Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Kwanza, Rais amekuwa ni mtu anayehariri maamuzi ya mtangulizi wake badala ya kuanzisha mema yake. Katika hali hiyo anashangiliwa kwa kuamini kwamba anapambana na maamuzi ya JPM aliyoyafanya. Ni siku 100 hatujasikia muelekeo wake wa uchumi mbali na kukamilisha waliyoanzisha na JPM na yeye kufufua yaliyokataliwa; Bagamoyo.

Pili ni tabia ya kutaka kumfurahisha kila anayekutana naye. Anakutana na akina mama, anatoa ahadi na kukubaliana nao kila kitu. Anakutana na vijana anatoa ahadi na kukubaliana nao kila kitu. Anakutana na wafanyabiashara, anatoa ahadi na kukubaliana nao kila kitu. anakutana na mwekezaji wa kulima kutoka Malaysia anatoa ahadi.

Unawezaje kukubaliana na kila ombi la wafanyabiashara, utadhani ndo wanaounda serikali? Yaani kwamba serikali haina maoni yake juu ya hayo wanayoyaita ni matatizo ya kibiashara? Rais anataka atunge sheria za kodi kwa kushirikiana na wafanyabiashara kweli?

Nchi inahitaji uongozi. Wanawake waongozwe, vijana waongozwe, wafanyabiashara waongozwe. Wengi hawajielewi zaidi ya familia zao na miradi yao.
 
Mtoa hoja usiwe mnafiki na mchoyo wa ukweli,ni mbaya mno unaonekana ni msema UONGO na hii ni hatari hata kwa familia yako,President Samia kwa muda mfupi ameiletea nchi uhuru wa haki,demokrasi imetamalaki ndio maana hoja hii imeileta bila wasiwasi wowote,uelekeo wa serikali yake ameuelezea kwa kina na nini anataka kukufikia katika awamu yake.

Nchi imerudi na kuwa sehemu ya dunia tena,serikali inaendesha shughuli zake kiuwazi(sio mtu mmoja kuamua kiamri)bajeti muhimu imetoka na kuekekeza juhudi kwenye masilahi ya wananchi.

President ametamka laumu ila pia toa the way forward sio kulaumu tu,so far kwangu mimi my President Samia she is on top of the game,na ondoa ndani ya kichwa chako mawazo ya utawala Dume!!
 
Kwanza, Rais amekuwa ni mtu anayehariri maamuzi ya mtangulizi wake badala ya kuanzisha mema yake. Katika hali hiyo anashangiliwa kwa kuamini kwamba anapambana na maamuzi ya JPM aliyoyafanya. Ni siku 100 hatujasikia muelekeo wake wa uchumi mbali na kukamilisha waliyoanzisha na JPM na yeye kufufua yaliyokataliwa; Bagamoyo...
Kule chato ulipata mgao wa nini? Shati?
 
Kwanza, Rais amekuwa ni mtu anayehariri maamuzi ya mtangulizi wake badala ya kuanzisha mema yake. Katika hali hiyo anashangiliwa kwa kuamini kwamba anapambana na maamuzi ya JPM aliyoyafanya. Ni siku 100 hatujasikia muelekeo wake wa uchumi mbali na kukamilisha waliyoanzisha na JPM na yeye kufufua yaliyokataliwa; Bagamoyo...
POLEN WAZEE WA KULINDA LEGACY YA MSEMAKWELI MPENZ WA MUNGU
 
Kwanza, Rais amekuwa ni mtu anayehariri maamuzi ya mtangulizi wake badala ya kuanzisha mema yake. Katika hali hiyo anashangiliwa kwa kuamini kwamba anapambana na maamuzi ya JPM aliyoyafanya. Ni siku 100 hatujasikia muelekeo wake wa uchumi mbali na kukamilisha waliyoanzisha na JPM na yeye kufufua yaliyokataliwa; Bagamoyo...
Mpuuzi weye!Kuwa kiongozi ni vema ukawafanya watu wako wafurahie maisha. Siyo kuwa mjingamijinga na kuwakatisha tamaa.Mama Samia saaaaaafiiiiii!😝😝😝😝
 
Back
Top Bottom