Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Timu Chato mnahangaika sana, Kiongozi tumeshapewa na Mungu tayari...wewe subiria ufufuo
 
Timu Chato mnahangaika sana, Kiongozi tumeshapewa na Mungu tayari...wewe subiria ufufuo
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Naona mnakazana kwelikweli kumponda mama Samia.

Mama Samia mpaka sasa amefanya kazi nzuri sana

1. Amesharudisha bei za bando kuwa kama awali

2. Ameshakataa Kodi za dhulma

3. Amefungulia online TV na mazungumzo yanaendekea kufungulia vyombo vingine vya habari

4. Ameshatuondolea riba ya 6% kwenye mikopo, bodi ya mikopo

5. Ametupunguzia PAYE 1%, Good gesture

6. Amefungua wafanyakazi kwenda kupata semina hata nje ya nchi as long as pesa za mafunzo si za serikali

7. Ametoa vibali vya ajira zaidi ya 9000, lengo ni kutoa ajira 40000 mwaka huu

8. Ameagiza darasa la saba walioachishwa kazi kipindi cha uhakiki wapewe mafao yao.

9. Ameshasaini dili la kuuza gesi Kenya, hii itatuletea pesa ndefu za kigeni.

12. Serikali yake imeshatangaza maelfu ya kozi za Ufundi Stadi (VETA) bure kwa maelfu ya vijana wa Kitanzania

13. Kwa kutumia diplomasia amewezesha mahindi yetu kuendelea kupata soko Kenya!

14. Ameshaagiza DPP afute kesi zote za kubambikizia watu

Kwa hiyo acheni, kuanzisha mada nyiiingi za kumchafua Mama, Mama anapiga kszi nzuri so far.

Alichotuzingua so far

1. Ni kuingilia Derby yetu.

2. Kugawa Benzi mali ya umma kama njugu

Lakini overall performace ni Nzuri nampa "A"

Sasa kinachofuata, tunataka kauli na maagizo yake mazuri ayatafutie namna ya kuyaweka kisheria, yaani arekebishe sheria kandamizi maana maneno matupu hata kama ni mazuri vipi hayavunji mfupa!
 
... Mama Samia ni Daudi aliyeinuliwa baada ya Mungu kumkataa Sauli aliyekuwa wakati mwingine akirukwa na mapepo machafu hadi apigiwe kinubi na kijana Daudi!

Kwa taarifa yako Daudi alihudumu katika utawala wa Mfalme Sauli na aliinuliwa kutokea humo humo ndani ya utawala baada ya mzee kuchemka vibaya! Mungu hutenda kazi zake kwa jinsi ya ajabu mno!

Kama kutumwa, Mama Samia katumwa sana kuwakilisha; kwa jinsi ya rohoni ilionekana kabisa kuna makusudi maalumu ndani yake. Yalikuwa maandalizi "kabambe" ya Mungu kumuandaa kwa kazi kubwa! Sasa wewe endelea kusubiri; sisi tuko na Mama.
 
Katika video yake ya wiki iliyopita, Tundu Lissu amesema Mheshimiwa Rais ni Malkia asiyetimiza ahadi zake,ambaye anaongea maneno matamu tu.

Bado hajatoa tamko kusema kwamba katika Katiba zipo Sheria kandamizi ambazo Tundu Lissu ameshaziona. Bado hajawaachilia huru wafungwa wa kisiasa. Tundu Lissu labda hajasikia kwamba Serikali inasema hakuna wafungwa wa kisiasa. Ingawa wanaweza kuwepo sasa kwa sababu kuna basi linatokea Geita linakwenda Dodoma wangu wangu.

Tundu Lissu anasema Rais Samia hajafanya chochote. Na hivyo ndivyo tunavyosema,hajafanya chochote, anarundikiwa sifa, redio zinakukuu maneno yake ya ' hekima'.
 
Dont cry for a little boy.
 
Hivi...? Kwani Raisi wetu Ni mwafunzi wa kuwa anafundishwa tu kazi kila siku bhana??

Mbeligijia atulie sasa!
 
Ameisha mwinua Mama Samia ndo maana umeona amekuwa rais bila kuiba kura
 
Do! kubalini kama mimi ni kweli hatuwezi kulinganisha utendaji wa Magufuli na huyu mama kwa kuwa kila binadamu ameubwa tofauti japo kwa kadri ya imani yangu kila binadamu ameubwa kwa mfano wa MUNGU na ndipo ninapoogopa kumdharau mtu.
mkubalini mama na atafanya kwa kadri ya muda utakapofika ikiwa ni pamoja na kulipa kodi na kuendelea kuwa waaminifu na watiifu wa nchi ambayo kwa sasa inaongozwa na mama.
tujifunze na sisi kufanya na sio kufikira mwingine kafanya nini ikiwa ni pamoja na kutafakari umefanya nini kumsaidia Rais wako ili atekeleze anayoahidi yata kwa kiasi kidogo tu.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚tundu kaanza kuwa sukuma gang
 
We jamaa una uhakika wakulima wana mashaka? Nenda Mtwara na Lindi ukawaulize wakulima na uwakumbushe yaliyopita uone kama utarudi na meno yako yote mdomoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…