Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Kwa mambo yanayoendelea hapa nchini kwa sasa, Ni wazi kwamba wananchi hawana tena imani chini ya uongozi wa awamu hii ya sita. Kila unapoenda ni lawama na hali ya kutoridhika na utendaji wa serikali.Mambo haya yamekuwa yakilalamikiwa sana.

1: Uchumi wa Tanzania Umeporomoka.Laiti kama uongozi ungekuwa thabiti hakika uchumi ungekuwa wa kati daraja la juu tofauti na hali ilivyo sasa ambapo Tanzania imeporomoka kutoka nafasi yake ya 8 kati ya nchi 10 zenye uchumi bora Africa mpaka nje ya top 10 na kuzidiwa na vinchi kama Ghana na Angola

2: Laiti kama uongozi ungekuwa imara nidhamu na uwajibikaji kazini ungekuwepo.Leo hii tunashuhudia wananchi wakihoji kuhusu hali ya umeme nchini pasipokuwa na majibu au majibu yenye uwalakini. Lakini pamoja na hayo bado viongozi wamebaki wakiwa maofisini pasipo kuwajibika kwa namna yoyote.

3: Kwa miaka kadhaa Tanzania imekuwa ikiifanya juhudi kubwa kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha miradi mikubwa na ya kimkakati. Licha ya kwamba tangu awamu ya sita iingie madarakani hakuna mradi wowote wa kimkakati ulioanzishwa bali pia hata ile miradi iliyokuwa ikiendelea imekuwa ikisuasua

4: Serikali ingekuwa makini hakika Umeme usingekuwa wa mgao.Tangu Rais S.S.H aingie madarakani hali ya upatikanaji wa umeme nchini imekuwa mbaya sana.Hali hii imepelekea kurejea kwa mgao wa umeme ambao watanzania wengi walishausahau tangu miaka kadhaa iliyopita.Hali inayopelekea kuwatesa wananchi hususan wale wanaotegemea umeme kujipatia vipato katika shughuli zao za kila siku.

5; Hali ya upatikanaji wa maji imekuwa ya kusuasua.Kwa miezi kadhaa hususan katika jiji la Dar es salaam pamekuwa na mgao wa maji.Hali iliyopelekea kukosekana kwa maji kwa muda mrefu katika maeneo mengi.Hali ambayo hakuwahi kushuhudiwa hapo awali.

6: Tozo zisizokuwa na tija na zilizoua uchumi wa wengi.Serikali ya awamu ya sita imedhulumu na kunyang'anya kwa nguvu fedha za wananchi kwa kigezo cha tozo katika miamala ya simu.Mama mjane anapomtumia mgonjwa wake hospitali kwa ajili ya matibabu anakatwa fedha ambayo kimsingi haikuwa ya biashara. Kwa mujibu wa report kutoka Vodacom hivi karibuni miamala ya simu imepungua kwa asilimia zaidi ya 30!.Hili si jambo la kupuuza hata kidogo kwa uchumi wa nchi.Ni sawa na kutoa fedha mfuko wa kushoto na kuhamishia Kulia.

7: Kupanda kwa bei ya Mbolea.Mara tu baada ya awamu ya sita kuingia madarakani bei ya mbolea ilipanda karibu mara mbili ya bei ya awali.Hii ni imepelekea uchumi wa watanzania wengi ambao ni masikini na wanategemea kilimo kudhoofika.

8; Kupanda kwa bei ya mafuta ya kupikia.

9; Kupanda kwa bei ya mafuta ya petrol.

10; Kupanda kwa bei ya bidhaa za ujenzi kama cement,Nondo n.k.

11; Teuzi za viongozi wasiokuwa na weledi kwa kigezo cha favour/Undugu/Kujuana (Mf. Riziwani Kikwete,Nape Nauye n.k) Tanzania ina vijana wasomi na wenye upeo mpana wa kifikra. Lakini cha kushangaza teuzi zimekuwa hazina matumaini ta kuipeleka Tanzania kule tunapotarajia.

