Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Wacha unafiki.
Mwezi uliopita ulibandika uzi hapa, kama kawaida yako, kusifia ripoti ya World Bank kuhusu Ufanisi mzuri wa Bandari ya Tanzania....hiyo ilikuwa 23may2023!

Tanzania tumewekeza takribani Trillioni 2 Shilingi katika kuboresha Miundombinu Bandarini hapo...Hakuna sehemu ripoti hiyo iliyodai Bandari ilikuwa Shamba la bibi, vilevile Mabarawa alisifia ongezeko la mapato....yaani nyuma ya sura zao walikuwa wanajua wanaenda kuigawa Bandari halafu wanakuja na hoja dhaifa kama 'Ufanisi' na 'Utendaji' ebo!

Isitoshe ulileta Uzi wa kupotosha kuwa mkataba huu uiliridhiwa na Hayati Magufuli na hivyo kutaka kuaminisha kadamnasi kuwa haya ni muendelezo wa Hayati....kwamba Bandari ilihitaji marekebisho na maboresho, sawa....ikiwa ina maana Hayati aliyaona mambo ya 'ajabu ajabu' na inaelweka ni jambo lililomuhudhi sana kama Raisi kuona kuwa Bandari inachezewa....unajua hilo....halafu unajitanua hapa kudai hayati ndie aliyeifanya Bandari kuwa shamba la bibi! Are you serious?
Ufanisi huo hautoshi yaani ni kujikongoja ila Bado Kuna shida kubwa,so Ili kufika uwezo wa Bandari kama Mombasa inatakiwa Mwekezaji mwenye uwezo zaidi..

Mwisho kama ulikuwa wa mwisho ukasogea kuwa wa 8 umejitahiri ila unatakiwa kuwa wa kwanza Kwa sababu uwezo huo upo.
 
Anatupelekaa Uarabuniiii...!![emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Huyo ndiye Rais wa nchi hiyo cheap popularity inaingiaje?

Mkitaka msitake yeye ndiyo kiongozi mkuu wa nchi na ndiye aliyeachiwa hatamu ya uongozi, mbona aliyepita kuna miradi aliiwacha hivyo hivyo?

Tuwe na subira, kwani yeye hajatoka upinzani ni kiongozi wa CCM ileile na ilani ileile kinachotofautiana ni utendaji tu. Ukizingua unazinguliwa.

Haya mambo ya kuwauzia nchi waarabu yamo kwenye ilaní ya ccm?
 
So kwa akili yako miradi ya Chato nayo ataendeleza? Hata daraja la Busisi tunapiga chini kwanza.

Mtapiga chini ili mlipe fedha mlizochukua kwa wachina kwa kufufua ujenzi wa bandari ya Bagamoyo?
 
Si nasikia kuna TIMU CHATO ambayo inamikakati ya kukwamisha mama na kumkosoa kwa kila afanyacho eti kisa kaanza kueleza ukweli wa yale yaliyo kuwa yanatendeka sirini, naona mmeanza kazi sasa.
Acheni ujinga wenu muwe wazalendo kwa kutetea nchi ; huyu mama anaiuza nchi kwa waarabu kimya kimya akishirikiana na Vasco Dagama na ndio maana mkwere hajatoa neno toka sakata la bandari lianze!!
 
Kwani Ndugai alisemaje ?

Huenda yeye kama Spika kuna aliyoyaona ambayo sisi hatuyaoni, ndipo huko huenda anatupeleka...
 
Kampa mbowe ruzuku anakula na watoto wake... Kamrudisha Lissu bongo anaishi hana pakukaa... Kamrudisha na kumlipia Lema deni la mkopo crdb alilokua amelikimbia... Kubwa zaidi nchi ipo huru wawekezaji kila kona... [emoji90][emoji90][emoji90]

Kumbe Ndiyo maana Lema anasema vile kuhusu mkataba?!
 
Haya mambo ya kuwauzia nchi waarabu yamo kwenye ilaní ya ccm?
Hakuna mtu anaweza kuuza nchi, hebu tufikirie mpaka sasa nchi gani umesikia imeuzwa? Sisi tunataka maendeleo na maendeleo yana gharama zake, miongoni mwa gharama zake ni kuleta wawekezaji ambao wengine wanatupiga au kupata misaada yenye masharti magumu. Sasa hawa ambao tunaingia nao mkataba wa keundesha baadhi ya gati za bandari hapa Dar wamekuja na matakwa yao, kizuri zaidi huo mkataba umewekwa wazi kila mwenye uwezo wa kuusoma na kuukosoa yupo huru, tushukuru kuwa tumepata viongozi wawazi, huko nyuma kuna mambo yalikuwa yanafnywa hata bunge halishirikishwi. Diplomasia ya uchumi ni miongoni mwa ilani za CCM, na swala hili la bandari ni miongoni mwa athari ya kukuwa kwa dilpomasia ya uchumi Tanzania, tumepata kiongozi mwenye maono ambaye anaka tuwe na uhusiano wa muda mrefu wenye kunufaisha nchi zinazoshirikiana. Leo hii Tanzania ina uhusiano na Israel na hata tuna ubalozi huko, nchi ambayo huko nyuma raisi wa awamu ya kwanza Mwalimu Nyerere aliuvunja uhusiano wa kidiplomasia kutokakana na vita baina ya waarabu na Israili, na hata leo hii waarabu nao wana uhusiano mzuri na Israili, hivyo haya mambo ya chuki kwa watu amabo tumeaminishwa ni waovu hayana msingi. Kwa nyakati zetu hizi ili tuendelee lazima tuwe na pesa, teknoloji na railimali, sasa sis tuna rasilimali pekee wacha tuungane na wenye pesa na teknoloji nasi tusonge mbele. Miaka 50 iliyopita Dubai kilikuwa ni kijii cha wavuvi tu ambapo sisi Tanzania tulikuwa na nchi yenye neema, lakini sasa hivi tumeachwa mbali sana.
 
