Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Kuna nn kwan? Sometimes tuwe waelewa yaan hana miezi sita tayar wakuda washaanza mara hawezi mara hivi. Ok bas arudi anaeweza, OVER!
 

Tatizo la Tanzania ndio hili
Yan kila mtu anauwezo wa kuisema the way anataka taasisi ya urais!

Ww ujui kuwa urais ni taasisi?
 
Ni mapema mno...let us give her time ...
 
Kumpima Mtu ambaye hata tu Siku 30 ( Miezi Miwili ) Ofisini ( Ikulu ) hana si tu ni dalili ya Upumbavu bali pia ni Roho Mbaya ya Kichawichawi.

Hivi 'Logically' Rais Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan angekuwa 'incompetent' angekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Hivi kweli Mtu ambaye amehudumu katika Siasa za Tanzania ( akiwa ndani ya Chama Tawala ( CCM ) kwa zaidi ya miaka 26 na ameshika 'Nyadhifa' mbalimbali za Uongozi nchini Visiwani na Bara leo unaweza kusema hafai Kuongoza na kuwa Rais?

Baadhi ya Watanzania tumezidi sana 'Nongwa' yaani kila Rais wa nchi hii akipatikana ni lazima tu 'tutamchokonoa' kutafuta Mapungufu yake ( hasa ya Kiubinadamu ) utadhani Sisi wengine tulioko huku nyuma ya hizi 'Keyboards' tumekamilika 100% kama Malaika wa Mbinguni.

Yaani Mama wa Watu 'mnamuandama' kwakuwa tu ni Mwanamke na Kiasili 'Haiba' yake ni ya 'Upole' tofauti na mlivyomzoea 'Mbabe' na 'Mkorofi' wenu?

Sasa kama Wewe unaona Rais Mama Samia hawezi Kuongoza vyema na kuwa Rais umtakaye Wewe kwanini Usijitokeze na Ugombee Wewe au uwashawishi Wajomba zako au Baba yako Mzazi atuongoze? Mnakera sana 'Fools: wachache nyie.

Na Wewe bila kuficha unaonekana ni Team Pro - Hayati na huenda ulikuwa ukifaidika nae 'Kimfumo' na sasa Mama ( Rais Samia ) kaingia ama amekutoa katika 'Ulaji' wako au unahisi kwa aina ya Roho Mbaya yako na 'Unafiki' uliokutukuka anaenda Kukutoa hapo na kurejea katika 'Umasikini' wako unaostahili kuwa nao.

Kama nyie 'Fools' wachache hamumuelewi na hamumpendi Rais Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan basi tupo Sisi akina GENTAMYCINE tunaompenda ( bila Kufaidika na chochote Personally ) kutoka Kwake na tuna Imani nae Kubwa tu pia katika huu Uongozi na Utawala wake.

Mwacheni Mama aandike Kitabu chake.
 
Aisee Maghufuli amekufa na hatarudi tena amini hilo. Pro Maghufuli mna shida sana. Mlitaka atawale maisha. Haikuwezekana , Leo kila moja mnamuona hafai. Nenda Chato. Ingawa hata mama Janet ameshatokako.

Pia ujue kila mtu ana namna yake ya uongozi . Na kama huamini ingia kwenye 18 zake . Uje ulete mrejesho .
 
Ili itakuwa Ni genge la BPS, mama ahakikishe analivunjilia mbali hili genge, other wise litamkwamisha Sana.
Kusifu na kuabudu philosophy za mwendazake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Urais ni taasisi bwashee, tumpe ushirikiano atatuvusha....
 
Ulipokosea ni hapo pa 'mbabe' na ' mkorofi' wenu...inaelekea ulikuwa humpendi huyo 'mbabe' na 'mkorofi' na huyu naye inaelekea hampendi 'mpole'..ngoma draw
 
Nakubaliana na wewe, ila kumbuka kauli na matendo ni vitu tofauti, na neno " kazi iendelee" haimaanishi atafuata ya Magufuri. Mbona huoji alivyotamka kufungulia uhuru wa vyombo vya habari na kila raia anaongea atakalo, wakati wa Magufuri nani alikuwa na uwezo wa kuongea atakalo?
 
Nafikiri kila raisi anapoingia madarakani anakuta nchi ina changamoto furani hivyo inabidi adili na hiyo changamoto

Tanzania aliyoikuta JPM ilihitaji afanye alivyo fanya na hasa lile la kutumbua maana alikuta watu waliobweka kstika nafasi zao na kuifanya hi nchi kama Mali yao ( wazee wa vijicent) hivyo JPM ilikuwa lazima afanye alivyo Fanya ili nchi ikae katika mstali na kweli walinyooka wazembe, mafisadi na mabeberu

Wazembe wameshaisha, mafisadi wameisha na mabeberu walisha nyooka mwacheni mama sasa angalie nyanja nyingine
 
Ngwanabukililo,umelielewa swali mwandishi aliloliuliza?, kama wewe unalojibu lake,mpe,
 
Hapo kwenye uhuru wa vyombo vya habari sio vyote bado kuna mkanganyiko wa baadhi wanatoa malalamiko wao hawajafunguliwa.
Kama umwsikikiza jana msemaji wao jana kwenye maadhimisho ya siju ya uhuru wa vyombo vya habari bwana balile hili swala aliliongelea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
suala la maji unauhakika halijafanyiwa kazi jadi sasahivi?
 
Labda tume kuhusu corona,japo kuunda tume na kuwajibika ni vitu viwili tofauti,hayo mengine yoote ni ablakadabra
 
Sawa nakubali lakini tumpe muda kwanza, kumbuka Rais wa Nchi ana mambo mengi sana na kila zuri na baya yote ni yake, utekelezaji wa maelekezo unaweza kuwa na changamoto pia. Nafikiri mama atalisikia hilo la msemaji wao na yataisha tu kuwa na amani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…