12: Ukosefu wa uzalendo na ubadhirifu miongoni mwa watumishi wa umma.Siku si nyingi tumeshuhudia kiongozi mkuu wa serikali akiwaasa watumishi wake wale kwa urefu wa kamba zao.Hii inaashiria kwamba hata kiongozi mkuu anashiriki katika ulaji huo.Hali hii ni hatari kwa rasilimali za nchi.

13; Wananchi hususan wa hali ya chini kukosa nafasi katika nchi yao.Siku si nyingi tumeshuhudia wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga wakinyanyaswa kwa kuhamishiwa katika maeneo yasiyokuwa tija kwao.Vuta nikuvute hii imepelekea hali ya unyonge na sintofahamu miongoni mwao na kupelekea kuongezeka kwa umasikini miongoni mwa watanzania

14; Mikopo isiyokuwa na tija kwa taifa.Tangu Tanzania ipate uhuru viongozi wake wote walisisitiza kufanya mambo yetu kwa fedha zetu wenyewe bila kutegemea wahisani. Tanzania imebarikiwa rasilimali za kila aina.Mito,Maziwa,Bahari,Madini kama Tanzanite,Mbuga za wanyama,Gesi n.k Inashangaza Sana kuona kiongozi badala ya kusisitiza au kubuni namna ya kuzitumia rasilimali hizi ziweze kuwa na tija kwa watanzania,Badala yake tumekuwa tukijivunia mikopo!

15 ; Kuongezeka kwa gharama za uunganishaji umeme kutoka 27,000 iliyokuwepo mpaka zaidi ya 300,000 ya hivi sasa.Hali hii imepunguza mno kasi ya usambaaji wa umeme

16 ; Muingiliano baina ya mihimili kwa kigezo cha uchama.Inasikitisha kuona kiongozi wa mhimili mmoja anakosa uwezo wa kuikosoa na kuurekebisha mhimili mwingine kwa kuhofia kibarua chake.hili tumelishuhudia baada ya kuona spika wa bunge la JMT kujiuzulu baada ya kuhoji kuhusu mikopo na tozo.

17 ; Safari zisizokuwa na tija wala umuhimu kwa taifa. Tumeshuhudia safari nyingi mno za nje ya nchi,Safari hizi zimekuwa zikiigharimu nchi fedha nyingi.Safari za vikao visivyokuwa na tija kama mkutano wa kujadili athari za gesi ya ukaa sidhani kama ina tija hususan kwa nchi ambazo bado uchumi wake ni mdogo.Ni sawa na mzazi anayemiliki baiskeli kwenda kuhudhuria kikao cha adha wanayopitia wamiliki wa magari kwa tairi zao kukosa ubora.

18 ; Kukosekana uhuru na ukandamizaji wa demokrasia. Tunaweza kusema kwamba pia hata katika awamu zilizopita hili lilikuwepo, Lakini hili la sasa limekuja kwa namna tofauti.Wakati mwingine baba anaweza kumpa mtoto adhabu ya kulima shamba,Mtoto akalia na kulaumu sana,Lakini shamba hilohilo baadaye likaleta chakula mezani wote wakala na kufurahia. Ila tofauti iliyopo sasa,Hakuna chakula kinachokuja mezani!

19 ; Kushughulikia zaidi mambo yasiyokuwa na tija kwa wananchi kuliko yale yenye umuhimu na tija kwa watanzania. Imekuwa jambo la kawaida kwa awamu hii kujihusisha zaidi na makongamano,Semina elekezi,Birthday Party pamoja na hafla mbali mbali badala ya kujikita katika kufufua na kubuni miradi ya kimaendeleo itakayosaidia kuwapunguzia wananchi mzigo wa umasikini na kuinua uchumi.Hafla ya machifu na watemi si muhimu kama hafla ya utiaji saini mradi wa uchimbaji na usambazaji wa gesi ya Mtwara!

