Anayesema Moshi pagumu kwa wageni, ugumu wake ni nini?

Wengi wameongea kiubinafsi sana na Kwa chuki kwa wachaga Moshi ni kugumu kweli na Sisi ambao tulizaliwa pale wengi tumekuja mikoa mingine kuangalia fursa za maisha Ila katika mikoa ambayo imebaki na identity yaake Kwa wazawa ni Moshi, mbeya, na mikoa mingi ya kanda ya ziwa Ila kiuhalisia Kilimanjaro ni ndogo sana ukiiacha dar mkoaa unaofata kiudogo ni Kilimanjaro katika mikoa iliyowahi kupata elimu Kilimanjaro ipo Kwa elimu waliyopata na tamadumi Zao si rahisi kuachia ardhi kirahisi na vile mkoa ulivyomdogo tofauti na mikoa mingine na kingine kilichochangia ugumu Moshi ni ubinafsi WA CCM katika maendeleo ya nchi hii kama Tanga ingeachwa kama mji wa Bandar na viwanda vingi vingeendelezwa leoo hii kaskazini ingekuwa mbali snaa kingine jamii nyingine zinaona kama umoja wa wachaga ni ubinafsi ivi unawza Acha kumuungisha rafiki yako kabila lako kwenye biashara ukanunue Kwa mwingine kama unaweza basi jua unaroho mbaya penda watu wenu penda mji wako penda vya kwenu ndyoo uendee Kwa mwingine CCM iliwaaminisha watu vitu vya hovyo sana na sijui hii mentality utatoka Lin vichwani kwenu
 
Dah, mnasambaza uongo mazee, pale ghorofani mbona kuna wa rangi mob na wakinga pale.
Hao wakuhesabu, angalia wale madogo kwenye vibaraza karibu wote ni wa kcmc na wamekaa pale sababu ya Totolii, rudi wanaotokea majengo nao utawakuta connection yao kwa Big na Meshaa, wa rau,KB na Soweto hauwezi wakuta sana sababu hawana foundation pale labda wachache wanatoka nazo shuleni (japo sijui kwa sasa)
 
Mkuu unaijua hata Conveyance kweliii? Au umeamua kujifurahisha tu
 
Moja ya vitu vinafanya Moshi Manispaa isitanuke kwa kasi ni maswala ya mazingira na maliasili, ikumbukwe Moshi Mjini imezungukwa na vijiji na hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, hii inafanya Mji wa Moshi usitanuke sababu watu watakwenda kuharibu uoto wa asili.

Sijajua kwa Mikoa mingine yenye hifadhi za taifa kama utanujaji wake unakwenda taratibu au kuzuiwa kama ilivyo kwa Mji wa Moshi ambao umezungukwa pande zote na vijiji pamoja na hifadhi ya Mt. Kilimanjaro.
 
Kumbe unawajua nje ndani. Ila sasa wanaface mabadiliko nadhani shida ilikuwa ni malezi. Maana Moshi daaah wanawake wa pande zile na Kilimanjaro kwa ujumla ni changamoto eneo la adabu.
Nina wafahamu vizuri na huku tuna matabaka ya wachagga pia πŸ˜… ukikutana na mchagga mwenzako town unajua huyu ni mchagga mwenzangu toka sehemu fulani so kuna aina ya mchagga sintomuelewa lugha hata akizungumza mfano mi Mrombo siwaelewi wakiongea kichagga chao yaani naweza daka neno moja japo ni uncle zangu kwa mama.

ila wakiongea wamachame au wauru nitawasikia sababu mi mkibosho labda πŸ€‘ sasa hata wadada wa kimarangu hawafanani kitabia na wadada wa kibosho wapo tofauti vile vile wa kimachame pia, wote hawa nawajuaga wapole wapi na gia ya kuwaingilia ni ipi πŸ˜…πŸ˜
Tatizo moja hawa dada bhna ole wako wajue wewe sio mchagga mwenzao na sio hivo tu wajue udhaifu wako πŸ˜… lazima uteseke, mi nikwambie tu hawa mi nakuwaga mukuria amna kabila dada zetu wanaogopa kulisikia hapa Tanzania kama wakuria au wamasai au pia aolewe na mchagga mwenzake wa kabila moja huwa hawana ujanja sana😏😏😏
 
Watu wamelishwa sana Matango pori kuhusu jamii ya kichaga kwamba ni wabinafsi n.k. wasijue hata chembe baadhi ya mambo yanayochangia mfano kutoboa moshi kibiashara.
 
