Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Mazimu wa Magufuli bado unawatesa wengi.
Ndo mjue mkichagua rais mnachagua na makamu
 
Mkuu kwani we ulitaka nani aongoze?
Kitu kama kizito unabwaga manyanga usisubiri mpaka kikuvunje mgongo, ni vyema kama hawezi asilazimishwe wala asijilazimishe ,kuliko kuanza kuweka ahadi ambazo zitamgarimu na likitota atatupiwa yeye mzigo ya kwamba amevuruga,aweke tume huru nzuri aweke katiba mpya nzuri kisha ajiuzulu,ingetosha ,watanzania wazito hasa waTanganyika hawabebeki.
 
Mkuu wa nchi sio kocha!
 
Akishajiuzulu ,unapendelea msukuma gani aje aongoze?
 
Watanzania mnapenda rough Sana,kuongoza watu sio makelele,sio kujinadi ila kuongoza ni kujenga kwa haki ..tusonge mbele tuache uzamani
 
Rais wetu si mtu wa mihemuko na kupiga kelele huku watu wapiga/wanaiba mali ya umma kama urithi wa baba na wajomba zao. Unaulizq amefanya nini ?? Ndani ya muda mchache ameondoa 6% VRF kwa wanufaika wa bodi, ameshusha mpaka 8% PAYE kwa wafanyakazi maskini, anahakikisha wastaafu wanapewa stahiki zao halali ndani ya muda, anapandisha madaraja wafanyakazi wote wanaostahili na kulipa malimbikizo, ameondoa uozo na wizi bandarini na kuweka mchwa/wapigaji/wezi wa mali ya umma kizuizini, huku kesi zao zikitokota na muda wowote watapandishwa kizimbani na hatimaye kuzitapika mali zote za umma walizokwapua, ndani ya siku chache amesimamia maslahi ya TZ ktk bomba la mafuta la hoima EACOP na kuhakikisha mkataba unasainiwa, mkataba uliosua sua kwa muda wa miaka wadau wakijivuta vuta. Hayo yote ameyafanya ndani ya muda mfupi .
 
.sukuma gang
Matumizi ya haya maneno ni sumu kwa umoja wa kitaifa.

Bahati mbaya yawezekana unalitumia bila kujua wabaya wa nchi yetu wanakufurahi ama unajua kuwa upo kwenye payroll ya wabaya wa nchi yetu!

Maneno ya namna hii yatawatafuna, na kuhakikishia hili.
 
Genge lile pendwa lilotaka kujimilikisha nchi kinyume cha utaratibu.
Ebu nitonye what happened, akina Bashu? Lepolepo?
 
Hapo ndipo unapobakia kufungwa tun'fungwa lakini chenga tun'walaa.
Nisikie nauli za ndege zimeshuka,nauli za meli zimeshuka,treni ,mabasi, mchele,maharage,sukari na vitu kadhaa vimeshuka bei ,utazidisha mishahara mpaka mamilioni ila kama hakuna unafuu itakuwa anachota maji kwa kutumia pakacha.

Hapa Vietnam kila kitu kipo ila bei zao zinatisha ,shati milioni mbili na Tz ndipo tunapokimbilia huko. Eti mshahara utapandishwa ukipandishwa unaupeleka wapi ,mnasifiwa mzunguko wa pesa utakuwewpow , hivi mnafahamu mnachosikilizishwa ?
 
Soma tena ulichokiandika, huwenda upo katika hali ya hasira ama msongo wa mawazo. Ni hivi ndani ya siku 60 hivi, ukitegemea muujiza wa bei za usafiri na chakula na mafuta kushuka ghafla utakuwa hasa hujui unachokitegemea, mwendazake alikaa madarakani miaka mingapi ? Hayo unayoyasema yalipatikana ? Kama hayakupatikana unayategemeaje ndani ya siku 60 za Rais Samia ? Hatuwezi kuwajibu kuhusu madai kua rais samia anahema kwa uoga maana tunajua mnajifurahisha ma hata nyinyi mnajua mnajifurahisha tuu.
 
