Nimeanza kupata wasiwasi haswa pale anaposoma hotuba, hotuba zake, tones ya sauti yake inaonekana kama inayovizia wasikilizaji, inaonekana ya mtu aliechooka na kama haitoshi ina kapresha fulani hivi, kapumzi cha kuhema, pengine ni unene alionao au hofu.
Japo anajisifu kuwa anafuata nyayo za Rais aliefariki Marehemu Magufuli na kuyatekeleza yale yote aliyoyaacha Marehemu, nakaribia kuapa kwamba hilo haliwezi hata azikiri...!
Magufuli alikuwa na uthubutu wa papo kwa papo na hata akiwa mbali, halazi damu kwa wazembe wa mchana kweupe. (Alikuwa na kasoro zake nyingi tu, ila alikuwa anajua kusimamia uchapa kazi).
Huyu Bikashoo nahisi anaona watu wako poa na kila akiitwa mama ,anasahau kama anavishwa kilemba cha ukoka. Mpaka sasa kuna mambo yameshaanza kupwaya, bado nasubiri kuona uchapa kazi wake, ila kwa sasa naona ni mtu wa mikutano wa kupenda kuhudhuria huku na kule akitoa hotuba na matangazo.
Rais Samia bado hajaonyesha uwajibikaji wa aina yoyote ile ,yupo yupo tu ,labda tusubiri mwezi wa ramadhani uishe, hayo ya kupanga Mawaziri ,makatibu ndani ya srikali na ndani ya Chama chake,si ya kushitua ni yao hayo ,na yeyote aakiipata nafasi hiyo ,hayo anaweza kuyafanya kwa mwembwe kuliko zake.
Ni jambo gani mwananchi anaweza kusema hili limefanyika kutokana na amri au uongozi wake,mimi sijaona kama yupo alieona atuwekee, spika amewaumbua askari polisi na kimeeleweka anachokisema, japo nae hana jema hata moja.
Tanzania haitajengwa kwa hotuba nzuri zilizosheheni ahadi.