Huwezi kuona ajira zikiwepo na biashara zitakuwepo, amna aliyekatazwa kuinvest there's nothing like monopoly system πŸ˜…
The main investor in the Economy is the Government, not individuals. Kwa hiyo Moshi lazima Kibaki nyuma kwani ni uamuzi wa serikali kuu kutokuwekeza Moshi huu ndio ukweli. Mtabakia na biashara za uchuuzi tu.
 
Mkuu,ni ngumu sana kushawishi watu wabadilike kimtazamo kwa taarifa walizorithishwa vizazi na vizazi..
Pengine muda utakuwa mwalimu mzuri..
Nimekaa na hii jamii kwa muda mrefu sana..Nimejifunza kujudge mtu mmoja mmoja..badala ya kuweka wote kwenye kapu moja..

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
The main investor in the Economy is the Government, not individuals. Kwa hiyo Moshi lazima Kibaki nyuma kwani ni uamuzi wa serikali kuu kutokuwekeza Moshi huu ndio ukweli. Mtabakia na biashara za uchuuzi tu.
It can be also sound like that....
 

wachaga wamechanganyikana na makabila mengi hapa Tanzania. naweza kusema hakuna kabila lililooleana na makabila mengine kuliko wachaga. pia hakuna kabila ambalo watu wake wametawanyika maeneo mengi ya Tanzania kuliko wachaga.

shida iliyoko katika mji wa Moshi mpaka ukaonekana ni mgumu kwa watu wanaoanza biashara ni uchache wa fursa zilizopo. pia ni mji ambao hauna mzunguko wa fedha mkubwa kulinganisha na miji mingine. Moshi ni mji wa zamani na hakuna biashara mpya au fursa mpya zilizojitokeza kwa miongo kadhaa kuvutia jamii mbalimbali kuhamia huko.

Kwa mfano, Moshi hakuna biashara ya madini kama Arusha, Kahama, na kwingineko. Moshi pia hakuna biashara ya mazao kama mahindi, mpunga, etc ambayo yatavutia watu kutoka nje. Moshi na Kilimanjaro kwa ujumla hakuna maeneo mapya yenye rutuba ambayo yanavutia watu wengi kuhamia huko.

lakini pia ishara ya wazi kabisa kwamba Moshi / kilimanjaro kuna fursa chache ni idadi ya wenyeji wa huko ambao wamelazimika kuhamia maeneo mengine ya Tanzania kutafuta maisha. kwa hapa Tanzania ukiona eneo fulani linakimbiwa hata na wenyeji uwezekano mkubwa ni kwamba hata mgeni akihamia huko hatofanikiwa.

kwa upande mwingine mimi nawafahamu jamaa wa kipare wako maeneo mbalimbali uchagani na wamefanikiwa kibiashara. lakini jamaa hao walihamia huko miaka ya 80 na 90 na walianza kama wafanyabiashara wadogo na sasa wamekuwa vigogo.
 
Hakuna cha ku single out! We bila shaka ni mkazi wa Dar pia. Huo upuuzi umeuona mahali gani hapa Dar es Salaam?

Hivi kuna mtu anafuatilia wewe umefungua biashara gani hapa mjini! Maduka ya nguo yamepangana kariakoo ila huwezi kukuta watu wananunua duka flani eti kwa sababu ni la Mchaga mwenzao au duka flani sababu ni kwa mkinga mwenzao! Hotels, Bars ni hivyo hivyo yani hamna ubaguzi eti silali Rombo view sababu ya mchaga πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Huo ujinga uko Moshi tu!

Hamna huo utoto mjini na ndio maana hao jamaa wamekimbia kwao wamekimbilia Dar.
 
Hapo tu kwenye population ni uhuni na uongo unaongea..

Tax records Moshi inakusanya zaidi ya jiji la Mwanza. Sasa sijui unaongelea nini hasa..

Alafu unavyosema Moshi hakuna kilichobadilika ni upuuzi na chuki zako kwa watu wa jamii hiyo

Ndio maana nawatizamana wanavyoandika ujinga nasema hiiiii
 
Mkuu mimi nipo huku, usifanye nianze kazi ya kupiga picha za kukudhalilisha humu.
Hahaha bdo unaendelea kubisha? Uchagani makaz Bora ni 90% yaan kila ukitembelea nyumba 10, 9 ni za kisasa(nzuri) indicator mojawPo ni kwamba uchagani yote haina hata nyumba moja ya nyasi kama kule kwenu Lindi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…