Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Samia Suluhu anafanyiwa Zengwe na hao Die hard Tagaz dawa ni apige chini Wachawi wote apange safu ya watu wapole wenye kupiga kazi kimyakimya bila kutafuta sifa kwa wananchi kwasababu ni wajibu wao
Wajane wa dhalim wana gubu sana
 

image.png

Na Nkwazi Mhango​

Si nadra siku hizi kusikia watu–––hasa wateule wake au wale aliowabakiza kwenye ulaji–––wakimwita rais Samia Suluhu Hassan ‘mama yetu’ ili kumfurahisha na kulinda ulaji wao. Kama tutakuwa wakweli kwa nafsi zetu, je kweli SSH ni mama yetu? Kwangu mimi, SSH ni rais wa JMT basi. Kwanini ninafikiri hivi? Nina sababu zifuatazo:

Mosi, Samia si mama yetu bali rais wetu hasa ikizingatiwa kuwa umama wa taifa haupewi mtu kwa sababu ni rais bali kutokana na mchango wake kama upo. Je tukilinganisha mchango wa SSH na akina Maria Nyerere, mjane wa baba wa taifa au Bi Titi Mohamed, mama aliyepigania uhuru wetu hadi kuathirika kifamilia kwa kuachika na kufungwa tena kwa kusingiziwa kweli tunaweza kusema kwa haki na heshima kuwa SSH ni mama yetu?

Pili, kama ni umama utokanao na urais, inakuwaje watangulizi wake kuanzia Mzee Ali Hassan Mwinyi, Hayati Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na Hayati Dkt John Magufuli hawakuitwa baba zetu? Hapa kuna nini au ni ule udhalilishaji wa mfume dume kama siyo tabia ya kujikomba ambayo ilianza kuota mizizi kwenye awamu ya tano tokana na ukali wa Magufuli? Tulizoea kusikia mke wa Magufuli, mama Janet, akiitwa na walipoende kujipendekeza kwa mumewe wakimwiti ‘mama yetu kipenzi’ sifa ambayo imepotea ghafla baada ya mumewe kufariki na kutokuwa madarakani. Je ni kweli mama Janet alikuwa kipenzi au madaraka ya mumewe? Mbona siku hizi tunasikia akiitwa mjane wa Magufuli bila sifa ya kipenzi kuendelea kutajwa kama kweli alikuwa akipendwa kweli? Je kwanini SSH, ghafla amegeuka mama wa kila mmoja wakati alipokuwa makamu wa rais aliitwa jina lake la SSH? Kunani hapa?

Hata hivyo, hili linahitaji wenye kuona mbali na ndani zaidi. Je hawa wanaomwita SSH mama yetu wanamaanisha hivyo au kujikomba na kumzuga aendelee kuwabakisha kwenye ulaji? Je––kama tutafuata vigezo––SSH anastahiki heshima ya mama yetu ambayo kwa maana nyingine ni mama wa taifa wakati mataifa karibu yote–––tokana na mfumo dume–––huwa hayana mama wa taifa isipokuwa baba wa taifa?

Kwa kujua tabia ya kujikomba inayoendana na madaraka, namshauri rais SSH akemee utapeli huu usiokuwa na sababu yoyote bali kujikomba na kumpumbaza na kumdanganya adhani wanampenda wakati si kweli. Hebu fikiria. Alipokuwa madarakani, Dkt Magufuli alikuwa akisema kila jambo na kuungwa mkono huku waliomzunguka wakimsifia na kujichekesha ilhali walikuwa wanalenga kumtumia na kumfurahisha ili wanusurike. Ukiangalia kwa sasa ambapo wale waliokuwa wakijifanya watu wake walivyomgeuka na kuanza kubomoa mema yake, utajua ninachomaanisha.