20 ; Kukosekana ajira. Ubunifu na uibuaji wa miradi mipya si tu umekuwa na tija kiuchumi Bali umekuwa ukiajiri vijana wengi.Kukosekana kwa ubunifu na sera mbovu za serikali zimesababisha kukoseka kwa ajira miongoni mwa vijana wengi

21 ; Kuongezeka matukio ya uhalifu.
Mara tu baada ya awamu ya sita kushika hatamu sote tumeshuhudia jinsi wimbi la uhalifu lilivyoongezeka.Sio tu matukio ya wizi na ujambazi bali mpaka uchomaji wa masoko kama Kariakoo, mchikichini n.k wizi mauaji na utekaji nyara vimeongezeka kwa kasi mno. Hii inaonyesha udhaifu katika usimamizi wa majeshi yetu ya ulinzi na usalama

22 ; Kuongezeka gharama za simu
Kutokana na kodi za miamala Kuongezeka kampuni za simu zimejikuta zikilazimika kupandisha gharama za muda wa maongezi na huduma zinginezo za simu kama vile huduma za vifurushi ili kuweza kubalance gharama za uendeshaji. Hali hii imesababisha mzigo mzito kwa wananchi hasa ukizingatia mawasiliano ni nyenzo muhimu sana katika shughuli zao za kila siku

23 ; Kutoa vipaumbele kwa mambo ya hovyo na yasiyo na tija kwa taifa hususan kwa wakati huu.Hapakuwa na ulazima kutumia gharama kubwa na uwekezaji katika kutumia kodi za wananchi kiongozi mkuu wa serikali kusafiri na kutumia muda mwingi kutengeneza filamu wakati fedha hiyo haina uhakika wa kurudi.Mfano fedha hiyo ingewekezwa kwenye timu maarufu zinazoshiriki ligi za ulaya ingekuwa na tija na matokeo zaidi na Rais angepata muda kutekeleza majukumu mengine ya kiserikali kuliko kupoteza muda mwingi kusafiri.

Hakika ni mambo mengi ambayo yamekuwa yakifanyika kinyume na matarajio ya watanzania wengi ambao waliwaamini viongozi wao na kuwaweka madarakani huku wakiwa na matumaini makubwa ya kuondokewa na maradhi, ujinga na umasikini ambao ndio maadui wakuu wa taifa kama ilivyobainishwa na Mwl Nyerere badala yake watanzania hao ambao wengi ni masikini na wameteseka kwa umasikini kiasi cha kusahau tarehe zao za kuzaliwa huku wakishuhudia wale waliowachagua wakikata keki ikulu!
 
Nianze Kwa kumshukuru Mwanajf ambae Alisoma Uzi wangu na kuuelewa vyema dhidi ya kumpinga dhidi ya kuwa na mjadala wa rushwa katika Taifa Zima kana kwamba sisi sote ni wala rushwa, ingelikuwa ni suala mfano la maradhi hasa maradhi ya mlipuko mfano ebola, corona na mengine hayo tunaweza sema tujadili kabisa maana ni maradhi ya mlipuko.

Binafsi nimekuwa napinga kabisa baadhi ya viongozi wetu wetu kutafuta visingizio visivyo na tija kwa mambo yaliyo chini Yao,

Mathalani, suala la watu wachache walio aminiwa na serikali kuto timiza wajibu wao ipasavyo mathalani kuiba, kufanya kazi kwa uzembe,ubadhilifu na vingine Ving Hawa wamekuwa ni WA kufukuzwa kazi Raisi anakimbia majukumu hawafukuzi anakuja mbele ya umma KUANZA kulia Lia, nilimsema Rais mwinyi, alipo Lia dhidi ya mkurugenzi wa Zaecca, Jana Rais Samia nae analia dhidi ya Takukuru na Zaecca, BAADA ya kuwa hawatimizi majukumu Yao ipasavyo!

