Andrew Chenge achukua fomu ya kugombea Uspika. Fahamu kuhusu wasifu wake

Andrew Chenge achukua fomu ya kugombea Uspika. Fahamu kuhusu wasifu wake

Very smart Kichwani, ambacho wengi hawajui ni kuwa "ufisadi mkubwa mkubwa, dili kubwa kubwa za wanene,huyu ndy Engineer wapi tuingilie na wakitupeleka korti tunatokea pale".Hii machine mujarabu ya kusafisha dili kubwa kubwa!! Huyu hunfungi ata utambike.!!Hii ni lulu ya Chama chao usipime!!
Ni msomi type ya Mugabe,kamuzu banda,savimbi,waliotumia elimu zao kuharibu nchi zao.
Wenzetu usoma Ili kuzijenga nchi zao
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
Mama angeongeza Wizara ya Uchawi na Mambo ya Utamaduni halafu akamkabizi huyu bwana nyoka.

Ili kazi yake iwe kiwaroga wananchi ili waendelee kuwa Ndoho tabhu kama Mazombi.
 
Hivi huyu si ndio Chenge aliwagonga wasichana wawili akawaua walikua kwa bajaj pale Oysterbay??? na hakua na insurance??? kweli mwenye pesa sio mwenzio, hii bongo imelaaniwa wallah laadhim.....HAFAI.
 
Chenge afai atapitisha mikataba ya upigaji huyu mzee kwenye dili la pesa macho uingia giza.
Dili zote kubwa za wizi yupo atosheki tu.
 
Hizi ni dalili za umasikini uliotopea. Hutaki mtu akuzidi, hutaki kusikia mafanikio ya wenzako. Chuki hizi mnazitumia hadi muwapo makazini na mwisho mnakuwa wafitini.
Kuna watu ufisadi wao ni wa kumulika na kurunzi; ila si babu yako Andrew Chenge! Ni aibu na fedheha kubwa sana kwa taifa hata kulitaja tu jina la jipu hili kwenye sentensi ama suala lolote jema kwa taifa!
 
Huyu ni zaidi ya fisadi asiye ogopa kushitakiwa
Basi atakuwa FASIDI--mtu atumiaye mamlaka ya elimu, ushawishi, na pesa ili kujipatia, kilaghai na udanganyifu, mali na cheo ambacho vinginevyo asingeweza kupata.
 
KUZALIWA

- Mbobezi wa Sheria Barani Afrika na "Alumni" wa Chuo kikuu bora Duniani- Havard cha Nchini Marekani Mh.Andrew John Chenge alizaliwa mwaka 1947 nchini Tanzania (Tanganyika wakati huo).

ELIMU

- Nguli huyu wa Sheria alianza safari ya kitaaluma katika Shule ya msingi Sasago (Musoma) kati ya mwaka 1955- 1958

- Kisha akajiunga na St. Pius Seminary Makoko Musoma kati ya mwaka 1959-1962

- Kisha akajiunga na St.Mary's Seminary Nyegezi mwanza kati ya mwaka 1963-1966 kwaajili ya masomo ya Sekondari.

- Kati ya mwaka 1967 - 1968 alijiunga na Mkwawa High school.

- Mwaka 1969 alikuwa kati ya wanafunzi wachache waliojiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwaajili ya masomo ya Sheria (LL.B) na kufanikiwa kuhitimu kwa ufaulu wa juu mwaka 1972.

- Mwaka 1974 - 1975 alibahatika kuwa kati ya wanasheria wachache Duniani kujiunga na Chuo Kikuu cha Havard kwaajili ya Shahada ya uzamili aliyohitimu kwa ufaulu mkubwa.

UTUMISHI NA UZOEFU SERIKALINI

- Kati ya mwaka 1972 - 1990 alihudumu kama mwanasheria wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

- Kati ya mwaka 1990- 1992 alihudumu kama Naibu Mwanasheria Mkuu (D/AG)

- Kati ya mwaka 1993 -2005 alihudumu kama Mwanasheria mkuu wa serikali.

- Mwaka 2006 alihudumu kama Waziri wa Kwanza wa Ushirikiano wa Afrika mashariki

- Kati ya 2006-2008 alihudumu kama Waziri wa miundombinu katika serikali ya awamu ya nne.

UZOEFU KATIKA BUNGE

- Kati ya mwaka 2005 - 2020 alihudumu kama Mbunge wa Jimbo la Bariadi Magharibi

- Kati ya mwaka 2008 - 2010 alihudumu kama mjumbe wa kamati ya Bunge ya Uchumi na Fedha.

- Kati ya mwaka 2012-2013 alihudumu kama Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uchumi na Fedha

- Kati ya mwaka 2013-2015 alihudumu kama Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Bajeti

-Kati ya mwaka 2015- 2020 alihudumu kama Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Sheria na pia kama mmoja wa Wenyeviti 3 wa Bunge.

#Bunge linahitaji kiongozi wa makamo kama Chenge
5ce361d4-6ca4-4b4f-996e-4004559e373d.jpg
 
Back
Top Bottom