Mfano wa karibu ni ile hali ya baadhi ya waliokuwa karibu naye kuanza kutetea bila aibu mambo ya aibu ana ajabu kama vile mradi mbovu wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ambayo Hayati Magufuli alipiga kalam una kutamka wazi kuwa hata mwendawazimu asingeweza kuuruhusu. Mbali na hiyo, rejea kubadilika kwa ghafla kwa wapiganaji wa miamvuli waliotuaminisha kuwa taifa letu lilikuwa hali corona na lilikuwa likilindwa na Mungu kiasi cha kutovaa mabarakoa kwa vile Hayati Magufuli aliyapinga wanavyovaa mabarakoa. Je huu si ushahidi wa unafiki na imani za woga?

Sina ugomvi na kuwepo kwa corona. Je kwanini mliokuwa mmezunguka Hayati Magufuli hamkumshauri au kuachia ngazi pale alipokuwa ameshikilia msimamo kuwa tulihitaji kinga ya Mungu na si barakoa na chanjo?

Taifa letu ni ajabu kidogo. Ilifikia mahali watu wanajua kabisa kuwa walikuwa wakihatarisha afya zao na wengine ilmradi waendelee kuwa madarakani wasijue wangeweza kufa na kuyaacha. Kwa kuzingatia tabia hii ya ajabu na hovyo, namshauri rais SSH asikubali kuitwa mama yetu wakati wanaomuita hivyo wapo wanawake wenye umri mkubwa kuliko yeye ukiachia mbali wanaume wanaoweza kumzaa. Nisisitize. Tuwe wakweli kwa nafsi zetu badala ya kuendekeza njaa na unafiki. Tunawapotosha viongozi na wananchi wetu.

Tokana tabia hii ya kinyonga, nachelea kuwa baadhi ya mambo aliyokataza Hayati Magufuli yanaweza kurejea taratibu kama vile safari za hasara na hovyo za maafisa wa serikali nje, matumizi mabaya, wizi, uzembe na mengine mengi. Rejea kadhia ya hivi karibuni ambapo wadau wa bandari walivyosikika kwenye mitandao wakilalamika kuwa bandari imerejea ujahiri wa awali ukiachia mbali wizi hata ujambazi kuanza kuibuka hata kabla ya Hayati Magufuli hajaoza.

Biblia ina maneno ya busara yasemayo ajikwezaye atashushwa. Pia tuongezee kuwa akubalie kukwezwa asipostahili atashushwa na wale wale wanaompaka mafuta kwa mgongo wa chupa au kumtwisha kiremba cha ukoko. Namshauri rais SSH ajikumbushe kisa cha Yesu siku ya matawi alipoingia Jerusalem akiwa amepandishwa kwenye mgongo wa punda huku wanawake wakitandika khanga zao na wengine matawi ili apite. Je alipokamatwa, watu wale wale walisema? Walisema “asulubiwe” hata bila makosa. Kumbuka.

Kabla––kwa mujibu wa biblia––Yesu aliweza kulisha umati pale alipobadili samaki sita na vipande vya mikate watu wakala na kusaza. Ajabu, baada ya hapo, ni wanufaika wale wale walisema bila aibu wala woga asulubiwe.

Mfano mwingine ni wa Musa. Alipowatoa wana wa Israeli Misri alishangiliwa sana. Cha ajabu, akiwa jangwani njiani kuelekea Kanani, walimgeuka wakakufuru wakisema walikuwa wamechoshwa na mana na pia walitaka wamuone Mungu vinginevyo wangemuua Musa. Mfano mwingine ni wa baba wa taifa. Alipokuwa kitini walimwimbia mapambio, ngonjera na nyimbo zote za sifa. Alipostaafu walimwita ‘Baba aambiliki” wakati walikuwa wakigwaya kumwambia zaidi ya kumsifu hadi wakaja na kile kilichoitwa zidumu fikra za mwenyekiti wa CCM. Je zilidumu au zimeishia wapi baada ya yeye kuishia? Hawa ndiyo wanadamu. Hawana tofauti na ndege kwenye mti wenye matunda. Yakiishia, nao wanaishia bila hata kugeuka nyuma kama ambavyo kwa sasa naona wakimpa kichogo Hayati Magufuli ambaye amebakiza wanyonge wake tu ila siyo wale walioshiba mikononi mwake.

