Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Wai na gwajima mkamfufue,wenzio washaenda
 
Sas a hivi Wafanyabiashara wengi hawatoi risiti za EFD wanatoa za makaratasi kwa kisingizio kwamba mashine ni mbovu. Samia endelea kuwatetea Wafanya biashara wa Bongo huku ukiwaponda TRA, utavuna mabua
 
Rais wetu ,mama Samia ,ulipofanya ziara huko Kenya ,nilitegemea kwamba utawashawishi wakenya waje wafanye uwekezaji.DFI.Ili tuweze kupata kodi,ajira na technology.

Hii ingetusaidia sana kusonga mbele,kwa kuwa tungepata mapato ya kodi,vijana wetu ambao hawana ajira wangepata ajira sasa.

Na ungewambia waje wajenge viwanda hapa Ili tupate technology. Nimeshituka na kushangazwa ,eti unasema unaondoa vibali vya ajira.Ina maana haujui hatuna ajira?Unataka waje huku waajiriwe,na sisi tuwe tunaangalia tu?Unapeleka gesi huko Kenya.Kwanini hukuwambia waje wajenge viwanda hapa Bongo Ili tufaidike .Kuwapelekea gesi ,je umeshafanya cost benefit analysis?

Kwamba wataendelea na viwanda huko kwao,huku hakuna.Tutajenga bomba.Tutatumia gharama.Kwann wasingekuja hapa kwetu?Wapatie gesi hapa kwetu na ajira kwa watu wetu .

Na kodi ingeingia nyingi.Nimeshituka na kusikitishwa sana.
 
Matanga....Daaah! Mbona Mother Kafanya kile inastaili... Mitanzania Akili ni Ndogo sana...Alichokifanya Madam President Ndio unakishauri, Tuliza Bongo please we're in the right direction under Mama's leadership.
 
Mmmm!!wapi alisema kuwa vibali vya kazi amefuta?uhuru yeye ndie amefuta vibali hivyo, kuhusu gesi, ina maana, wewe uganda na zambia wanakuuzia umeme, je wanafanya kosa?nyie pambaneni muwavutie wawekezaji waje wajenge viwanda, duniani kote kama una nishati ya kutosha lakini, lazima uwauzie majirani zako, wale walioko mbali zaidi ndio watakuja kujenga viwanda kwako, sasa kila anayetaka, umwambie eti aje kujenga kiwanda kwako?inaingia akilini hiyo?kwani kenya mbona anawauma sana wakuu?mtu aliyekuzidi , kimaendeleo , kumchukia hakukufanyi umzidi, cha msingi changa karata zako vizuri uone kupitia kwake unaweza inuka vipi, kwa hiyo huyo meko aliyekuwa anasema kuwa umeme huo wa bwawa la nyerere tutakuwa tunauuza nje , je walengwa walikuwa ni nchi gani?, ni majirani zetu au mtauuza CAPE VERDE?, CHINA, AUSTRALIA, mbali huko(hahaa)ili hata wakijenga viwanda ni mbali huko?!!
Kuhusu gharama za bomba hilo nadhani watakuwa wameshafanya tathimini zote, kwani hilo lilikuwa la muda mrefu tu, Meko ndio alikuwa kizingiti, yeye kila kitu anahisi kuibiwa tu, nadhani kwa kutumia bomba hilo pia linaweza kutumika kusambaza gesi kwenye viwanda vyetu vya hapa hapa nchini, kwa mikoa litakapopita kwenda kenya.Duniani kote kuuziana nishati ni jambo la kawaida sana, acheni akili za joka la mdimu"linakaa kwenye mti wa ndimu halili ndimu ila mtu akienda kuchuma ndimu halitaki"
 
Kama tumeshindwa kuleta tija tulipoaminiwa ,acha tujifunze kutoka kwa wenzetu huenda,akili zikatukaa sawa na kuacha uvivu na mchezo pindi tuwapo makazini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…