Angalia daraja Mbuchi na Mbwera Kibiti la Bilioni 7.2 lililojengwa na Rais wetu Mpendwa Samia Suluhu. Tujipongeze

Angalia daraja Mbuchi na Mbwera Kibiti la Bilioni 7.2 lililojengwa na Rais wetu Mpendwa Samia Suluhu. Tujipongeze

IMG_0987.jpg

Waziri mkuu keshazindua daraja la bilioni 7 na hapo akifurahia jambo na viongozi wenzake
 
IMG_0986.jpg

Waziri mkuu hapo alizindua kibanda cha mlinzi huko tabora chenye gharama ya milioni 13 na hapo akiteta jambo na viongozi wenzake
 
Salaam wakuu,

Ni baraka na Neema iliyoje kumpata Rais mwenye Uchungu na Mali za Umma? Hakika Mungu anatufundisha na kutuonesha Umakini wa Rais wetu Samia Suluhu. Mungu anatuonesha Uwezo wa kufuatilia mambo wa Rais samia na wakati wa kupiga kura hatutaumiza kichwa kujua ubora wake kwani tumeona Uwezo wake wa juu wa kupambana na Ufisadi. Huu ndo uwezo wake wa juu wa utendaji ambao Mungu kamjalia.

Hii imepelekea Wakazi wa Kata za Mbuchi na Mbwera Kibiti Mkoani Pwani wamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa daraja la Mbuchi lenye urefu wa mita 61 linalounganisha kata hizo ambao umegharimu shilingi bilioni 7.2.

Hongera sana Rais Samia Suluhu Hassan. Hakika wewe ni kielelezo cha Wanawake.

Kazi iendelee.

Asitokee mtu akamkosoa rais kwa utendaji huu. Tumpigie makofi tu kama anavyotaka. Kama Watawala wanaafiki hi kitu inatusaidia kujua akili zao na madhumuni ya kugombania vyeo.

Hadi sasa sijajua Watanzania wana uhusiano gani na Mungu. Hadi tunapata Viongozi/Watawala wa hivi.

Tumewaseti watu wapongeze, then tunawapa elfu 50 kila mmoja. Angalia Video. Majaliwa mjanja sana
View attachment 2430635
View attachment 2430613View attachment 2430614
Sijaelewa shida iko wapi kwa hili daraja..

Pili Kuna watu wanachukia Rais akisifiwa na kuja na fix kibao ooh sijui wanasetiwa kwa 50,000 na blaa blaa za kijinga.
 
Mama yetu Sa100 tunakupenda ila
Punguza upole, tazama pesa za wadanganyika zinavyoliwa kizembe.
Maneno ya kutumbua au kufukuza kwann kwako hayatumiki so long haujamuonea mtu?!.
Soko la machinga pia Dodoma hali ni hiyohiyo upigaji mkubwa umefanyika.

Usipochukua hatua wananchi wanaona kama unabariki hali hiyo.
Pesa zimepigwa wapi hapo?
 
Ni jambo la muda tu kabla yule mkaguzi mkuu wa mahesabu ya serekali au mtu mmoja kule bungeni atumie nafasi yake kuhoji kipi kilichofikisha daraja hilo kuwa hizo billions
Una uhakika? Unajua maana ya 62m? Kwanza kwa navyowajua TanRoads hiyo Pesa bado Ni ndogo kukamilisha huo mradi.
 
Acha Uchawa we!?
Lini ulimkuta hapo akishika Nondo!?
Hizi ni Fedha zilizotolewa Kwa ajili ya WaTanzania na pia ziko za ndani.
Hakuzitoa Kwenye familia wala mfuko wake. Acheni misifa hadi inakera!
Mambo mengine ni wajibu wa Serikali iliyoko ofisini Wala sio mtu Fulani!! Jifunze.
Jinyonge tuu mzee Wala usipate shida 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20221129-085223.png
    Screenshot_20221129-085223.png
    179 KB · Views: 2
Huyo mkandarasi yupo saiti ipi??njia ya mloka ni njia kubwa sana ila hakuna rami.

Mbunge yuko bize kuanzisha matamasha ya burudani sijui ndio hitaji kuu la wana rufiji.

Itoshe kusema rufiji imebarikiwa sana kwa aridhi nzuri na mto mkubwa inaotiririsha maji mwaka mzima.

#MaendeleoHayanaChama
Bila miundombinu hizo Baraka zako za ardhi zitakusaidia Nini?

Ndio madaraja yameanza kuwekwa hivyo
 
Ahsante mkuu!
Jf hii, ukiisikia habari ipokee kwa umakini kweli.......watu humu wanazusha balaa, na watu humu wanakurupuka kupokea vilivyorushwa bila kutafakari balaa. Wakiona kichwa cha habari tu wameshakimbilia kucomment lawama, kama kawaida yao.

Siajabu hata hiyo taarifa mtu hata hana, ameona daraja na kusikia bil 7 point kadhaa zikitajwa basi ameunganisha taarifa yeye mwenyewe na kuja kuwapatia haters wa mama wapate sehemu ya kujifajia.
Wengi wao wapumbavu na wanaohemka achana nao.

Hayana hata BoQ kujua Nini kimefanyika Ila yanapayuka tuu.
 
Wananchi wanalalama juu ta tozo, mgao wa umeme, maisha magumu na mzunguko wa.pesa uliodorola. Lakini mkuu wa kaya upo kimya. Hii ni wazi.kuwa hauna machungu na unaowatawala.

Mfano tulitegemea itolwewe hotuba kali kuonyesha unasikitika juu ya wananchi kukwama shughuli zao kutokana na mgao wa umeme huku waziri Makamba akidai kuna ziada ya Mw 1400.

Ukipigania mzunguko wa pesa uongezeke kwenye jamii maana ajira kubwa ni sekta binafsi na hao ndio wanategemea mzunguko wa kupata mlo.

Harufu ya ufisadi inazidi kutamalaki na mkuu upo kimya na haukemei hadharani. Hauna uchungu na wananchi walipa kodi.
👇🏿View attachment 2431256
Hotuba Kali ndio italeta mvua ? 😜😜
 
Back
Top Bottom