Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Huo ni ukweli ulio bayana.

Ukiangalia na kusikia ya hapa na pale ndani ya muda ambao Rais Samia amechukua madaraka hakika magomvi, dharau na kutuhumiana waziwazi kwenye kada mbalimbali kumetamalaki.

Mfano ni katika Idara mbalimbali za Serikali Viongozi wengi kwa muda mfupi baada ya kifo cha Magufuli waziwazi ama wanatishana kuuana kwa sababu ya maslahi ama wanadharauliana na kuchongeana ili tu mmoja wao aonekane bora dhidi ya mwingine.

Kinachosikitisha hayupo yeyote anayewakemea ama kuwaadhibu. Mamlaka za wagomvi wale zipo kimya jambo ambalo katika Utawala uliopita kamwe wajinga wale wasingevumiliwa.

Kwa muktadha huo naliona mapema sana anguko la Samia.
Dhambi ya uchafuzi uliotendeka 28/10 itaendelea kuwatafuna. Ila "tune" ya andiko lako ina vinasaba vya mwendazake.
 
Ziara za nini?
Nyie mnaelewa kazi za Rais kweli???
Hao mawaziri, manaibu, makatibu wakuu,wakuregenzi, wakuu wa mikoa, wilaya, wana kazi gani kama mnataka kuona sura yake kila mahali??
Jiwe aliwazoesha vibaya sana.
Hawa mwendazake alikuwa hasafiri nje ya nchi, ila ndani ya nchi ilikuwa Dar Chato mara 4 kwa mwaka, wanakula miposho ya SAFARI, kuliko hata anayeenda New York.

Bado kutembelea mikoa mingine, mama Rais Samia hajamaliza hata miezi miwili wanataka naye awasafirishe vilevile, watulie wacheze ngoma ka wengine.

Eti miradi ya kimkakati, wanahofu, hawajui hatma ya maslahi yao binafsi, wala hawana interest na maslahi mapana ya nchi.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Inasikitisha sana! Toka achaguliwe hajafanya ziara hata moja kwenye miradi mikubwa ya kimkakati

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Hapa nikumwonea wazi wazi, yaani mtu hata kujipanga vizuri bado aanze na maziara?

Yupo kwenye conceptualization ya vipi aendelee na kwa jinsi ipi kwakua kwanza hili hakulitegemea kama lingetokea na kisha yeye siyo replica ya Hayati, sasa mpaka asome vizuri na kuji align unafikiri mchezo?

Draft yote hii ya uongozi hayakuwa original thinking yake ni kwamba alishiriki na alikuwa katika kusaidia siyo ku originate...Sasa unaachiwa mchoro ambao wewe siyo origin uuongoze kama original unafikiri ni kazi rahisi?

Tuache uonevu, tuwe objective na wenye mtizamo chanya. Tuepuke kumdharau Mh. Rais kwakuangalia gender yake, urais ni taasisi na humo kuna gender zote katika kuliongoza taifa...Tumpe muda, too early kum attack tena negatively!
 
Ni kweli mama Ana uwezo mdogo lakini kama wasaidizi wake wakiwa wazuri Basi hamna shida.

Siku zote wanawake huwa Wana uwezo mdogo ndo maana 99.999% ya manabii Ni wanaume...walioacha legacy Wengi Ni wanaume
Mkuu; "you seem to be gender insensitive". Wanawake wanaweza bila kuwezeshwa.
 
Inasikitisha sana! Toka achaguliwe hajafanya ziara hata moja kwenye miradi mikubwa ya kimkakati

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Uchaguzi ulifanyika lini??
Tokea aingie kikatiba, kikatiba, kisheria.

Hujui hata mambo yanafanyikaje.

Safari za Dar Chato mara 4 kwa mwaka, mkiwa misafara ya magari 50, sasa basi!
Poleni mno! Karibuni kwa wanyonge huku.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Inasikitisha sana! Toka achaguliwe hajafanya ziara hata moja kwenye miradi mikubwa ya kimkakati

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Hill ni jawabu sahahi. Hana interest na hiyo miradi. Anaota mambo yanayo husu taifa la kudemka .
Haijawahi kutokea miradi ikafanyika bila kuitembelea. Tusubiri miujiza .
 
Timu Magu kazini.

Ujue kuna muda wakuzibua watu vibao washtue mzee alishafariki na lazima kukubali utawala mpya.

Hayo ulosema yapo tangu muda tuu sema wakati umelewa mvinyo wa maneno ya Magu ulikuwa huyaoni.. Alafu ule ulikuwa sio uongozi ila ni ubabe.. Mlipendelewa nyie timu kuabudu alafu wengine wakiumia . Sa hivi kibano kimegeuka mnalia.
A lift in CCM ranks in offing?
 
Ushahidi naleta mimi au alete yeye kunithibitishia hajaiba? Unatumia nini kufikiri?
Sasa mnataka aendeleze ya hayati, akiendeleza mnasema kaiba, afanyeje nyie binadamu?

Mpeni heshima Rais wa nchi ni nembo ya taifa letu...Kama tulimlinda Hayati na mama pia ana haki hiyo, tusiwe na double standard...Rais ni mbeba maono wetu akivurunda ni sisi watanzania tumevurunda, nguvu yetu ni yake...Tusimvunje moyo please, Tanzania ni nchi yetu, tuipende tuilinde...Katupa uhuru wa kukosoa lakini siyo kumdhalilisha na kumkosea heshima hii siyo kabisa!
 
Kuna watu uwa wanajisikia kuwashwa washwa makalio pale wanapoona mtu anamponda jiwe wanataka kila mtu amsifie,binafsi siwezi kulisifia jitu lenye roho mbaya,katiri na fedhuli.

