Andiko la mchekeshaji Shafii, limeniumiza sana mimi kama kijana

Andiko la mchekeshaji Shafii, limeniumiza sana mimi kama kijana

Boss, hakuna mahusiano yaliyowahi kuniyumbisha maisha yangu kama yalee aisee.

Ilee familia ingeniua; nilitokea kumpenda yule binti daaah.. sasa hivi siwezi kupenda tena nikiwa kwenye mahusiano nakuwa tu kwenye mahusiano ila sipendi kwamwe, akitaka akae asipotaka aende ila siwez kumcheat wala nn?
Shida ilikua Nini mkuu, mpaka kusema walitaka kuku ua
 
Nimeumizwa sana na mchekeshaji shafii, huyu kijana alikua na mchumba wake, wakishirikiana vizuri tu. Baadae kapata taarifa mchumba wake kaolewa Dodoma, kumbe yule Binti kalazimishwa na wazazi wake pamoja na kaka yake, kisa kazi ya shafii wao waliona ni ya kijinga sijui ni ya kimaskini, kazi ya shafii ni uchekeshaji, hivo wao hawakufurhishwa nayo. Wakabeba mtoto wao akaolewe na mwanaume mwingine.

Unaambiwa Binti kalia sana Kwa wazazi akaishi na mtu anae mpenda, lakini jibu alilo pewa ni kuwa akitoa mguu wake kwenda kuolewa au kuishi na shafii mchekeshaji, basi wao si wazazi wake tena na asikanyage nyumbani kwao.

inasikitisha sana, vijana oeni msikae timu kataa ndoa, vijana wanataka kuoa mnawanyanganya na kudai hawana hadhi. Daaah
Kama kweli huyo demu kafanya maamuzi kwa ajili ya fedha atarudi, nimeshuhudia kwa mademu kama wawili na wanakuwa tayari kuwa hata vidumu.
 
Una kaa na binti wa watu miaka mitano 😳,Safi sana wazazi wa huyo binti no kuongeza Single mama
Ila hapo kwenye miaka mitano, mhh kweli haikua busara kama ni pika pakua, hapana aisee, mitano mingi sana labda kama, walikua makazi tofauti
 
Kama kweli huyo demu kafanya maamuzi kwa ajili ya fedha atarudi, nimeshuhudia kwa mademu hawa wawili na wanakuwa tayari kuwa hata vidumu.
Hapana demu hana noma kwani unaambiwa sasa analoa tu shida wazazi ndo wamemkataa jamaa
 
Wazazi huleta nyoko ila binti akikomaa na mshikaji wake kibishi wazazi huja ku appreciate hapo baadae mambo yatakapokuwa bam bam
 
Wamekaa kwenye mapenzi miaka mitano, aliwahi taka kutoa mahali wakamkatalia? Au alikuwa na "nia njema" kwa mdomo tu na si vitendo.

Mimi ningekuwa kaka wa huyo dada ningemzaba vibao kudate na huyo jamaa miaka mitano bila bila.

Btw hakuna mzazi anataka binti yake aolewe na mtu ana career haisomeki na character ya mashaka.
Shafii si amesema hapo wazazi wa binti wamemkataa au
 
Miaka mitano(5) bila binti kula udongo,kupata kichefuchefu,kula ndimu,kutema mate kwenye kikopo na kuota kitambi?

Ndugu yetu ajitafakari sana kama hii story yake ni ya kweli, unaishije na mtoto wa mtu miaka mitano kizembe? Maana angelimtia mimba wasingemtafutia mtu mwingine amuoe.

Pia kwa hizi pigo zake kulialia mitandaoni, hiyo familia ina haki ya kufanya walichofanya.

#Hallelujah!!!
 
I walk on the sky, can't let any shit get over me that ain't no lie.

Pure taliban moves, just cruising around with immaturity
 
Nimeumizwa sana na mchekeshaji shafii, huyu kijana alikua na mchumba wake, wakishirikiana vizuri tu. Baadae kapata taarifa mchumba wake kaolewa Dodoma, kumbe yule Binti kalazimishwa na wazazi wake pamoja na kaka yake, kisa kazi ya shafii wao waliona ni ya kijinga sijui ni ya kimaskini, kazi ya shafii ni uchekeshaji, hivo wao hawakufurhishwa nayo. Wakabeba mtoto wao akaolewe na mwanaume mwingine.

Unaambiwa Binti kalia sana Kwa wazazi akaishi na mtu anae mpenda, lakini jibu alilo pewa ni kuwa akitoa mguu wake kwenda kuolewa au kuishi na shafii mchekeshaji, basi wao si wazazi wake tena na asikanyage nyumbani kwao.

inasikitisha sana, vijana oeni msikae timu kataa ndoa, vijana wanataka kuoa mnawanyanganya na kudai hawana hadhi. Daaah
Dogo asiwe na pressure, ashushe pumzi akubaliane na hali japo si rahis

Kwa uzoefu wangu ndogo ambazo ni za kulazimisha huwa hazina uhai wa muda mrefu why sababu upendo na mapenzi haviko pale.

Msingi wa ndoa yoyote ni mapenz ya kweli, si ya upande mmoja. Msingi ukikosekana
Huo muunganiko hata miaka mi 6 hautofika
 
Atakubali kuwa step father kwa single mother?
 
Vijana, Kila siku usisahau neno hili "MUONEKANO" mara nyingi hili neno linaweza kukuondolea au kukuondoa karibu na watu unao wapenda kwasababu neno hilo linaweza kukufanya uwe au uwekwe kwenye maswali mengi hasa katika jamii zinazoamini mila na desturi...

Mwambieni atoe rasta kichwani zile
 
Back
Top Bottom