Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Wewe tunakujua kuwa ni mpinga maendeleo na utangamano kwa watanzania.

Na uliingia nchini kutoka burundi kuja muvuruga umoja wetu.
JF watu wanajua kutoa makavu jamani.
Makavu laivu bila chenga! Haa haa daah
Mrundi aliyekros boda kagundulika!🤣

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Comments reserved
 
Kapewa chama na serikali ni yake utamwambia nn ndugu. Atakupiga marufuku kwenda kokote.
 
Ingelikuwa kuna mawasiliano na mazungumzo huko kuzimu waendako wafu, basi bila shaka JN & JPM wangekuwa wameinamisha vichwa vyao deileee kwa mshangao wa ghadhabu dhidi ya intentional madudu afanyayo huyu Bi Mkubwa!!!
 
Hiyo ni kusema CCM mumeshindwa kuongoza , kila anayekuja anakuja na visa vyake.
Tunataka katiba mpya na tume huru.
 
Moja,
Mkutano wake na wazee wa DSM: Hapa alisema hawezi kulipa pensheni ya elf sh 30 kwa Mwezi Kwa kila Mzee sababu uwezo mdogo ki uchumi. Ikapita hio.
= Hapa Mama yetu alimaliza vema kabisa hakukuwa na dosari kubwa kubwa.

Mbili,
Uzinduzi wa kitabu cha Mzee Mwinyi: Alimpa zawadi ya gari la chini zuri aina Benz wadau wakisema linagharimu kiasi cha sh 250 milioni.
= Hapa Mama yetu kipenzi kazingua big time. Siku chache kuongea na walalahoi wanaomba bima za Afya ukawajibu huna hela then kesho yake unatoa zawadi ya Benz.

Mwinyi sio mtanzania mnyonge wala mlalahoi. Yule ni Waziri Mstaafu, pia Rais Mstaafu wa Zanzibar na Bara. Anapata stahiki zote zote serikalini. Hajashindwa kununua gari la chini.

Mtoto wake ni Rais, tena yupo madarakani. Hajashindwa kumnunulia Baba yake gari la chini.

Mzee Mwinyi ana marafiki kibao hawajashindwa kujichanga kumnunulia Mzee Mwinyi gari dogo la chini.

Mtoto wake ambaye ni Rais ana marafiki kibao hajashindwa kuchangishana kumnunulia Mzee gari dogo la chini.

Ki ufupi options zote Mzee anazo mkononi mwake.

Tatu,
Mechi ya Yanga na Simba: Ilileta taharuki kubwa mno haijawahi kushuhudiwa. Hizi ni club mbili za soka zenye tension kubwa sana kwenye ulimwengu wa mpira hapa nchini na pengine Afrika kwa ujumla.

Hakuna ajuaye sababu hasa ni nini zaidi ya cycle ya TFF na Wizara.

Hadi navyoandika hapa Mama yetu amekuwa kimya hata hajatia neno. Hii haijakaa sawa, maana wanazi wa JPM watakuchukulia km Rais dhaifu na pia hujali watz na zaidi utaonekana ww ndo ume engineer kuharibu utaratibu wa awali uliopangwa.

Nne,
Kumkabidhi Rais Mstaafu nyumba mpya iliyopo kawe:
Just very few days baada ya kuongea na wale wazee ambao kimsingi tunawaita ni maskini ama wanyonge kwa lugha ya JPM hii haijakaa Sawa ki siasa.

Sasa Twende Damage Control Room:

1. Kuhusu wazee wa DSM acha iende hivyo

2. Benz la Mwinyi: Lifanyike hivi. Ifanyike twist moja ya namna hii: Itengenezwe mpango wa kupitisha donation kwa baadhi ya wenye nazo kwa ajili ya kupata pesa ya kulipia hilo Benz ili kuepuka kugusa pesa za Umma. Hili lifanyike na public iwe aware. Mama sema mm ni mama maskini hivyo nimeomba omba michango tukishirikiane na Mwinyi Rais wa sasa wa Zanzibar tupate tuhela tudogo Kwa ajili ya Benz ili tusiguse pesa za Umma. Hapa mama unachukua point zako 3 muhimu in the eye public.

3. Mechi ya Yanga na Simba. Ongea kwa ukali sana kukemea kukiuka kanuni za soka, na Jambo hili limgharimu yeyote kwenye Wizara huyo anakuwa kama ametolewa sadaka. Then, mechi irudiwe tena baada ya consultation ya hapa na pale. Hapa Mama yetu again unachukua point zako 3 muhimu in the public eye.