DED wa Bumbuli aliyempitisha January bila kupingwa atakiwa na Waziri Ummy kujitathmini kama bado anazo sifa!​

 
Sasa moja kwa moja kwenye mada husika,tangu huyu Mama aingie madarakani nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana mwenendo wake,ingawa kweli ni mapema sana kuanza kumtolea hukumu,lakini nachelea kusema huyu Mama HATUFAI hata kidogo especially kwa wale tunaotaka kuona Tanzania inapiga hatua za kweli za kimaendeleo na sio siasa,

Kwa sasa nisingependa kuongea mengi ila ninachoweza kusema ni kwamba HAJUI Taifa hili linataka nini ili kujikomboa,anaonekana ni mtu wa KUFURAHISHA watu tu,bila kujali hii inchi inaathirika au inafaidika vp na anachokifanya,nauona mtindo wa utawala wa Kikwete ukijirudia kwa kasi sana nchini,

Ni dhahiri mpaka sasa huyu Mama anafanya mambo kwa kupangiwa au kuchukuliwa na upepo tu wa kwenye mitandao ya kijamii lakini yeye binafsi hana mipamgo na maono yoyote ya kueleweka juu ya Tanzania.
Kumbe nchi uongozwa na maono ya mtu na sio taasisi katiba na sheria ilizojiwekea?
 
Nyumbu hamjui maana ya kukopy na kupaste siyo. Magu kwenye vibali hakusema alichosema huyo b mkubwa wenu. Hizo stori za kupunguza mifugo kwa wafugaji ni akili za kimsoga msoga. Kama ulikuwa umepevuka tayari mwaka 2005 utaelewa namaanisha nini.

Pia Magu alianzisha Nyerere National Park ili pamoja na mambo mengine tuilinde Uranium yetu mpaka pale tutakapoweza kuishughulikia wenyewe. Sasa huyu anayesema tuchimbe maana wanyama hawaihitaji ndiye wankumfananisha na Magu kweli!

Acha dharau. JPM mfananishe na JKN siyo hawa wa uhuru wa manyani. Katika vyote alivyowahi kufanya JPM, kosa lake kubwa zaidi ni kumpendekeza huyu timu msoga mwaka 2015.
Tumwombee afya njema ni kiongozi mzuri. Kwake yeye JK ndio alimkaribisha katika maisha ya kiuongozi alipokuja huku Bara.

Ni vigumu kwake kwenda kinyume na mitazamo ya JK . Ni sawa na mchezaji nyota wa mpira wa miguu anavyomheshimu kocha aliyemtoa timu ndogo na kumpeleka Yanga au Simba, hawezi kuja kumsahau hata siku moja.

Sidhani kama kila mkakati wa JK hauifai Tanzania ya leo na kesho. Anaweza kuwa alijisahau na watu wakapiga sana serikalini na ikakosekana heshima lakini bado alikuwa na maono mengi mazuri.
 
Hapo sio sawa, hiyo ni kumpa free ride. Akivurunda awajibike kivyake.
Kama unasema hivyo basi hayati was right kufanya alichoona kinafaa sawasawa na katiba ilivyompa privillage...To every right there is a responsibility kama tunataka asivurunde ni jukumu letu kumpa viable options ili yeye akiacha kuchagua au akachagua vibaya awe responsible, short of that ni uonevu na tunakinbia uwajibikaji kama raia wa nchi yetu.
 
Wewe huna akili,utateseka bure haiwezekani humu kila mtu awe na mawazo kama yako humu kila mtu yupo huru kutoa maoni yake sasa matokeo yake ndio hayo,ila kwa matusi hapa umefika bado kinda sana na nakuambia wazi siwezi kumsifu kwa lolote huyo mbwa wako unayempigania
Tarrtiibu nitakukuza binti hahaa.
 
Hizi ndizo akili zenyewe zinadumaza maendeleo ya mtu mweusi. Ndizo akili ambazo zinaufanya umaskini uendelee kuwepo kwenye mataifa mengine ya dunia ya watu duni.

Mama anaowasaidizi wengi wanaume, urais ni taasisi mkuu. Inabidi uelewe maana pana ya urais kuwa taasisi.

Wanaume watano wameongoza TZ na bado malalamiko yanasikika kutoka kila kona, ngoja Mama apewe miaka hii minne tuangalie wanawake nao watatufikisha wapi.
Nchi sio mahabara.... Its a real staff with real people... Apishe kisitaarabu tu.
 
Nyumbu hamjui maana ya kukopy na kupaste siyo. Magu kwenye vibali hakusema alichosema huyo b mkubwa wenu. Hizo stori za kupunguza mifugo kwa wafugaji ni akili za kimsoga msoga. Kama ulikuwa umepevuka tayari mwaka 2005 utaelewa namaanisha nini.

Pia Magu alianzisha Nyerere National Park ili pamoja na mambo mengine tuilinde Uranium yetu mpaka pale tutakapoweza kuishughulikia wenyewe. Sasa huyu anayesema tuchimbe maana wanyama hawaihitaji ndiye wankumfananisha na Magu kweli!

Acha dharau. JPM mfananishe na JKN siyo hawa wa uhuru wa manyani. Katika vyote alivyowahi kufanya JPM, kosa lake kubwa zaidi ni kumpendekeza huyu timu msoga mwaka 2015.
Alichomekewa hakuwahi mpendekeza... She was there for the purpose, chaguo lake was Dr Mwinyi... But kwa kuwa Msoga aliwahi kutafuna (ndio ukweli) akamguide.
 
Back
Top Bottom