Hii ni kutokana na ukweli kuwa ukiwa na madaraka, ulaji au utajiri na nguvu watakusifia. Zana hizi zikishakutoka waliokuwa wakijifanya kukupenda wanakuponda. Waliokuwa wakikweza wanakushusha na kukushua. Jifunzeni toka kwa Hayati Magufuli na yanayoendelea. Leo sisemi mengi zaidi ya kuuliza tena.

Je kweli SSH ni mama yetu au rais wetu? Je anahitaji sifa hii kweli? Namshauri SSH akatae unafiki na unywanywa wa kutaka kuingizwa mkenge na wasaka tonge na wachumia tumbo ambao wako tayari kucheza ngoma yoyote ilmradi tonge liende kinywani.
 
Tulianza na suala la Vifurushi Rais alikosa msimamo Wakabadili mwelekeo ..

Tukaja na tani moja ya madawa ya kulevya hatujaona wala kusikia hii kesi iko wapi wahusika akina nani na wamechuliwa hatua gn

Tukaja kuzawadiana mibenzi tukio la kustaajabisha kabisa tajiri kama Mwinyi unampaje gari la kifahari lilinunuliwa kwa kodi za wananchi hela ambayo ingeweza kujenga kituamo cha afya..
.
Tukaja suala la mkataba wa gesi bila kueleweka

Tukaja na suala la kuahirishwa kwa simba na yanga

tumeshaanza kushudia mauaji ya ALBINO

Maigizo y Chanjo tunaanza kuyaona


TRA ilizimwa makusudi waibe

TPA huduma zinaenda taratibu

TANESCO nao wako mzigoni
 
Tulianza na suala la Vifurushi Rais alikosa msimamo Wakabadili mwelekeo...
Kuwa na mtazano chanya,ndugu hata kama ni mkwamia awamu yako pendwa. Kukosa kuwa Chanya na kufurahia yasiyo mema inatosha kukuweka kwenye kundi la wanaofanya majaribio ovu. Kwa nini usisaidie kutambua wenye nia ovu, ili tupige hatua
 
Tulianza na suala la Vifurushi Rais alikosa msimamo Wakabadili mwelekeo ..

Tukaja na tani moja ya madawa ya kulevya hatujaona wala kusikia hii kesi iko wapi wahusika akina nani na wamechuliwa hatua gn...
Kitendo cha kuwa huru na kuandika haya mawazo yako inatakiwa umshukuru Mama, unafaham kipindi cha marehemu ungetoa maoni kama haya tungekukuta coco beach kwenye kiroba.
 
Tukaja na mambo ya kutekana kishamba.

Tukaja na mambo ya kuambiana barakoa ni kama titi hivi lililokatwa.

Tukaja na mambo ya kuambiana haya kakaeni na mavi yenu nyumbani.

Tukaja na mambo ya kubambikizia watu kesi za uhujumu uchumi.

Tukaja na mambo ya kutumia pesa za wastaafu huku tukisema hizi ni pesa zetu za ndaniiiiiiiiiiii.
 
Tulianza na suala la Vifurushi Rais alikosa msimamo Wakabadili mwelekeo ..

Tukaja na tani moja ya madawa ya kulevya hatujaona wala kusikia hii kesi iko wapi wahusika akina nani na wamechuliwa hatua gn...
Haya ni mawazo hovyo yanayotoka kwenye kichwa mtu ambae hata samia angefanya nini,bado ungesema hajafanya
 
Tulianza na suala la Vifurushi Rais alikosa msimamo Wakabadili mwelekeo ..

