Kila siku hapa huwa tunasema kuwa mwanaume anapopata mafanikio ya kiuchumi huwa anauwezo wa kulala kingono na wanawake wengi tofauti tofauti ila huwa anachagua kutafuta mwanamke m'moja mzuri anayejitambua na kuanzisha nae maisha na kuwa Mume na mke na kujenga kiota chao waishi kwa upendo na kujenga ukoo.Ki ukweli huyu dada nami nilikubali sana kabla hajaanza hata kuimba
Tulikuwa tunashiriki naye kwenye huduma moja Dar ikiitwa New life crusade
alipoanza album yake akawa maarufu sikumuona tena akihudumu kwenye semina na mikutano
mbali mbali nikajua amezidiwa na huduma,sasa naona huduma zimeongezeka,nipo njia panda
nashindwa nimtakie kila la kheri, au nimshauri arudi nyumbani
At least umeongea jambo linalomake sense. Robert Heriel Mtibeli angekuja kihivi kidogo tungejadili mada ya kueleweka ila sio pumba alizoandika hapa. Ameamua kuwa w****'s advocate.Watu wenye pesa wanaume hupenda kuoa au Ku-date na wanawake ambao wapo financial broke ili kuwafanya kuwa submissive - kuwatii wanaume.
Na ndoto kubwa ya masikini huwa ni kulipiza Mapito yao waliyofanyiwa Kama , kudharauliwa, kutukanwa , kuteswa , hivyo msamaha wa MTU masikini ni kisasi.
Shusho anachopitia sio mapepo wala dharau kwa mme wake .
Isipokuwa anajaribu kuishi katika dark side yake.
Na dark side hakuna MTU ambaye Hana dark side.
Si ndio hapo mkuu, ndio maana namwambia Mleta mada aachane na Hilo suala.Miaka 20 ya ndoa, huyu kalazimishwaje kuishi na mtu miaka 20,miaka 20 alikuwa akitombwa hapati raha? [emoji848]
HahaaaaTuanze kuimbaa
''Mtetezi wangu Yesuu!!! Anaishi leoo!!!,
mtetezii wangu yu-haii!.''
Au basi twende na hii
''Mungu alipo-muumba Adamu!!,
hakumuacha awe pekee yake,
akamfanyia na msaidiziii!!,
wakuu-fanana nayee!!''
Dj.. Dj..
Angekuwa ni nandy, giggy money, shilole au lulu wala hakuna ambaye angeshangaa...ingeonekana ni kawaida.
Tatizo linakuja kwamba ni mwimbaji wa
Dini...Dini ambayo wengi tunaamini ndio mahali pa faraja..anapoasi kwa style hiyo.
Tukumbuke pia, Tina sio binti.wala mdada kama akina frola mbasha..ni jimama..ana watoto wa kuolewa na kuoa...probably hata wajukuu siajabu anao...inashangaza sana
Credit ziende kwa mleta threadPoint kubwa sana hii.
Kama Tulia AksonMwanamke anayejua haki zake ni yupi
Kaka mpare nimependa umetumia lugha ya kiungwana maana alistahili ya kukalipia,yaani anachukulia ndoa kama taasisi ya kibiashara mbinu za kuajiri wafanyakazi analeta kwenye ndoa.Nimesoma post yako kama nusu tu nikaona huna uelewa wa mambo ya Ndoa hivyo huna sifa ya kuandika mambo yanayo husiana na ushauri wa ndoa; unge endelea na yale mengine ya kisiasa
1. Kudhibitisha kuwa huna sifa ya kuongelea mambo ya Ndoa, umeweza kumsikiliza Christina Shusho na kuamini kila anachosema na kutoa hukumu wakati hujasikiliza upande wa pili wa mUme wake
2. Kwa maelezo yako ni kuwa, mwanamke asiolewe kama hana kazi au niseme wanaume wasije kuoa wanawake wasio na kazi au Kipato; sijui unajua ni asilimia ngapi ya wanawake au niseme vijana wenye kazi?
3. Kama unafikiri mtu akioa mke kwa sababu anataka asifanye dhambi ya kuzini mtaani ananyanyasa mke wake kwani anataka kufanya tendo la ndoa; inabidi ujitafakari upya...
4. Hiyo ya kusema mke asilipiwe mahari sijui umetoa wapi????
5. Kwa wenye maarifa wanajua kuwa, masuala ya ndoa sio mepesi kama kuongelea Siasa au pengine kuongelea mpira wa Yanga & Simba
Mungu hakupi vyote amejaliwa kipaji na uzuri lkn hakujaaliwa kuolewa na chaguo lakeCHRISTINA SHUSHO AMEMKOSEA MUMEWE, ATUBU
Kitendo cha Christina Shusho kusema kwamba aliozeshwa akiwa mdogo bila idhini yake ni kumdhalilisha huyo aliyekuwa mume wake kwamba alikuwa mkubwa sana kwake (mzee) na alimuoa kimabavu, kwanini hakuachana nae kipindi hicho hicho au kwenda kushtaki? Au kuna kitu alikuwa anapata hakipo tena ndio anaamua kumchafua? Maswali ni mengi yenye mashaka
Nmeona video anahojiwa hata pete ya ndoa hajavaa anaulizwa kwann anasema ni suala la makubaliano aliamua kumuacha mumewe kwenda kutimiza ndoto zake na ilikuwa kwa amani anasema habari za mume na mke kuwa mwili mmoja kwake siku hizi hazipo. Kule kwa mumewe alipokuwa anasema akiamua anaenda kutembelea tu. Hii sio sahihi ndugu zangu.
Imefika hatua anasema kwamba hapendi kuitwa pastor Christina Shusho anasema yeye sio mchungaji ila ana watu wa karibu wachungaji yeye hajiskii vizuri kuitwa pastor, kweli? Muimbaji wa nyimbo za Injili unaehubiri kupitia nyimbo hutaki kuitwa mchungaji??? Unaogopa nin? Ni mambo gan hasa yanakupa aibu kuitwa pastor?
Binafsi nasimama na huyo mume, naona suala la ndoa la Christina Shusho limekaa upande mmoja yeye tu ndio anaongea kwenye media na majukwaa mbalimbali kwamba alifosiwa kuolewa mara alijitoa kwenye ndoa kutimiza maono yake nk ukweli unabaki kwa mume huenda nae ana mengi ya kuzungumza ila ana kifua, sio ropo ropo.
Nadhani siku huyo mzee (ambaye Christina anadai aliozeshwa kwake akiwa mdogo kwamba ni mkubwa sana kwake) akiongea huenda tukakosa pa kuficha sura zetu yanaweza kuwa mambo mazito mno
Nadhani mume ameamua kutumia busara kukaa kimya kuepusha taharuki kubwa zaidi
Sioni kama kulikuwa na haja ya Christina Shusho kuongelea haya mambo hadharani yalipaswa kuwa binafsi
Wanawake jifunzeni, mambo ya ndoa sio ya kuweka hadharani.
Bila Me na Ke..... wewe ungekuwepo duniani. Na usingeandika bandiko hili.........inawezekana huna mke au mkeo anakutawala.Jambo kuwa kiasili haimaanishi ni HAKI.
Niliwahi andika hivyo lakini haimaanishi nililiunga mkono.
Mwanamke aolewe katika umri ambao kwa hiyari yake anataka kuolewa.