KERO Angalia Barabara toka Dodoma kwenda Iringa. Serikali ijitafakari

KERO Angalia Barabara toka Dodoma kwenda Iringa. Serikali ijitafakari

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Hii barabara imejengwa 2013, na sasa imesha haribika.

Sijui ni ubovu wa materials au Rushwa pindi wanatengeneza hizo barabara. 🤒
Waziri wa "mabarabara" wa wakati huo alikuwa nani mkuu?Tukumbushe?😂😂😂😂
 
Nimepita hiyo barabara hivi karibuni, ni moja ya barabara mbovu kuendelea kutumika.

Ni ajabu inatumika na Wabunge wa Mikoa ya Iringa, Njombe, Ruvuma, Mbeya, Songwe, Rukwa n.k huku wakiendelea kuwa mabubu pasipo kuipigia kelele

Hata spika aliyestaafishwa naye alikuwa akitumia barabara hiyo hiyo pasipo kuisemea

Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Kasekenya naye anaendelea kuitumia ikiwa hivyo hivyo

Siku wakipoteza maisha abiria 30 ama 40 watakuja mbele za camera wakitoa pole wakati muda wa kuirekebisha upo 🙌
Mkuu kwani hata barabara zinahitaji ''kusemewa''? Ukiwa kwenye zile nchi zenye viongozi wa kweli, kila barabara kubwa inajulikana ilijengwa lini na life span yake, yaani itakarabatiwa lini. Unakuta wanakwangua lami ya juu kabla hata barabara haijawa na mashimo. Ratiba za matengenezo ndiyo zinaongea na pia wanafanya ukaguzi kila mara. Huku kwetu utambiwa Kiziga na Abdul walipiga fedha ya ukarabati wakaenda kununua magari ya kifahari.
 
Nimetoka huko last wiki now nipo garage mataka taka kibao chini ya gari yameharibiki na nilibugi kuendesha usiku
 
Nimepita hiyo barabara about a month ago, aisee ni kipengele. Kuna mashimo unaweza kufuga samaki.
 
Back
Top Bottom