Andiko la mchekeshaji Shafii, limeniumiza sana mimi kama kijana

Andiko la mchekeshaji Shafii, limeniumiza sana mimi kama kijana

Kuhusu wanawake wa dodoma na wazazi wao hiyo ni kama desturi, yaani uki date na mwanamke kutoka dodoma tegemea jambo kama hilo

Ilimitokea mimi na mwanamke alilazimishwa kuolewa na akaenda na akaolewa

wazazi wake walikula pesa ya mahali ya shillings milioni 1, binti akanambia nikataka niitoe kama mahali na nilisema ikibidi nitaiongeza hiyo pesa, walikataa katu katu, nikakosa mke kwa mtindo huo

Cha ajabu baada ya kuzalishwa jamaa alimuachaga yule msichana akarudi mjini akawa anadanga tu

Wazee wa dodoma hii ni kawaida yao
 
Nimeumizwa sana na mchekeshaji shafii, huyu kijana alikua na mchumba wake, wakishirikiana vizuri tu. Baadae kapata taarifa mchumba wake kaolewa Dodoma, kumbe yule Binti kalazimishwa na wazazi wake pamoja na kaka yake, kisa kazi ya shafii wao waliona ni ya kijinga sijui ni ya kimaskini, kazi ya shafii ni uchekeshaji, hivo wao hawakufurhishwa nayo. Wakabeba mtoto wao akaolewe na mwanaume mwingine.

Unaambiwa Binti kalia sana Kwa wazazi akaishi na mtu anae mpenda, lakini jibu alilo pewa ni kuwa akitoa mguu wake kwenda kuolewa au kuishi na shafii mchekeshaji, basi wao si wazazi wake tena na asikanyage nyumbani kwao.

inasikitisha sana, vijana oeni msikae timu kataa ndoa, vijana wanataka kuoa mnawanyanganya na kudai hawana hadhi. Daaah
huenda Mwenyezi Mungu kamuepusha na shari ambayo ingempatia masikitiko na huzuni maisha yake yote huyo mchekeshaji. Na sio rahisi wengi kufikiria hivi.

Nadhani kijana anapaswa kumshukuru Mungu tu, na kumuomba baraka na neema zake aweze kumpata mwingine alie sahihi zaidi na mwenye msimamo thabiti katika shida na raha, magonjwa, dhiki, faraja n.k

Ni wazi muungwana bado ni kijana, na changamoto hiyo anafaa kuichukulia kama fursa muhimu zaidi ya kujipanga upya na maisha mapya ya mahusiano mapya. Bado anayo nafasi na fursa ya kufurahia maisha ya mahusiano na pengine ndoa takatifu yenye amani na furaha zaidi, pengine kuliko hata angekua na huyo alemsaliti kwa msukumo wa wazazi wake.🐒
 
Kuhusu wanawake wa dodoma na wazazi wao hiyo ni kama desturi, yaani uki date na mwanamke kutoka dodoma tegemea jambo kama hilo

Ilimitokea mimi na mwanamke alilazimishwa kuolewa na akaenda na akaolewa

wazazi wake walikula pesa ya mahali ya shillings milioni 1, binti akanambia nikataka niitoe kama mahali na nilisema ikibidi nitaiongeza hiyo pesa, walikataa katu katu, nikakosa mke kwa mtindo huo

Cha ajabu baada ya kuzalishwa jamaa alimuachaga yule msichana akarudi mjini akawa anadanga tu

Wazee wa dodoma hii ni kawaida yao
Wana njaa hao, yani wako radhi Kwa lolote ilimradi wapate pesa tu
 
Kuhusu wanawake wa dodoma na wazazi wao hiyo ni kama desturi, yaani uki date na mwanamke kutoka dodoma tegemea jambo kama hilo

Ilimitokea mimi na mwanamke alilazimishwa kuolewa na akaenda na akaolewa

wazazi wake walikula pesa ya mahali ya shillings milioni 1, binti akanambia nikataka niitoe kama mahali na nilisema ikibidi nitaiongeza hiyo pesa, walikataa katu katu, nikakosa mke kwa mtindo huo

Cha ajabu baada ya kuzalishwa jamaa alimuachaga yule msichana akarudi mjini akawa anadanga tu

Wazee wa dodoma hii ni kawaida yao
Basi vijana wachukue tahadhari na mabinti wa huo mkoa😁
 
Kenge huyo Shafii upendo huwa unakujaa mwishoni.1.Kuhudumia 2.Kuongoza 3.Kupenda.Wazee na mimi mwenyewe nikimpigia mahesabu ya mbali huyo tutusa naona chekibobu tu anayetaka kuharibu maisha ya Binti wa watu.
Mkuu kisa ni muonekano wake au? Hiyo ni kazi yake inayo mpa riziki, hakabi Wala haibi mkuu
 
Nilihaidi kulipa pesa zaidi lakini wazazi wake walikataa

Ila nilifurahi sana yule binti alipoachwa na aliyemuoa, roho yangu ililidhika sana aisee

Kweli wana tamaa wapo radhi wafanye lolote ili wapate pesa
Inasikitisha sana mkuu japo, si sawa kufurahi ex wako anapo endewa mlama na maisha
 
Inasikitisha sana mkuu japo, si sawa kufurahi ex wako anapo endewa mlama na maisha
Boss, hakuna mahusiano yaliyowahi kuniyumbisha maisha yangu kama yalee aisee.

Ilee familia ingeniua; nilitokea kumpenda yule binti daaah.. sasa hivi siwezi kupenda tena nikiwa kwenye mahusiano nakuwa tu kwenye mahusiano ila sipendi kwamwe, akitaka akae asipotaka aende ila siwez kumcheat wala nn?
 
Back
Top Bottom