Kuna msomaji amenifata pahala na kuaniambia Kwa ujumbe usemmae hivi'' ni vyema ukiwa unapingana na Rais basi shauri Nini kifanyike?''
Nakubaliana na wewe maoni yangu ni haya,
1.Mimi pamoja na kukosa Imani na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama baada ya polisi kunyoshewa mikono sana BADO Nina Imani kubwa sana na idara ya usalama wa Taifa.
Nina Imani na idara hii sana na ufatao ni ushauri maana naisi Hawa wanao uwezo mkubwa wa kumsaidia mama

Kwanza avunje ofisi zao zote ila ibakie moja makao makuu Ile ya karbu na nyumbani kwa Magufuli iliyojengwa Kwa ramani ya ndege pale karibu kanisa la St Peter hiyo ibakie ila Mimi sioni umuhimu wa kuwa na ofisi zao kweny Kila mikoa au wilaya au vitongoji.

Nasema hivyo nikiwa na maana yakuwa Hawa usalama waingizwe kweny idara mbalimbali za serikali, kuanzia Kijiji mpk mikoani mpk halimashauri.

Wasi wasi wangu upo hapa, je yawezekana usalama siku hizi wanaajili mijitu hisiyo na Taaluma yoyote?yaani jitu ni o level mfano halina Taaluma yyte linaajiliwa uko?kama mfumo sio huo ni vizur Kam tuna waasibu sjui Nini tuwasambaze kwenye Vituo vya kazi mbalimbali walah watapata taarifa mapema na kuhakikisha ujinga huu unao waliza maraisi wetu haupo.

Enzi za ukuaji wetu sisi tulikuwa tukikiwaona watu wanatembea hovyo barabarani wakiongea peke Yao, tukajua ni machizi kumbe wanaume walikuwa kazini na kweli uhuu wizi WA ovyo haukuwepo, Kwa Nini ndani ya Takukuru hakuna Tiss Kwa nn ndani halimashauri ofisi ya mkurugenzi Haina mtumishi ambae ni Tiss?Kwa Nini Tiss wanatengwa?Hawa walitakiwa kuchanganywa na watumishi wengine maana mission ya wizi ni mnyororo sio hishu ya mtu mmoja.

Katika mnyoror huo lazima watakikanyaga kumshikisha nyoka wetu na mambo inakuwa mswano.

Raisi Magufuli alikuwa anaelekea KURUDISHA mfumo huu na alikuwa anaelekea kufanikiwa sana sana sana sana MAana vijana wetu walianz kufanya kazi ipasavyo lakini mambo yanarudi tuliko toka kisa uongozi wa juu hauna vissionna na mission dhidi ya KUKUTUMIA hiki chombo kamwe.

Ushauri mkuu Kwa wakuu WA kaya Zanzibari na Tanganyika.
Watumieni hawa vijana ipasavyo maana hata ukimbizwapo Mwenge, taarifa za ubadhilifu wanao zitoa ni hao hao vijana Kwa wakimbiza mwenge,

Ni jambo la ovyo sana kuwa na jeshi la Usalama wa Taifa linaro lipoti Kwa Wakimbiza Mwenge it's not health for our Nation give them a chance.
Sifi Leo 15/10/2022.
 
Mwanza jijini maeneo ya Buzuruga, Nyasaka centre, Kiloleli,Mahina & others maji shida, umeme tunalala giza cha ajabu Mwauwasa bili wanachukua kila mwezi hali ni mbaya sana watu hatujui kesho yetu
 
Chain of information sio salama tena, baadhi ya watumishi wa idara pendwa kwa sasa uzalendo kwao sio kipaumbele tena wanaangalia watafaidika vipi na taarifa zinazowafikia mezani kwao.

Wengi wao wamekuwa wakitumia taarifa hizo kujinufaisha wao wenyewe na sio katika kulisaidia taifa, kwa ufupi idara pendwa iko corrupted, na taasisi hii ikishakuwa corrupted hakuna chochote kitakachofanyika.

Huko takukuru ndio uozo mtupu, napata mashaka na namba moja katika kufanya maamuzi hii ni mara ya pili amekuwa akimsema Hamduni ila hajamchukulia hatua, sasa naelewa kwa nini huyu kiongozi wetu amejawa na udini, huyu bwana angekuwa mkiristo huwenda muda huu naandika hapa asingeendelea kuwepo ofisini.
 
