KERO Angalia Barabara toka Dodoma kwenda Iringa. Serikali ijitafakari

KERO Angalia Barabara toka Dodoma kwenda Iringa. Serikali ijitafakari

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Alafu serikali inahamishia burden kwa madereva eti wanawakata point kwenye driving licence zao kwa kusababisha ajali au makosa ya badabarani, hivi katika hali ya kawaida kabisa barabara kama hii itamuacha dereva salama?
Tunasema Serikali Kazi Yao Ni Kuhamisha Goal
Wanawalazimisha Madereva Wanaonekane Hawafai
Kusoma Kila Mara Wakati Viongozi Wakipata Diploma Degree
Mpaka Afe Nayo
 
Kuna ya dsm to mtwara aisee ile barabara noma mkuu.
Sema kushughulikia matatizo ya wengi ni kazi kubwa sana ila basi tu yaan unakaa pale mtu mmoja inabidi ushughulikie watu wote wanaokupinga na wanaokukubari sio kazi kidogo, mtwara ndio kuna barabara mbovu kibao zingine miradi haikuisha zimetelekezwa tangu Magu aende zake
 
Sasa hujafika pale getini Mtera kwenye kile kiteremko kuna kichefu chefu kikali sana.

Moja kati ya Barabara nzuri sana kimatumizi ila ki uharisia ni hatari zaidi kama hujui na uko na haraka zisizo na maana.

Hata hii T1 ni mbovu mbovu...kuanzia Kibaha hapo Mpaka unafika Tunduma..moja ya barabara hatari sana kutembea nayo.Lolote chochote saa yeyote unaenda na maji mchana kweupe.
 
Hii barabara imejengwa 2013, na sasa imesha haribika.

Sijui ni ubovu wa materials au Rushwa pindi wanatengeneza hizo barabara. 🤒
Rushwa na kutaka sifa tuna kilomita kadhaa za lami.
 
Alafu serikali inahamishia burden kwa madereva eti wanawakata point kwenye driving licence zao kwa kusababisha ajali au makosa ya badabarani, hivi katika hali ya kawaida kabisa barabara kama hii itamuacha dereva salama?
Barabara kama hii huwezi kupata ajali maana haina surprises,mwanzo mwisho ni mashimo hivyo unaenda kwa minyato. Barabara hatari ni ile unaamini lami imenyooka unajiachia mara ghafla bonge la shimo ukikwepa chali,ukilivaa kichakani. Hio ilinikuta Dodoma-Morogoro ilibidi nirudi kwenye mwendo wa mjini 60-80kph.
 
Back
Top Bottom