Rais wetu ,mama Samia ,ulipofanya ziara huko Kenya ,nilitegemea kwamba utawashawishi wakenya waje wafanye uwekezaji.DFI.Ili tuweze kupata kodi,ajira na technology. Hii ingetusaidia sana kusonga mbele,kwa kuwa tungepata mapato ya kodi,vijana wetu ambao hawana ajira wangepata ajira sasa.Na ungewambia waje wajenge viwanda hapa Ili tupate technology. Nimeshituka na kushangazwa ,eti unasema unaondoa vibali vya ajira.Ina maana haujui hatuna ajira?Unataka waje huku waajiriwe,na sisi tuwe tunaangalia tu?Unapeleka gesi huko Kenya.Kwanini hukuwambia waje wajenge viwanda hapa Bongo Ili tufaidike .Kuwapelekea gesi ,je umeshafanya cost benefit analysis? Kwamba wataendelea na viwanda huko kwao,huku hakuna.Tutajenga bomba.Tutatumia gharama.Kwann wasingekuja hapa kwetu?Wapatie gesi hapa kwetu na ajira kwa watu wetu .Na kodi ingeingia nyingi.Nimeshituka na kusikitishwa sana.