Andrew Chenge afika kwenye Kamati ya Katiba, awataka Wajumbe warudi kwenye Rasimu ya Warioba

Mtu yeyote anayetaka kukwepa Rasimu ya Warioba basi ana jambo lake na hana nia na katiba mpya
 
Amedai ni kweli si rahisi kumzuia Rais wa Nchi kuteua Maofisa wa Serikali , lakini anawateua kwa utaratibu gani ? ni lazima Wateuliwa Waombe nafasi na Wasailiwe , amesema utaratibu huu ndio utakoiletea heshima nchi .
Wazee wa mtelezo a.k.a chawa wa uteuzi wakiona kauli hizi wanachachawa🤣🤣🤣
 
hakumung'unya maneno , amewataka wajumbe wa Kamati hiyo kurejea kwenye Rasimu iliyopendekezwa na Wananchi , Amedai ni kweli si rahisi kumzuia Rais wa Nchi kuteua Maofisa wa Serikali , lakini anawateua kwa utaratibu gani ?
Na mimi simung'unyi maneno, je hakuwemo kwenye BMK wakati ule!?
 
NI kweli mzee chenge amepatia.kuwa waziri wa mambo ya ndani alafu unadai katiba mpya ya warioba.anahitaji kupongezwa Sanaa mzee chenge
Kuna wakati saa mbovu ya mshale huonyesha majira sahihi. Chenge ni saa mbovu ya mshale iliyoonyesha majira sahihi.
Katika hili ninampa hongera Chenge.
 
Maoni yake ni mabaya?. Mtu kasema tutumie rasimu ya warioba inayo ungwa mkono na upinzani. Ulitaka upinzani wabadilishe msimamo wao kisa Chenge?.
)
NI kweli mzee chenge amepatia.kuwa waziri wa mambo ya ndani alafu unadai katiba mpya ya warioba.anahitaji kupongezwa Sanaa mzee chenge
Chenge waziri wa mambo ya ndani??🤔
 
Leo Chenge ni Mzee mwenye Busara? Hii nchi ngumu sana.... 🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…