Angalia daraja Mbuchi na Mbwera Kibiti la Bilioni 7.2 lililojengwa na Rais wetu Mpendwa Samia Suluhu. Tujipongeze

Bilioni 7.2 kwa urefu wa mita 61 tena single lane bila kuwa na pedestrian. Ni wizi mkubwa hapo tayari, mleta mada umemuharibia mama badala ya kusifu.
Huo mstari wako wa mwisho ndo lengo la mleta mada.. ujumbe upo indirect zaidi
 
'vita ya urusi na ukraine' imepandisha bei za malighafi
 
Hizo ni gharama za daraja pamoja na barabara ya Mohoro- Mbuchi- Mwera, yenye urefu wa km 35 na sio daraja peke yake.
Ahsante mkuu!
Jf hii, ukiisikia habari ipokee kwa umakini kweli.......watu humu wanazusha balaa, na watu humu wanakurupuka kupokea vilivyorushwa bila kutafakari balaa. Wakiona kichwa cha habari tu wameshakimbilia kucomment lawama, kama kawaida yao.

Siajabu hata hiyo taarifa mtu hata hana, ameona daraja na kusikia bil 7 point kadhaa zikitajwa basi ameunganisha taarifa yeye mwenyewe na kuja kuwapatia haters wa mama wapate sehemu ya kujifajia.
 
Hivi unajua bil 7 wewe?! Inashangaza mno kwa hela zote hizo kujenga daraja la kuunganisha vyuma. Madaraja hayo ni ya dharura na hujengwa na Jeshi kwa muda mfupi sana na hilo halipaswi kamwe kuzidi billioni 2!
 
Nyie endeleeni kuweka joking wakati watu wanatumbua pesa ambazo zinapaswa kujemga misingi kwa ajili ya watoto wetu, Wabongo ni watu wajinga sana, pesa zinapigwa na comment za watu unakuta ni asilimia 99 zemejaa utani tupu
Unataka tufanyeje mkuu, tuandamane?
 
Hapo nimekuelewa turudi sasa kwenye daraja la bilioni 7.2
 
Yaani kuweka daraja la temporary wanasifia hivyo.... Mbona ni kama wameli stretch tu na kukaza nuts...!!
 
Daraja/barabara hujengwa na wakazi wa eneo husika!?..huko kupigwa kwa watu wa rufiji kunakujaje kwenye miundombinu ya serikali!?..acha chuki za kijinga na watu wa rufiji!!..ulitaka wachange wanunue mabasi mazuri zaidi ya akida!?..watu wengine huwa mmebeba nini vichwani!?
 
Kwakua wanataka kusifiwa tuu basi acha tuwasifie, wameupiga Sana tumeona jinsi "masese" yetu yametumika vyema kabisa πŸ‘πŸ‘πŸ‘ bravooooooπŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ˜ŽπŸ˜Ž
 
Nyie endeleeni kuweka joking wakati watu wanatumbua pesa ambazo zinapaswa kujemga misingi kwa ajili ya watoto wetu, Wabongo ni watu wajinga sana, pesa zinapigwa na comment za watu unakuta ni asilimia 99 zemejaa utani tupu
Hongera kwa kulitambua hilo,watu wanaweka utani kwenye mambo ya muhimu yahusio mustakabali wa taifa hakika watanzani tupo gizani tena giza totoro,tuna safari ndefu sana ya kuja kutoka kwenye fikra za kutojitambua ,Mungu atusaidie hakika
 
Bilioni 7.2 kwa urefu wa mita 61 tena single lane bila kuwa na pedestrian. Ni wizi mkubwa hapo tayari, mleta mada umemuharibia mama badala ya kusifu.
Mbona hata Waziri Mkuu kawapongeza tanroad kwa ubunifu huo na kwamba mavyuma hayo yameokoa mabilioni ya pesa. Hivyo tutegemee kuona madaraja mengi yakijengwa gharama hiyo ya TSh 120 million kwa kila mita moja ya urefu (7.2 billion Γ· 61 meters)!!!

Kwa kweli haingii kichwani hayo mavyuma kuwa na gharama hiyo ya TSh 120 million kwa kila urefu wa mita moja. Yaani siku hizi hawa wahandisi wetu ndiyo wameamua kutupigwa kipumbafu namna hii? Wale wahandisi wa tanesco ndiyo kubwa lao, wamewaacha Maharage na January wananchi hawawaelewi. Masikini kale ka pharmacist ka Mkuranga kamefukuzwa kazi kwa kupiga buku nane tu na kako mikononi ya takukuru ambako hawatakaacha salama.
 
C
CCM haiupingi mwingi Bali mlipa Kodi anaupiga mwingi!!
 
Bilioni 7 zingeweza kujenga daraja la zege, la kudumu na chenchi kubaki kwa maendeleo mengine! Hilo ni daraja la muda ambalo life span yake haitazidi miaka 25 kabla kudai matengenezo!
Ok. Kwa hiyo liko chini ya kiwango fedha haiendani na thamani ya daraja au tatizo muda wa matumizi ni miaka 25? Hongera kwa kujadili hoja, baadhi wanatema tu sumu mithili ya joka dragonπŸ™πŸ™πŸ™
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…