Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Kuondoa retention ya 6% kwa wakopaji wa loan board, kutangaza ajira, promotion,
 
Ataweza kuiongoza JK yupo
 
Labda tume kuhusu corona,japo kuunda tume na kuwajibika ni vitu viwili tofauti,hayo mengine yoote ni ablakadabra

Tunampima hatua kwa hatua. Kwanza tuzisikie ripoti hizi. Kisha tuone hatua zinazofanywa.

Kumbuka #1, #2 na #3 zinawahusu pia #4.

Benefit of doubt. Tunampa muda.
 
Unaona hatareee hii ? Kama uhaki utaonywesha Chama hicho alichokuwemo kilishaanguka zamani,na ushahidi mzuri ni Zanzibar na zaidi mkowa wa pemba,tuliache hilo.
Si kila mkuu wa jeshi anaweza kuwepo front line hata awemo jeshini kwenye vikundi mbalimbali,front line ni jambo lingine kufa au kupona,kuna Raisi amefariki hivi karibuni akiwepo kwenye vita dhidi ya waasi ,sio wale vita imeisha eti ndio anakwenda mstari wa mbele na mipicha kibao ,turudi kwenye mada.

Kuuliza si ujinga na maendeleo hayana Chama...sawasawa..., Rasi Samia ameingia kwa jazba na kuwaaminisha wengi kuwa anaweza,ripoti ya CAG na yaliojiri BOT yanachemka juu ya mabega yake ,sasa kimya kimekuwa kikubwa,pengine hakujua matokeo yatamgusa aliemteua au aliowateuwa,hatuwezi kujua.

Tunaona amecheza drafti kupanga kete anavyohisi yeye atashinda, kunapotolewa maagizo halafu ukaona kimya na hakuna haua wala update basi ujue hapo kuna tatizo la piga tajame.
 
Ulipokosea ni hapo pa 'mbabe' na ' mkorofi' wenu...inaelekea ulikuwa humpendi huyo 'mbabe' na 'mkorofi' na huyu naye inaelekea hampendi 'mpole'..ngoma draw
Ila mkorofi hapana [emoji16][emoji1787]
 
Sawa nakubali lakini tumpe muda kwanza, kumbuka Rais wa Nchi ana mambo mengi sana na kila zuri na baya yote ni yake, utekelezaji wa maelekezo unaweza kuwa na changamoto pia. Nafikiri mama atalisikia hilo la msemaji wao na yataisha tu kuwa na amani
Tuko pamoja bwashee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe tangu mama aingie madarakani miezi yote iyo umefanya nini cha maana mpaka sasa tuanzie hapo kwanza
 
WaTZ au WANANCHI; tumekuwa na tumeshazoeshwa KUPEWA kiongozi mmoja baada ya mwingine kwa MFUMO uleule, watu walewale, na porojo zilezile!
MFUMO huu nguvu zake zinatokana na jamii iliyogawanywa katika MAKUNDI makuu machache:

1. WATAWALA; wenye mamlaka serikalini, ndani ya CCM, mahakama, ktk BUNGE na vyombo vyote vya ulinzi na usalama.

2. WANANCHI; ambao kwa faida ya WATAWALA:

a. Wamegawanywa ktk vikundi visivyo na mwelekeo:
'wazee', 'vijana', 'wanawake' wafanyabiashara wadogo na wajasiriamali; na wafanyakazi ambao pia kupitia vyama feki chini ya TUCTA hawana mwelekeo, pia wanachama na wasio wanachama wa vyama vya siasa; wote wamenyamazishwa! Pamoja na wanaojiita watetezi wa haki za binadamu kupitia viji-NGO feki.


2. WANANCHI hawa kupitia vikundi tajwa hapa juu, hawana mamlaka kwa maana ya sanduku la KURA, (wameporwa SAUTI zao kupitia MFUMO).

Kwa neno 'MFUMO' namaanisha vitu viwili: Katiba ya JMT/1977 yenye (matundu), mianya ya UDIKTETA, na WATAWALA wenyewe kama nilivyowaainisha hapa juu; ambao wapo kwa madhumuni ya kulinda na kuutetea MFUMO na usalama wa mslahi ya kundi lao.

HAKUNA uwezekano wa kuubadili MFUMO kidemokrasia hata kwa namna yeyote. Ndiyo maana tunaona 'maigizo' ya kina Nyarandu, Dr. Slaa, Lowassa na wengine kila kukicha. Hayo si maigizo ya kujitakia tusiwalaumu.

Ila tukumbushane:
The hallmarks of bad governance:
1. Ambiguousness,
2. Arbitrariness,
3. Capriciousness.
 
Aisee mi sijakuelewa, anayeweza yuko?. Mi ni nachojua na kukiona mpaka sasa ameweza na anaongonza nchi.

Kila awamu au kila kiongozi wa awamu husika lazima kuna mambo yataenda vizuri na kuna mambo hayawezi kwenda vizuri!.

Mfano huyu mama ameweza kuundoa hofu miongoni mwa wananchi yaani ule uhuru wa kujieleza tunaanza kuuona kwa mbali ukirudi, wakati mtangulizi wake uhuru huo tulikuwa tunaona unapotea taratibu na watu walikuwa wamejaa hofu na kulikuwa hakuna wa kusema!. Mi kwangu hilo naweza kusema mwendazake kuwa hakuweza kuongoza!.

All in all niulize, je twaweza kusema Mwalimu nyerere aliweza kuongoza nchi hii?, je Mzee Mwinyi aliweza kuongoza?, je Mzee Ben aliweza kuongoza?, je Mzee Jakaya Kikwete aliweza kuongoza?, je Mzee Magufuli aliweza kuongoza?.

Hivyo itoshe kusema kila awamu ya uongozi wowote lazima kutakuwa na mazuri na mapungufu ya uongozi husika. Mama nae ameweza kuongoza ndio maana unaona mambo yanakwenda.
 

Hata kichaa Lissu alisema tutaokota maiti barabarani kwa wave hiyo ya India, mbona hata yeye hajatuokotea hata maiti moja?? na wewe na machadema wenzako wave ya India ikipita mniokotee maiti moja mtaani tuone basi!! wacha kututisha!!!
Wee mpumbafu na spika wako kila siku unamuota lissu tu vp unamtaka
 
Hivi unajuwa kuwa report ya CAG hata bungeni halijajadiliwa ?!. Na Bunge ndiyo yenye kuielekeza serikali nini hatua za kuchukua kufuatia report Ile. So usiwe na haraka kama kijana wa balehe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…