Hivi unawaza Kwa kutumia kiungo gani?
Rasilimali za asili zisizo mnufaisha mwananchi na zikaendeshwa na mgeni hiyo ni sawa na nini?
Wewe kwenye eneo lako
Una mamlaka yeyote na gas kule mtwara?
Hii mikataba ukomo wake ni lini?
 
Ikiwa rasilimali zetu za asili haiztunufaishi na zinaendeshwa na mgeni huo ni ukoloni tu, itabidi tufanye harakati za kudai uhuru tena.
Unataka mamlaka gani uyapate kule Mtwara kwenye gesi?
Asilimia 70 ya gesi inayozalishwa na kiwanda cha gesi Mtwara inatumiwa na Tanesco katika uzalishaji wa umeme nchini.
Kila kitu kina ukomo, hebu tuwaachiye wanataaluma kwenye taaluma zao tunachotaka ni maendeleo yetu na vizazi vyetu.
 
Kwa haya ya Bandari na Loliondo, huyu mama akipewa miaka mingine mitano 2025, mjue hatutakuwa na kwetu. Yeye atasepa na kurudi zanzibar na Mbalawa wake.
CCM mnaojitambua kataeni huyu mtu.

Maxence Melo tunaitetea tanganyika, msiufute uzi huu
Duuh
 
Kwa haya ya Bandari na Loliondo, huyu mama akipewa miaka mingine mitano 2025, mjue hatutakuwa na kwetu. Yeye atasepa na kurudi zanzibar na Mbalawa wake.
CCM mnaojitambua kataeni huyu mtu.
Kwamba atauza mpaka ardhi?
 
Miradi ya JPM:
1. SGR
2. NYERERE HYDROELECTRIC POWER
3. Upanuzi wa barabara njia 8 + 4(service road)=12 kimara mpaka kibaa
4. Rada 4 za kulinda anga la Tanzania
5. Kufufua ATCL kanunua ndege 12
6. Elimu bure
7. Viwanda (kalakana/gati) za kutengeneza meli ziwa Victoria
8. Daraja lefu zaidi East Africa na kati 5km la busisi ziwa Victoria
9. Elimu bure
10. Makazi bora ya vyombo vya ulinzi (polisi) nchi nzima
11. Kuunganishiwa umeme vijiji vyote karibu na bure kwa kulipa tu 27,000/= ulishaona wapi?
12. Hostel za wanafunzi UDSM
13. Serikali kuhamia Dodoma
14. Ikulu mpya Dodoma chamwino
.
.
n.k

Ongeza nyingi
Ujenzi wa majengo ya kisasa ya mahakama kila mkoa/mkoa
 
Mama Samia achana na cheap popularity haitakusaidia lolote unatakiwa usiwe muongeaji sana maana naona unaanza kutoboa matundu ya hela wakati huo ukiwa umewekwa kwenye mtego mgumu na mzito sana wa ilani yenye kurasa 300 ya kutekeleza miradi yote iliyoko kwenye ilani.

Yaani kumbuka sasa hivi hauko kwenye meli mpya uko kwenye meli ileile sema tu imepata mawimbi katikati ya safari.

Mama nimekushangaa sana unaposema kuna miradi mingine iko kwenye makaratasi wakati wewe na Hayati Magufuli ndio mliotembea nchi nzima kuinadi kwa hiyo tunataka ahadi zilizoko kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Tofauti na hapo hatutakuelewa tutanyima kura 2025 kama ukitaka kuomba ridhaa ya kugombea tena.

Jitahidi sana kwenye suala la kodi usiwalaumu tu TRA waonye hata wafanyabiashara pia maana ni wakorofi.
Tulishapotea siku nyingi, hivyo tunazungukazunguka tu kwenye kupotea kwetu.
 
Niliona maadili yamepungua katika nchi na Kiongozi mwenye dhamana anaona sawa tu,niliona jahazi likigonga Mwamba na kupasuka,niliona laana ikiwatafuta wote wenye dhamana niliona wakiaibika japo mwanzo walionekana ni watu wa suluhu na Dunia mzima ilisema huyu ndiye tuliyemtaka,baada ya miaka miwili niliona akivua ngozi ya Kondoo na kubaki na ngozi yake ya mbwa mwitu,nilisali ndoto hii isije kuwa kweli lakini ilishaandikwa kwenye kitabu cha ufunuo 6:1-8 nayo ni lazima itimie.
 
ufunua 6:1-8 inaongelea mambo mengi,sijajua unataka kuambia nini hapo
 
Back
Top Bottom