapa kazi wake, ila kwa sasa naona ni mtu wa mikutano wa kupenda kuhudhuria huku na kule akitoa hotuba na matangazo.

Rais Samia bado hajaonyesha uwajibikaji wa aina yoyote ile ,yupo yupo tu ,labda tusubiri mwezi wa ramadhani uishe, hayo ya kupanga Mawaziri ,makatibu ndani ya srikali na ndani ya Chama chake,si ya kushitua ni yao hayo ,na yeyote aakiipata nafasi hiyo ,hayo anaweza kuyafanya kwa mwembwe kuliko zake.

Ni jambo gani mwananchi anaweza kusema hili limefanyika kutokana na amri au uongozi wake,mimi sijaona kama yupo alieona atuwekee, spika amewaumbua askari polisi na kimeeleweka anachokisema, japo nae hana jema hata moja.

Tanzania haitajengwa kwa hotuba nzuri zilizosheheni ahadi.
 
Ogopa sana mtu ambae anapenda kuongea maneno matamu na anaeyependa kumfurahisha kila mtu... watu wa aina hii hawana msimamo na ukikosa msimamo kila mtu utajikuta unafata ushauri wake na mwisho kama ni dereva mtajikuta mpo mtaroni.

Inakwenda miezi 3 niambieni ni kitu gani cha maana ambacho huyu mama amefanya ktk mavitu yote aliyoongea nitajieni kimoja tu. Ila kwa vile wanaopiga mapambio ni wengi watu hawaoni udhaifu wake ila soon mtaona baada ya pombe ya kusifu na kuabudu kuisha kichwani.
 
Inaonekana umeanza kukua nyakati za hayati Magufuli inaonekana enzi za Mkapa na JK ulikuwa bado huelewi maana ya urais na namna gani Rais anafanya kazi.

Kosa lako linafanywa na wengi, kuamini kuwa ni lazima Rais Samia afanane mia kwa mia na hayati. Hakuna ulazima huo kila Rais ana vipaumbele vyake, ana hekima yake inayojitegemea na anayo haki ya kuwa yeye kama yeye.

Ondokana na dhana potofu ya kufananisha marais.
 
May 31 ikigonga hakuna jipya kiuthabiti kabisa kwenye angalau lolote katika haya:

1. Ripoti ya CAG BOT na TPA
2. Ripoti ya tume kuhusu Corona
3. Hatua zilizochukuliwa kuhusiana na ripoti za CAG
4. Genge lile pendwa lilotaka kujimilikisha nchi kinyume cha utaratibu.

Mzima mzima atakuwa kasema mwenyewe kama anayaweza au ndiyo hivyo tena.
 
JPM ameshaondoka duniani ameshakuwa sehemu ya historia.

Cha muhimu mpe muda Rais wako afanye kazi. Yule ni Rais wa nchi sio admin wa group la whatsapp la chuo au la mliosoma wote shule ya msingi.

Kile ni cheo kikubwa sana, matunda ya kazi yake hayaonekani ndani ya mwezi mmoja au miwili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…