Mtu ambae anahamasisha ufisadi kwenye Taifa hawezi kupambana na Rushwa
 
Hizi pumba pelekea nguruwe wakale kama huna nguruwe zipige moto. Huu ni Uzi wa SUKUMA GANG.

Halafu Samia amefungua uhuru wa maoni na kusema. Wakumponda wanamponda, na wa kumpongeza wanampongeza pia.

Siyo Magufuli ambaye aliishia kusaka watu mitaani na mitandaoni ya wanaomkosoa. Tanzania iko mikono salama na Rais SSH
 
Unaweka fisi akulindie mnofu wako? Hii haipo sawa kabisa. Polisi ni corrupt sana na wana mtandao wao wa uhalifu toka kwa konstebo hadi IGP mimi nashauri mama apange safu zake upya hii kuchukua polisi kwenda kuongoza PCCB haipo sawa hao PCCB wana tamaduni yao ya kupambana na rushwa kwa kutumia PCCA Na.11/2007 ndo msaafu wao. Kuna uzi nilianzisha mwaka jana kitu kama hicho kushauri PCCB na ZAECA ziungane kuwa chombo cha Muungano kama vyombo vingine leo hii jamhuri ya Muungano vyombo 2 sheria zinakinzana kwa muktadha huu vita ya rushwa itazidi kufeli. Hamduni kapwaya anafanya kazi Dom kuishi Kigamboni mida mingi na Chanika concentration ya kazi hakuna. Acha wapige rushwa vijana
 
Huyu mama ni kama ameokota dodo chini ya mbuyu. Yaani mfano hapo ukiamsha ukimuuliza umepanga kuifanyia nini tanzania, hana jibu.

Bahati mbaya mfumo alioukabidhi nchi na kuuamini ni watu wasio serious na nchi, isipokuwa familia zao na matumbo yao.

Yaani yeye hajui na aliowaamini hawajui.

Yeye amenogewa na urais, v8, saluti na safari za nje. Na ameambiwa kwa damu au maji utakuwa tu rais tena, we tuachie. Anasubiria urais tu tena.

Kifupi kwa aliyeijua serikali ya JK wala hapati shida kujua nani rais, nani msaidizi. Samia ni msaidizi tu.

JK hajawawahi kuwa serious na mambo ya uongozi iwe nchi au familia yake ,tuliishuhudia alipokuwa rais namna familia yake ilivyokuwa ikifanya.

Leo hii kila kitu kinaenda kama kilivyo. Wao wako bize na safari, birthday parties na kupeana nafasi za upigaji nchi.
 
Mwanza jijini maeneo ya Buzuruga, Nyasaka centre, Kiloleli,Mahina & others maji shida, umeme tunalala giza cha ajabu Mwauwasa bili wanachukua kila mwezi hali ni mbaya sana watu hatujui kesho yetu
Inasikitisha sana, Baadhi ya maeneo karibu wiki nzima hawapati umeme. Maji ndiyo balaa! Wakati huo kiongozi anabadili route kutoka Oman mpaka USA
 
So far kiuchumi awamu ya sita inafanya vizuri sana compared na awamu zilizotangulia. Na tunapoelekea ni pazuri zaidi maana kwa jinsi wanavyojipambanua kisera wanaleta confidence zaidi kwa wawekezaji.

Nadhani unasumbuliwa tu na chuki na husda dhidi ya awamu ya Sita. Huna hoja yeyote
 
Huyu mama ni kama ameokota dodo chini ya mbuyu. Yaani mfano hapo ukiamsha ukimuuliza umepanga kuifanyia nini tanzania, hana jibu...
Kiongozi asiyekuwa na maono ni hasara kwa taifa, Nchi inakosa dira na mwelekeo sahihi.Mara aseme atajenga kiwanja Msalato mara kipaumbele huduma za wanawake na makundi maalum yaani hakuna dira ya taifa.Haya ni madhara ya kuwa na kiongozi asiyekuwa Chaguo la wananchi
 
Back
Top Bottom