Siku Ile ya Tarehe 17/3 , nipo Lodge Mara TV linatangaza habari ,Samia anamtangaza Kifo Cha JPM.
Kwanza shoo ikaishia palepale, nikaanza kububujikwa na machozi.
Kilichoniliza , sio Kifomcha JPM pekee, Niliwaza, nikaanza kumbuka Maujinga ya wakati wa JK MASIKIN alivyokua choka mbaya kabwera, Tajir akawa Tajiri wa kutupwa,, ukimsifia Papa nani huko anakumwagua Hela , Nchi ikachakaa kwelikweli, Rushwa, ufisadi ulokithiri ,Nchi ikafubaaaa.
Kwa ujanja wa Jakaya, akawa anaajiri Kila mwaka, akaacha watu waongee wanavyotaka , wajinga wakafurahia mambo mepesi, ila nchin ikazidi kuliwaaa.
Oyaaaaa, nikasema Moyoni mwangu, Hivi ndiko Sasa tunarudi tulipokua??.
JPM kafa, watanzania na mabeberu yakaanza kufungua kesi mahakamani, Yanarudishiwa Pesa yalotuibiaa .
JPM Kafa, Wamasai wanahamishwa.
JPM kafa, Wafanyabiashara wanajiamlia bei.
JPM kafa, Nchi Haina bei elekezi.
JPM Kafa, Rushwa ufisadi ndo usiseme.
JPM kafa, Tunaambiwa JNHEPP Ina nyufa.
JPM kafa, Bandari zote kapewa Mwarabu .
Kuna wakati kama mwanadam ,unaweza jikuta unavuka ukomo wa Uvumilivu na kuanza kumhoji Mungu, kwanini ulimchukua JPM???.
Binafsi katika Moja ya Maombi nayoomba Kila siku ni huyu kiumbe Mmoja kuaga Dunia....
JK.
Ndugu Carlos usidanganye watu, Hakuna anaye furahia kifo cha mtu ila tarehe 17 Machi iliepusha nchi kuingia kwenye shimo la sahau!
Kwanza kumuingiza JK kwenye hoja yako kuhusu ufisadi bila kuweka wazi kiasi cha ufisadi ndani ya uongozi wake dhidi ya ufisadi ndani ya uongozi wa JPM hutendi haki.
Kwa kukusaidia, kwa mujibu wa ripoti ya CAG, mpaka JK anatoka madarakani miaka 10 ufisadi ulikadiriwa kufikia bilioni 360.
Ilihali kwa mujibu wa CAG hadi JPM anafariki, yaani ndani ya miaka 6 ufisadi ulikadiriwa kufikia zaidi ya trilioni 3. Na ndio maana CAG aliondolewa na sheria ya takwimu kubadilishwa.
Kuhusu kesi, kesi nyingi zimetokana na maamuzi mbaya ya JPM aliyoyafanya bila kufuata sheria, na hivyo kupekea tunashindwa. Kipindi cha JK ndio ulishindi kesi ya kutumia maji ya ziwa victoria na kesi ya radar miongoni mwa kesi nyingine ulipatikana.
Kuhusu kuhamisha wamaasai utaratibu wa sheria iliyopo imefuatwa, wamepewa eno, nyumba na miundo mbinu muhimu, hela ya kujikimu na nauli juu.
Je kipindi cha JPM, wakazi wa pembeni mwa Morogoro road walifanyiwa hayo? Wakati wa tetemeko la Kagera walifanyiwa hayo? Usikumbushe watu machungu!
Tangu lini wafanya biashara wakajiamulia bei? Bei ya mafuta ndio mzizi wa bei ya bidhaa nyingi. Je mafuta wanapanga wafanya biashara au EWURA?
Kuhusu nyufa za bwawa la Nyerere, ukweli ni kwamba Ufa wowote huanzia kwenye msingi, msingi wa bwawa hilo kajenga nani? Sio JPM?
Kuhusu makubaliano ya kushirikiana kuhusu kuendesha bandari zetu na Kampuni ya DP world, unauhakika wanahisa wake ni waarabu tu! Kwa mazingira tata ya uwekezaji aliyoyaacha JPM ulitegemea makubaliano yaweje?
Ndugu yangu kama unavyo sikitika na kujiuliza kwa nini Mungu kamchukua mapema ndivyo na wengi wanavyoenda kwa Mungu huyo kutoa Shukrani kwa kuingilia kati mapema.
Isitoshe, JPM mwenyewe walikuwa akiomba watu wamuombee sana, kila mtu na Mungu wake akamuombea, Majibu yakatoka. Kubaliana na majibu.
Kuhusu kuomba kifo cha JK, Mungu akiyasikia maombi yako, hewala! Kukushauri tu punguza chuki dhidi ya JK, unajiumiza bure.