Hapa kuna jamaa alitafuta ticketi akakosa.kuwa ZIMEJAA. NO SEAT AVAILABLE.
Akatumia kujuana, akapata. Kuja akauta mabehewa matupu!
Sidhani kuwa system ya serikali haramu haijui. Kuna mkono wa HARAMIA MKUU anayehusika na haya!
Ningelikuwa mimi, ningelileta management from top bottom kutoka Ulaya waendeshe "wadigo" wandengeleko" mwende mkalime mihogo
Soma hii maana nilitaka identify ya mtu isiwepo. Ngoja niiweke
Ameandika Askofu Bagonza
NIMEWASIKIA TRC KUHUSU SGR
1. Napenda kuushukuru uongozi wa shirika la Reli kwa kutoa ufafanuzi juu ya “swali” langu la 7/10/2026 ikiwa SGR inahujumiwa au shida ya mtandao? Mmefafanua kwa uungwana nami nawapongeza.
2. Baada ya kukosa ndege, niliingia mtandaoni kutafuta tiketi. Seat zote za tarehe 7/10 na 8/10 kwa madaraja yote zilikuwa zimejaa. Ndipo nililazimika kutafuta msaada wa “kujuana” nikapata tiketi.
3. Kama seats zilikuwa zimeuzwa na abiria hawakutokea, basi shirika linatengeneza faida kwa kutosafirisha watu! Nina picha zaidi ya nilizoonyesha, kwamba seats nyingi hazikuwa na watu mpaka Dodoma.
4. Nilihojiana na wafanyakazi wawili (msiwatafute kwenye CCTV CAMERA) na walikuwa na ujasiri kuniambia kwamba, “seats zote za madaraja ya chini zinafungwa mtandaoni ili abiria waende na mabasi”. Tuhuma hii isipuuzwe.
5. Ni kweli nilisafiri na treni ya mwendokasi isiyo na daraja la Economy, lakini business class ndiyo economy kwa Royal class. Nilizunguka mabehewa yote na kukuta wafanya usafi wanatunza vifaa vyao vyooni na kusababisha kero kwa watumiaji.
Napenda kwa moyo wote kuishauri TRC kuchukulia kwa uzito maoni na ukosoaji wowote bila kinyongo ili kuliepusha shirika na kuporomoka mapema. Mimi sikuhukumu, niliuliza swali.
www.facebook.com