TANZIA Anayesadikiwa kuwa MwanaJF afariki dunia

TANZIA Anayesadikiwa kuwa MwanaJF afariki dunia

Memba mwenzetu ametangulia mbele ya haki. Pengine nisingejisumbua kuripoti huu msiba lakini mazingira ya kifo chake ni ya kuhuzunisha na yenye mafunzo. Sijui username yake ya JF kwani tulikutana ''casually'' kwenye kilevi mwezi wa tatu mwaka huu tena siku moja tu. Katika maongezi alinijulisha kuwa yeye ni ''active member'' wa JF na anapenda sana kuchangia. Baada ya kilevi (maeneo ya Boko) tulipokuwa tunaondoka akanionyesha nyumbani kwake na mimi nikaondoka kurudi kwetu Msasani ninakoishi.

Fast forward, wiki kama mbili zilizopita nilirudi tena maeneo tuliyokutana kwenye mishe zangu. Nikaona msiba kwenye boma aliloniambia ni nyumba yake. Kuulizia kulikoni nikaambiwa ni yeye, mwenye nyumba amefariki. ''Eti'' alitoka kwenye kilevi usiku, akagonga geti, mke akagoma katukatu kumfungulia. Akachukua uamuzi wa kuruka ukuta. Kwa bahati mbaya akachomwa na moja ya nondo zilizoko kwenye geti la nyumba (nadhani wengi mnafahamu nondo zinazochongwa kama mkuki na kuwekwa juu ya kuta au geti ili kuzuia vibaka). Kwa bahati mbaya akavuja damu nyingi mpaka akapoteza maisha. RIP member.
Kuishi na binadamu mwenzio ni kazi! Yamekwisha, apumzike kwa Amani!
 
Mi napendekeza uweke namba ya Mpesa tukutumie mchango upeleke hapo pasipojulikana ili tuifariji familia ya member asiejulikana na sisi tuliotoa tusijulikane
 
Mungu aturehemu tuliobaki. Siujui mwsho wangu so may his soul rest in peace.
 
Hongereni kwa michango mizuri To yeye na Depal , Wanawake wote wangekuwa huru kama ninyi huenda Dunia ingekuwa mahali salama zaidi kuishi.

Wanaume wenu watakuwa wanainjoi Sana mahusiano yenu.

Pole kwa Kila Mmoja aliyeguswa na Msiba huu.
 
Hongereni kwa michango mizuri To yeye na Depal , Wanawake wote wangekuwa huru kama ninyi huenda Dunia ingekuwa mahali salama zaidi kuishi.

Wanaume wenu watakuwa wanainjoi Sana mahusiano yenu.

Pole kwa Kila Mmoja aliyeguswa na Msiba huu.
Barikiwa sana Mkuu,apumzike
 
ndoa zina mengi hizi,mwanamke alishachoshwa na kufungua geti akaamua amute,mkeo unamfanya sa ngapi ikiwa unarudi usiku wote huo,wanaume badilikeni sio unaoa mke kumtesa.
kuoa sio kufunga tu ndoa kanisani kuna zaidi ya hayo,manhood is not simple as you think
kwa scenario hii hakuna wa kulaumiwa,isipokuwa mke atajuta maisha yake yote,Mungu amtie nguvu nawe uliyetangulia tunakutakia pumziko jema
 
Kwahiyo kuepusha gubu ndio unaona ukwende kushinda bar? Hapo unasuluhisha nini sasa?

Hivi mtu mnapendana na kuheshimiana vizuri hizo gubu zinatoka wapi? Ingawa najua kuna watu wapo both me & ke wana lawama sana
usihukumu kabla hujajua ukweli. kuna wanawake wengine ni controlling na wana gubu sana. pengine jamaa aliamua kuwa anapita bar kuepusha balaa la gubu la wife
 
Back
Top Bottom