Tukaja na tani moja ya madawa ya kulevya hatujaona wala kusikia hii kesi iko wapi wahusika akina nani na wamechuliwa hatua gn....
Hayo yote hata yakiwekwa pamoja, hayawezi kufananishwa na matukio ya kishetani ya kuteka, kupoteza na kuua watu.

Wala hayawezi kulingana na uovu na uibilisi wa kubambikia watu kesi.

Mungu Baba wa milele, tunakushukuru kwa sababu umetupa nafasi nyingine tena ya kuuona ukuu wako.

Yawezekana tusiwe na pesa mfukoni, lakini tuna utajiri wa amani mioyoni mwetu. Yawezekana tunatembea kwenye barabara za vumbi, lakini tuna furaha mioyoni mwetu kwa kuwa hatuna hofu ya kutekwa, kupotezwa au kuuawa na watu waliotakiwa kutulinda. Umetuondosha kwenye utawala wa sangara ambaye hula mpaka watoto wake mwenyewe, ukatuweka kwenye mikono ya mwenye upendo kwa wana wake.
 

Na Nkwazi Mhango​


Si nadra siku hizi kusikia watu–––hasa wateule wake au wale aliowabakiza kwenye ulaji–––wakimwita rais Samia Suluhu Hassan ‘mama yetu’ ili kumfurahisha na kulinda ulaji wao. Kama tutakuwa wakweli kwa nafsi zetu, je kweli SSH ni mama yetu? Kwangu mimi, SSH ni rais wa JMT basi. Kwanini ninafikiri hivi? Nina sababu zifuatazo:
Mosi, Samia si mama yetu bali rais wetu hasa ikizingatiwa kuwa umama wa taifa haupewi mtu kwa sababu ni rais bali kutokana na mchango wake kama upo. Je tukilinganisha mchango wa SSH na akina Maria Nyerere, mjane wa baba wa taifa au Bi Titi Mohamed, mama aliyepigania uhuru wetu hadi kuathirika kifamilia kwa kuachika na kufungwa tena kwa kusingiziwa kweli tunaweza kusema kwa haki na heshima kuwa SSH ni mama yetu?
Pili, kama ni umama utokanao na urais, inakuwaje watangulizi wake kuanzia Mzee Ali Hassan Mwinyi, Hayati Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na Hayati Dkt John Magufuli hawakuitwa baba zetu? Hapa kuna nini au ni ule udhalilishaji wa mfume dume kama siyo tabia ya kujikomba ambayo ilianza kuota mizizi kwenye awamu ya tano tokana na ukali wa Magufuli? Tulizoea kusikia mke wa Magufuli, mama Janet, akiitwa na walipoende kujipendekeza kwa mumewe wakimwiti ‘mama yetu kipenzi’ sifa ambayo imepotea ghafla baada ya mumewe kufariki na kutokuwa madarakani. Je ni kweli mama Janet alikuwa kipenzi au madaraka ya mumewe? Mbona siku hizi tunasikia akiitwa mjane wa Magufuli bila sifa ya kipenzi kuendelea kutajwa kama kweli alikuwa akipendwa kweli? Je kwanini SSH, ghafla amegeuka mama wa kila mmoja wakati alipokuwa makamu wa rais aliitwa jina lake la SSH? Kunani hapa? Hata hivyo, hili linahitaji wenye kuona mbali na ndani zaidi. Je hawa wanaomwita SSH mama yetu wanamaanisha hivyo au kujikomba na kumzuga aendelee kuwabakisha kwenye ulaji? Je––kama tutafuata vigezo––SSH anastahiki heshima ya mama yetu ambayo kwa maana nyingine ni mama wa taifa wakati mataifa karibu yote–––tokana na mfumo dume–––huwa hayana mama wa taifa isipokuwa baba wa taifa?
Kwa kujua tabia ya kujikomba inayoendana na madaraka, namshauri rais SSH akemee utapeli huu usiokuwa na sababu yoyote bali kujikomba na kumpumbaza na kumdanganya adhani wanampenda wakati si kweli. Hebu fikiria. Alipokuwa madarakani, Dkt Magufuli alikuwa akisema kila jambo na kuungwa mkono huku waliomzunguka wakimsifia na kujichekesha ilhali walikuwa wanalenga kumtumia na kumfurahisha ili wanusurike. Ukiangalia kwa sasa ambapo wale waliokuwa wakijifanya watu wake walivyomgeuka na kuanza kubomoa mema yake, utajua ninachomaanisha. Mfano wa karibu ni ile hali ya baadhi ya waliokuwa karibu naye kuanza kutetea bila aibu mambo ya aibu ana ajabu kama vile mradi mbovu wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ambayo Hayati Magufuli alipiga kalam una kutamka wazi kuwa hata mwendawazimu asingeweza kuuruhusu. Mbali na hiyo, rejea kubadilika kwa ghafla kwa wapiganaji wa miamvuli waliotuaminisha kuwa taifa letu lilikuwa hali corona na lilikuwa likilindwa na Mungu kiasi cha kutovaa mabarakoa kwa vile Hayati Magufuli aliyapinga wanavyovaa mabarakoa. Je huu si ushahidi wa unafiki na imani za woga? Sina ugomvi na kuwepo kwa corona. Je kwanini mliokuwa mmezunguka Hayati Magufuli hamkumshauri au kuachia ngazi pale alipokuwa ameshikilia msimamo kuwa tulihitaji kinga ya Mungu na si barakoa na chanjo?
