Angalia video Hii kisha utoe hukumu kwa haki.
Hii serikali legevu kama.ya kikwete kipindi cha magufuli huu ujinga ulikoma. Haya mambo yalishamiri awamu ya 4 sasa yanarudi tena
Hujakosea kabisa mkuu. Magufuli ni mkulima na mfugaji pia anajua athari ya jambo hili.

Sasa Samia au kikwete Tofauti na njiwa za kutunza majini ana mfugo Gani?
 
Nasikia hata ukimwagia kinywaji cha Pepsi kwenye mazao Yako wakila imekula kwao. Ila hakikisha unahama mji muda huohuo vinginevyo tutakuita rip.
Hii ya Pepsi sijui... Ulichosema ni sahihi mfugaji anathamini sana mifugo yake kuliko uhai wa mtu ukiwa mifugo yake lazima nawewe uifuate tu hukohuko
 
Ng'ombe anapokula majani hayatafuni kwa sababu hana kichwa chake hakina mfumo wa kutafuna, hivyo majani huenda kwenye tumbo la kuyasindika yalainike kisha kuyacheua yaliyolainika na kuyameze tena sasa kama chakula. Ng'ombe akila majani yaliyopakwa asali huvimbiwa kutokana na mfumo wa joto na kemikali za tumbo la kuchakata majani kushindwa kufanya kazi kunakosababishwa na asali hivyo tumbo kujaa hewa na kusababisha kifo.
 
Safi saana
 
Binafisi mimi nimetokea kwenye familia ya wafugaji wa mifugo karibia yote yaani mbuzi,kondoo na hata ng'ombe .

kipindi tukiwa tunachunga ilikuwa ni fahari sana kulisha mazao ya wakulima tena ikitokea mkalisha na msionwe au kukutwa mtajipongeza kweli.

Ukweli usiosemwa ukisikia vita ya wakulima na wafugaji jua tu mchokozi ni mfugaji kwa 97%.

Hii video ukiangalia vizuri ni zaidi ya ng'ombe ya 40 wanachungia kwenye mahindi ya mkulima imagine umelima kwa gharama kubwa then unafika shamba unakuta yameliwa yote na mifugo.

Bahati mbaya sana ukienda kudai haki yako utapewa kiasi kidogo tu maana wafugaji huwa wako karibu sana na ma bwana shamba na viongozi wengine kwa kuwapa maziwa na kuwalimia bure mashamba yao.

Hivyo viongozi wanakuwa hawana meno kabisa kuhukumu kwa haki.

Matokeo yake ndo haya mkulima ananunua asali hata lita3 tu anapaka paka kwenye mazao yake ili ng'ombe akila habari ya uzima inaishia hapo!

Wengine hupulizia sumu pia.

Je wewe utahukumuje hii kesi?
View attachment 3442383
Safi sana
 
Back
Top Bottom