4. Hilo la nyumba la JK halijaleta nongwa. Lipite hivyo hivyo.

Kuendelea kukaa kimya kimya muda mrefu kuhusu hili la Mwinyi na mechi ya Yanga na Simba sio nzuri kisiasa. Point 3 zipo nje nje chukua.

Ushauri wengu mwingine: Mama unda Damage Control Team (DCT) iwe inakuangazia masuala Kwa jicho la tatu itakusaidia mno mno mno.

Kuongoza watu ni sayansi ya ku deal na hisia zao tu.

NB: Naomba nafasi kwenye DCT nikusaidie Mama yangu.
 
Yaani unamfundisha aseme uongo aliojitungia mwenyewe!??? Bi Mkubwa ndiye chanzo, mapito na magumu ya nchi. Kumbe Watanzania ni wa kugeuzwageuzwa kama chapati kwenye kikaangio!??? Shame!!!
 
Benzi linagharimu Tshs 250,000,000?

Labda reconditioned au second hand...

Mercedes Benz Brand New kutegemeana na model ina bei kati ya $600,000 na 3,000,000 (kabla ya kodi na tozo zingine)
 
Benzi linagharimu Tshs 250,000,000?

Labda reconditioned au second hand...

Mercedes Benz Brand New kutegemeana na model ina bei kati ya $600,000 na 3,000,000 (kabla ya kodi na tozo zingine)
View attachment 1779262


Itakuwa hawa masponsa wamempatia Bi Mkubwa Ilani tofauti na ileeeeee tuliyosomewa mwaka jana kuwa JPM katwishwa three times mzigo wa muhula wake wa kwanza.
 
CCM ni ile ile ! Huyu anazindua vitabu..

Aliyemtangulia alikua na anapokea jogoo njiani huku akimpa option mleta jogoo kuwa anaweza kumpa mama yake mzazi amuoe...

Mara kutafuna mahindi njiani na kugawa pesa njiani tusishangae maana alisema yeye ni kitu kimoja na CCM ni ile ile
 
Lol, kumbe unajitafutia ulaji? Wabongo acha kabisa !
Yeah, tena nimebadili kabisa na ID. Yaani nipo very determined yaani. Sitaki tena kuchat kijinga kijinga mtandaoni, nachat ki manufaa zaidi na kuonyesha potential yangu kwa wanaonifuatilia. Yaani sasa hv nipo ki manufaa zaidi ujinga ujinga tupe kule. Ndio.
 
Samia alitakiwa achukua desa kutoka kwa Johnson alivyorithi madaraka baada ya kifo cha Kennedy. Pamoja na kuwa walikuwa mahasimu wa wazi kabisa waliopingana waziwazi kwenye primaries, ila Johnson alivyorithi serikali ya Kennedy, aliiendeleza na mawaziri wale wale bila kudai kuwa anaanza mambo yake upya mpka baada ya uchaguzi wa 1965 ndipo akaunda serikali yake tofauti. Mama amekuja madarakani na munkali ambao siyo sahihi kwa mrithi wa madaraka. Anafanya kazi kama vile ni mtu aliyepindua serikali iliyokuwapo. Busara kidogo ilitakiwa namna ya ku-approach changamoto tulizo nazo.
 
Najua walalahoi wengi, mama ntilie, wamachinga na wakulima wanahofu kubwa kuwa itakuwaje sasa baada ya mtetezi wa wanyonge kuondoka kiaina. Wengi mpaka sasa vichwa vinagonga na kuhoji. Itakuwaje sasa maana mtetezi wao alikuwa akitoa tamko nchi nzima inatambua kuwa kuna tamko limetoka.

Wamachinga mmeanza kuondolewa barabarani huko Dar, msihofu Mungu yupo.

Wakulima mnamashaka makubwa juu ya dhulma, msihofu Mungu yupo.

Leo hii waporaji na wanyag'anyi wameanza kuinuka alafu Mkuu wa nchi anamuomba Igp kuwachukulia hatua badala ya kutoa amri.
 
Yani aje yupi mwingine? Tatizo mmezoea dezo, the universe is a wicked place, it's a gang world, there is no place for the innocent.

Keep on playing innocent mtakoma mlizoea kujinyongesha mnanunuliwa mapapai tu. Watu tunahitaji zaidi ya mapapai na mahindi ya kuchoma.

Alisema tutahama mjini na hatujahama na mlifurahia sana , sasa nanyi mtahama mjini. Zamu yenu
 
Kweli Mungu ni mwema kusikia sala za Watanzania walio wengi kuukataa unyonge ulioasisiwa na jiwe.
Yupo wapi?
Mama Samia Suluhu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…