Taifa letu ni ajabu kidogo. Ilifikia mahali watu wanajua kabisa kuwa walikuwa wakihatarisha afya zao na wengine ilmradi waendelee kuwa madarakani wasijue wangeweza kufa na kuyaacha. Kwa kuzingatia tabia hii ya ajabu na hovyo, namshauri rais SSH asikubali kuitwa mama yetu wakati wanaomuita hivyo wapo wanawake wenye umri mkubwa kuliko yeye ukiachia mbali wanaume wanaoweza kumzaa. Nisisitize. Tuwe wakweli kwa nafsi zetu badala ya kuendekeza njaa na unafiki. Tunawapotosha viongozi na wananchi wetu.
Tokana tabia hii ya kinyonga, nachelea kuwa baadhi ya mambo aliyokataza Hayati Magufuli yanaweza kurejea taratibu kama vile safari za hasara na hovyo za maafisa wa serikali nje, matumizi mabaya, wizi, uzembe na mengine mengi. Rejea kadhia ya hivi karibuni ambapo wadau wa bandari walivyosikika kwenye mitandao wakilalamika kuwa bandari imerejea ujahiri wa awali ukiachia mbali wizi hata ujambazi kuanza kuibuka hata kabla ya Hayati Magufuli hajaoza.
Biblia ina maneno ya busara yasemayo ajikwezaye atashushwa. Pia tuongezee kuwa akubalie kukwezwa asipostahili atashushwa na wale wale wanaompaka mafuta kwa mgongo wa chupa au kumtwisha kiremba cha ukoko. Namshauri rais SSH ajikumbushe kisa cha Yesu siku ya matawi alipoingia Jerusalem akiwa amepandishwa kwenye mgongo wa punda huku wanawake wakitandika khanga zao na wengine matawi ili apite. Je alipokamatwa, watu wale wale walisema? Walisema “asulubiwe” hata bila makosa. Kumbuka. Kabla––kwa mujibu wa biblia––Yesu aliweza kulisha umati pale alipobadili samaki sita na vipande vya mikate watu wakala na kusaza. Ajabu, baada ya hapo, ni wanufaika wale wale walisema bila aibu wala woga asulubiwe.
Mfano mwingine ni wa Musa. Alipowatoa wana wa Israeli Misri alishangiliwa sana. Cha ajabu, akiwa jangwani njiani kuelekea Kanani, walimgeuka wakakufuru wakisema walikuwa wamechoshwa na mana na pia walitaka wamuone Mungu vinginevyo wangemuua Musa. Mfano mwingine ni wa baba wa taifa. Alipokuwa kitini walimwimbia mapambio, ngonjera na nyimbo zote za sifa. Alipostaafu walimwita ‘Baba aambiliki” wakati walikuwa wakigwaya kumwambia zaidi ya kumsifu hadi wakaja na kile kilichoitwa zidumu fikra za mwenyekiti wa CCM. Je zilidumu au zimeishia wapi baada ya yeye kuishia? Hawa ndiyo wanadamu. Hawana tofauti na ndege kwenye mti wenye matunda. Yakiishia, nao wanaishia bila hata kugeuka nyuma kama ambavyo kwa sasa naona wakimpa kichogo Hayati Magufuli ambaye amebakiza wanyonge wake tu ila siyo wale walioshiba mikononi mwake. Hii ni kutokana na ukweli kuwa ukiwa na madaraka, ulaji au utajiri na nguvu watakusifia. Zana hizi zikishakutoka waliokuwa wakijifanya kukupenda wanakuponda. Waliokuwa wakikweza wanakushusha na kukushua. Jifunzeni toka kwa Hayati Magufuli na yanayoendelea. Leo sisemi mengi zaidi ya kuuliza tena. Je kweli SSH ni mama yetu au rais wetu? Je anahitaji sifa hii kweli? Namshauri SSH akatae unafiki na unywanywa wa kutaka kuingizwa mkenge na wasaka tonge na wachumia tumbo ambao wako tayari kucheza ngoma yoyote ilmradi tonge liende kinywani.
41G3oJN8nHL._SX331_BO1,204,203,200_.jpg
download.jpeg
 