SUKUMA GANG LA AKINA MNYETI MPO HOIII , POLENI SANA
 
Looo, sijapata kuona mtu anajikanyaga kama wewe. Hebu tuanze na kulinganisha sentensi zako hizi mbili: Awali umesema :
  • Nimeanza kupata wasiwasi haswa pale anaposoma hotuba, hotuba zake, tones ya sauti yake inaonekana kama inayovizia wasikilizaji. Na mwisho ukamalizia na:
  • Tanzania haitajengwa kwa hotuba nzuri zilizosheheni ahadi.
Yaani mwanzo umetilia wasiwasi usomaji wa hotuba zake kana kwamba Hotuba ndio kigezo muhimu sana cha kumtambua Rais mzuri au la. Na mwisho unahitimisha kwa kuweka bayana kabisa kuwa hotuba nzuri sio ndio itayoijenga Tanzania.

Kwanza tuwekane sawa kabla hatujaendelea unachohitaji wewe ni vitendo au hotuba nzuri?

Unajazia kwa kumtaja Magufuli kama ifuatavyo, nanukuu "Magufuli alikuwa na uthubutu wa papo kwa papo na hata akiwa mbali, halazi damu kwa wazembe wa mchana kweupe. (Alikuwa na kasoro zake nyingi tu, ila alikuwa anajua kusimamia uchapa kazi). Jitafakari uandishi wako, kwani sijui kama unataka kusema kuwa Magu alikuwa mzuri ktk hotuba yake na utendaji au vipi? Hiyo kasoro ilitokea ktk nini?
 
Sina hasira nina usongo,ahadi na mabango aliyoingia nayo yametoweka au yanatoweka kwenye thin air. Mbona kuna mabadiliko ameyafanya ndani ya siku hizo sitini ? Mvinyo anaokunywa ukianza kufanya shughuli zake aka kulewa madaraka .

Mimi Nimeuliza tu ataweza mbona hizi ahadi mbili tu zilizotokana na mkaguzi na yeye Raisi kuzivalia njuga, ghafla bin vuwm kimya kama siye ? Wala hamtaji tena mkaguzi wala mpekuzi wa mahesabu. Tunajua muda upo siku mia Raisi anatakiwa ajilabu,japo kufanyia kazi hili alilolikwaa la mkaguzi wa mahesabu.
 
Sijui kama unaelewa unachokiongea, maana unajichanganya mno, sasa kama yapo mabadiliko ndani ya siku 60 ulichokuwa unasema ni nini ?? Mwendazake kakuta sukari, mafuta, unga na nauli za ndege na mabasi ulizo sema zikiwa kiasi gani ? Na kaziacha zikiwa kiasi gani ? Iweje utegemee rais samia kuleta maabadiliko overnight? Huo unaita usongo ndio mihemko, na sio usongo ni msongo wa mawazo. Kazi iendelee
 
Jiwe mwenyewe katupoteza kichakani..yaani hapa tulipo hatujui tupo pori gani hasa... Mama anachofanya ni kutafuta walau ka njia njia ili tujaribu kurudi tulipotokea kwanza then tutafute uelekeo mwingine..

total loss, nchi ilikuwa gizani - Mama hana kosa.
 
Inaonekana hata kuongoza familia yako huwezi,asubuhi yote hii kuanza kumsema mama wa watu kwamba hana uwezo!! Shame on you...Fanya kazi acha majungu tena asubuhi yote hii
Huyu rais hana msimamo ukwel lazima usemwe ata mimi sijui anatupeleka wapi, mimi naona giza tu mbele.
 
Dah, mkuu wasukuma wamekufanya nini mbona umejaa sumu hivyo?.
Achana na lofa huyo me huwa najiuliza kwanini watu wa kanda fulani huwa wanachuki na wasukuma sana, ila mimi nawaona wasukuma ni watu poa tu.
 
Ulishamwoma mama akila mahindi njiani au kugawa mapapai? au akienda kuswali anarushwa kwenye vyombo vya habari?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…