KERO Angalia Barabara toka Dodoma kwenda Iringa. Serikali ijitafakari

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Mkandalasi yupo site .....kama mtoa post umepita hii njia Leo au Jana nadhani umemuona mkandalasi kwahyo si vema kulalamika wakati umeona ukarabati unaendelea. Shida siyo ujenzi wa barabara shida ni jiografia ya eneo huska ukiangalia tu utagundua aina ya udongo wa eneo ambalo mkandalasi yupo site.

NB: mm nimepita hiyo njia Jana nikitokea Iringa. Nipo tayari kuweka ushahidi wa tiket na picha za mkandalasi akiwa site
 
Nadhani barabara ilishakufa kilichobaki ni viraka tu...
 
Kwa kweli hii Nchi yetu, utasema haina Viongozi.

Ukienda TANROADS wana huo mpango wa ukarabati kadri ya life span ya barabara husika

Changamoto ni utoaji wa vibali na fedha za utekelezaji wa hiyo mipango yenyewe
 
Hapa magari ya mizigo yanalamba nyasi, utafikiri uko Congo vile, tena hiyo nayo imewekwa kwenye data base ya barabara yenye lami, halafu tukiitwa MANYANI tunakataa na kulia tunabaguliwa.
 
Sio hiyo tu Barabara Zote Kuu nchi hii zimeozaa na zinashida kubwa kwa kweli ni aibu haiwezekani hii nchi kipindi cha Magufuli barabra zilikua nzuri leo hii zimeoza zoote....Hakuna ukarabati na Waziri aliekuepo Ulega yule hamna kitu kabisa....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…