Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Ndio maana nasema tuelendelee kula mtori nyama tutazikuta chini ila dalili za mvua ni mawingu kiongozi akitoa agizo au tamko linafanyiwa kazi mama ametoa matamko mangapi mpaka sasa hakuna lolote lililofanyiwa kazi? Haya subirini wave ya India hii hamtoki
 
Samia sio Magufuli. Kwanza kubalini hilo. Magufuli kuongoza nchi kwa hii miaka 5 mnataka ndio iwe template ya urais wa Tanzania!!

Viongozi hawajawahi kufanana, huyo unayemuona ni mfano wa kuigwa kuna watu walikuwa wanaombea asiwepo madarakani for another day. Unayoita udhubutu kuna watu walikuwa wanaona ni uharibifu tu. Kuamini kwamba uongozi ni kufoka na kujifungia Tanzania huku ukigombana na kila nchi na taasisi za kimataifa ni ujinga. Kama Samia hakufaa, kwanini shujaa perfect alimuweka pale?
 
SN.BARRY
Povu la nini? Ndo uhuru wenyewe,Mpe elimu tu ya kutosha sio kukimbilia kutukana haisaidii,watu kama hawa wanapaswa kupewa elimu!
 
Una uhakika upi kuwa maagizo hayo hayajafanyiwa kazi?.

Tutulie tu hii ni Awamu ya sita.
 
NDUGU ZANGU MTANIKUMBUKA
 
Yaani asubuhi yote hii unaamka na hangover kwa mama? Wacha ujinga mwamba! Mama mbona kazi anapiga fresh tu? Mlizoea kututukana nyie Wasukuma kila uchao! Tukubali tu kwamba Jiwe limefamba na hatutaliona tena!
 
kwanza technically ni miez miwili. second nakushangaa unapima urais in two month eti nn kafanya?
ni mapema sana
 
Kwa mujibu wa uharo wako kuchapa kazi ni kutumbua watu🥺🥺🥺🥺🥺.

Duuuuuuhhh , kweli Afrika bado tuna safari ndefu.

Kwa Wazungu uchapa kazi ni kusimamia haki na utu kwa wanadamu ila kwa nyie wasukuma kuchapa kazi ni kutekana, kuuana, kudharauliana, kuchota pesa hazina na kupita kuhonga wapinzani, kugawa vyeo kwa uswahiba and so.
 
ivi mzee ccm kuna mtu wamaana ujuwe ccm huu sasa ni mwaka wa 60 wanatawala hivi kuna la maana umeliona bro.
 
Mama atafeli akitaka kupendwa na Kila mtu,watu Wana uchu wa pesa na Mali ndo Mana Kila mtu anataka lake litimie.
Awe makini Sana Hapo,Si wafanya biashara,wafanyakazi,wanasiasa,wanaharakati,ajira mpya,madaraka pamoja na nchi za nje.Wote wanataka kutimizwa ya kwao.
Miluzi mingi hii itamponza achague Cha kuanza nacho Kisha aende mdogo mdogo.

Zaidi ya yote akae mbali Sana na kikundi Cha kikwete maana kilikataliwa na wananchi muda mrefu sana kiasi hata wanachama wa CCM walikua wanaona aibu kujitanbulisha mbele ya jamii.
Awafuate usalama wa Taifa wamsaidie kuunda team yake kuliko kuunda team kwa msaada wa JK.
Nafikiri ameshaskia Sasa wananchi wananong'ona kuhusu JK na team yake jinsi wanajisogeza kwa kasi zaidi,atemane nao kabisaaaa Bora ashirikiane na Hussein mwinyi Wa ZNZ anaijua Zaid Tanzania bara na Nani wa kuteuliwa na Nani asiteuliwe.

All in all mzigo Ni wake ukimuelemea aibu Ni yake
 
ni heri tuishi kwa matumaini kuliko hofu.....ni heri tuishi kimasikini kuliko ndugu zetu wapotee na wemgine wapate ulemavu kisa kuhoji.
 
Ametumbua yale majizi yaliyokuwa yanalindwa na jambazi kuu ....

Bashiru, lile la Bandari, yale ya TASAC, lile la Posta... yote kayafutilia mbali...

Yaende Chattle yakasujudu kaburim la mungu wao...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…