Kuwa na mtazano chanya,ndugu hata kama ni mkwamia awamu yako pendwa. Kukosa kuwa Chanya na kufurahia yasiyo mema inatosha kukuweka kwenye kundi la wanaofanya majaribio ovu. Kwa nini usisaidie kutambua wenye nia ovu, ili tupige hatua
Kwani mtoa mada kuna ambalo kalibainisha sio la kweli?
Kitendo cha kutaja sehemu zilizoonyesha kasoro ni kuonesha wenye nia ovu tayari, na anakuwa kwenye kundi la wanaotaka tupige hatua.
Wewe usiyetaka kuyaona hayo au hata ukiyaona unayachukulia kawaida wewe ndie mwenye nia ovu usiyetaka tupige hatua.
 
Mara bandarini kuna tatizo, mara tra mfumo hauko sawa mara tanesco mfumo unazingua mara albino wameanza uliwa tena....
Mama anacheka tu mitandaoni...!
aliowateua wanafanya kazi gani.?
yaan yeyr ndio afanye kazi za mawazir. wakurugenzi.. makatib wakuu? aliowateua hawana uzoefu kazin mpaka wapigiwe kelele
 
Timu Chato wafahamu Mh. Samia Suluhu Hassan siyo Queen Regent bali ni Rais wa Jamhuri ya Muungano mwenye mamlaka kamili na siyo 'mama yetu au Queen Regent'

Wanaosema 'Mama Yetu' ni ndugu zetu wanaotaka kumfanya mwendazake ni 'baba' yetu hivyo wanataka kumpa cheo kandamizi Mh. Samia Suluhu Hassan rais wa Jamhuri ya Muungano kuwa ni 'mama yetu ' ili wapate wasaa na nafasi ya kusema tunamkumbuka 'baba' angekuwepo 'mama' .... ukweli wanataka kumfunga hatamu Mh. Rais Samia Suluhu Hassan asifanye mambo anayoyaamini.

A regent (from the Latin regens: ruling, governing) is a person appointed to govern a state pro tempore (Latin: 'for the time being') because the regnant monarch is a minor, is absent, abdicated the throne, is incapacitated or dead, or unable to discharge the powers and duties of the monarchy.
 
Back
Top Bottom