Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

China moja hiioooo
... 2020 hakupata ubunge huyu? If yes, jimbo gani au viti maalum kama kawa ya "waliobarikiwa" kula mema ya nchi? Wengine twala laana tu yakhe; jasho twavuja lakini baado laana zatuandama toka vizazi.
 
Nasikitika kuwasoma baada ya yaliyotokea.. je, mlikuwa wapi kabla kumsifia nae afurahie kazi yake??? Mimi pia ningefurahi kufahamu habari nzuri za kiongozi Mh huyu.

Kazi iendeleeeee...
 
Sometimes huwa najiuliza sana hawa wateuaji kuwa wanatumia njenzo gani kuwapata wateuliwa, naishia kujipa moyo tu kuwa labda kuna taarifa sina
 
Sometimes huwa najiuliza sana hawa wateuaji kuwa wanatumia njenzo gani kuwapata wateuliwa, naishia kujipa moyo tu kuwa labda kuna taarifa sina
Utateuliwa kama unafahamika na wakubwa wenye chama....hizo sifa zingine ukitoa hii ni mbwembwe tu.
 
Mama tunakuomba, tunakusihi tuondolee hilo li Jenista huyo mtu aitwaye Jenista Mhagama hatumtaki na hafai, huyo mama hafai popote, lakini kama umeona anakufaa sawa mpange popote lakini turudishie Mchengerwa wetu huyu ametutibu majeraha aliyotujeruhi Jenista, Jenista Mhagama ni zaidi ya mkosi kwa watumishi. Naamini Mh Rais utasikia kilio cha watumishi kabla ya kuwaapisha viongozi wateule
 
Ukiona mtu anapigwa mawe ujue ni mchapa kazi na machawa na makupe wameanza kutaharuki,huyo anaonyesha anawafaa hapo maana ataondoa mauzauza mnayofanya,kazi iendelee huyo anafaa kabisa .
 
Watumishi tunaona una kila sababu ya kutawala milele mpaka useme baaaasi!! Ila sasa mama umetuletea mkosi "vuvuzela" sijui linaitwa Jenista!?? Hilo zigo mama kaa nalo huko hatulitaki huku utumishi, hilo ni jini litatunyonya damu

Mama, Tunakupenda sana ila hilo vuvuzela hapana!!! Tunafikiria uwe Rais angalau miaka 23 endapo marekebisho ya katiba yatafanyika mapema.
Ni zigo kweli teh teh teh..
 
Sometimes huwa najiuliza sana hawa wateuaji kuwa wanatumia njenzo gani kuwapata wateuliwa, naishia kujipa moyo tu kuwa labda kuna taarifa sina
Kwa jenista lazima msoga team ihusike. Ukiangalia walioula safari hii ni watu wake. Kuanzia mkata umeme, mtama na sasa huyu mama
 
Kweli watumishi mmeumizwa sana Poleni.
naamini Mhe. Rais Mama yetu atalifanyia kazi suala hilo.

Lakini pia kama Jeni ujumbe umemfikia basi ni bora akajiengua mapema kuliko kuja kuenguliwa kwa fedheha, upepo unao vuma dhidi yake sio mzuri hivyo ajitafakari mapema kabla ya hatari.
 
Samia ameshasema yeye Rais huwa hakosei, hivyo basi Mchengerwa kamwe hata rudishwa utumishi (maana amepaharibu!) na Jenister Mhagama ndio amefika utumishi yaani anapaweza na atakuwa hapo sana tu.
 
Ukiona mtu anapigwa mawe ujue ni mchapa kazi na machawa na makupe wameanza kutaharuki,huyo anaonyesha anawafaa hapo maana ataondoa mauzauza mnayofanya,kazi iendelee huyo anafaa kabisa .
You are a confused fellow
 
Back
Top Bottom