Uchaguzi 2020 Angalizo: Kumdhibiti Godbless kunahitaji " timing" vinginevyo watatumbuliwa watendaji wote wa Arusha!

Uchaguzi 2020 Angalizo: Kumdhibiti Godbless kunahitaji " timing" vinginevyo watatumbuliwa watendaji wote wa Arusha!

Jaffo kwa sasa anaulazimisha uwaziri mkuu kwa kila aina ya vibweka
Kiukweli Arusha hawashtuki kabisa na hayo mambo. Lema angewaita wangemwagika kama siafu na nyuki. Kuita wananchi ni kazi ya Mkurugenzi wa hilo jiji anashirikisha wataalam wake wa kata ambao hufikia wananchi huko kijijini na mitaa. Aisee udhalilishaji huu.
 
Lema ni hajafanya chochote arusha, wanaomshabikia ni wahuni tu, hamna cha maana alichofanya arusha zaidi ya kujiimarisha mwenyewe kiuchumi, kazi kutwa kushinda kwenye mitandao na maneno maneno tu mitandaoni na kushinda mahakamani
Naona umeamua kututukana sisi wana wa Arusha, maana mkoa mzima wa Arusha unampenda na kumkubali mh Lema
 
Si kwamba Lema ni mwanasiasa mzuri sana au utendaji wake ni wa viwango, kiukweli huyu jamaa ametokea tu kukubalika.

Inahitajika saikolojia ya viwango kuweza " kumfifisha" huyu jamaa mbele ya machalii wa A - town na siyo hii ya kuadhibu wataalamu barabarani kana kwamba nao ni wanasiasa.

Watu kuja kushuhudia ufunguzi wa miradi inabidi wahamasishwe na wanasiasa wa CCM siyo watendaji au wataalamu.

Ni angalizo tu.

Maendeleo hayana vyama!
Ndugu John, ninakubaliana nawe 100%++++, kweli ike dhulma aliyoifanya waziri Jafo kwa yule kiongozi wa Tarura haisameheki, inabidi Raisi aliangalie jambo hili kwa jicho la tatu.

Road engineer anauhusikaje na ushawishi wa wananchi.

Pili kosa kubwa lilifanyika Arusha ni kumuondoa Gambo, ambaye aliweza kumudu Lema vizuri sana. Alipotumbuliwa Lema aligawa pombe nyingi sana, alifunga Bar watu wanywe bure.
 
Jimbo laArusha lina barabara za lami za kutosha toka awamu iliyopita. Na sio barabara tu, miundombinu mbinu mingine karibia yote iko sawa. Kwa taarifa yako Arusha imeshatoka kwenye siasa za kichovu za kushangilia barabara. Wasukuma ndio wana muda wa kushangilia barabara, maana ni vitu vigeni kwao.
[emoji23][emoji23][emoji23]

JESUS IS LORD[emoji120]
 
Je niulize kuna mkutano aliofanya Lema bila kufatiliwa na Mapolisi??
Alipozindua ujenzi wa Hspl kwa fedha za wafadhili si mliona alivyo andamwa na Gambo mwisho wakajidai ni mradi wao.
Wana Arusha wanajua Lema anagharamia masomo zaidi ya watoto 400 wasiojiweza.
Lema alibanwa kila kona, uzuri wake wana Arusha sio mazezeta wanajua wanataka nini!!
Maendeleo bila uhuru huo ni utumwa!!
Duh,masikini ndo maana Mungu anampigania na kumtetea!
Wote wanaopambana nae naona wao ndo wanaondoka wanamuacha!
Hawajaligundua hili!

JESUS IS LORD[emoji120]
 
Ndugu John, ninakubaliana nawe 100%++++, kweli ike dhulma aliyoifanya waziri Jafo kwa yule kiongozi wa Tarura haisameheki, inabidi Raisi aliangalie jambo hili kwa jicho la tatu.

Road engineer anauhusikaje na ushawishi wa wananchi.

Pili kosa kubwa lilifanyika Arusha ni kumuondoa Gambo, ambaye aliweza kumudu Lema vizuri sana. Alipotumbuliwa Lema aligawa pombe nyingi sana, alifunga Bar watu wanywe bure.
Mmh,yaani Lema agawe pombe kwa kutumbuliwa gambo?!!!
Walioko Arusha wanajua ukweli,usitudanganye!
We fuatilia wote wanaopambana na Lema Leo hii wako wapi? Eti gambo alimumudu Lema?!! OK,yuko wapi ss na wenzake?
Kwa wenye uelewa wameshaelewa!

JESUS IS LORD[emoji120]
 
Lema ni hajafanya chochote arusha, wanaomshabikia ni wahuni tu, hamna cha maana alichofanya arusha zaidi ya kujiimarisha mwenyewe kiuchumi, kazi kutwa kushinda kwenye mitandao na maneno maneno tu mitandaoni na kushinda mahakamani
Nyie vijamaa vijinga sana.Sasa huo mradi uliokosa wahudhuriaji wa kijani umefanyika wapi? Na katika kipindi nani akiwa Mbunge? Au ili isemwe kafanya kitu ni mpaka atoe fedha mfukoni kwake kujenga barabara au hospitali. Amka bwana!!!😃😃.
Chochote kinachofanyika kwa ajili ya umma katika kipindi cha mbunge husika na credit anapewa huyo Mbunge
 
Nyie vijamaa vijinga sana.Sasa huo mradi uliokosa wahudhuriaji wa kijani umefanyika wapi? Na katika kipindi nani akiwa Mbunge? Au ili isemwe kafanya kitu ni mpaka atoe fedha mfukoni kwake kujenga barabara au hospitali. Amka bwana!!![emoji2][emoji2].
Chochote kinachofanyika kwa ajili ya umma katika kipindi cha mbunge husika na credit anapewa huyo Mbunge
huyo harudi tena ndio mwisho wake arusha..wana arusha wameteseka sana wanaofurahia ni wahuni ambao hawana kazi mjini
 
Naona umeamua kututukana sisi wana wa Arusha, maana mkoa mzima wa Arusha unampenda na kumkubali mh Lema
acha kujitoa ufahamu ..wana arusha wameteseka vya kutosha, kwa miaka kumi, chini ya mbunge ambaye hawez hata kuisemea arusha na maendeleo, unashinda kutwa twitter na mahakamani kila siku kesi, mara anamdhihaki rais, mara kafanya hiki, mara kile, yani upuuzi tu, arusha kama tungekua na muwakilishi mzuri angeiwakilisha vizuri arusha pamoja na kwamba utalii unaibeba arusha , arusha ilitakiwa iwe mbali sana kimaendeleo, ma hayo maendeleo hayawez kuletwa kamwe na chadema, wala mbunge anayetokea chadema.
 
Lema ni hajafanya chochote arusha, wanaomshabikia ni wahuni tu, hamna cha maana alichofanya arusha zaidi ya kujiimarisha mwenyewe kiuchumi, kazi kutwa kushinda kwenye mitandao na maneno maneno tu mitandaoni na kushinda mahakamani

Aliyempeleka mahakanani (kumshitaki) Lema ni nani?

Ukimjuwa,

Mlaumu Huyo kwa Lema kushindwa kufikia malengo ya kuitumikia Arusha.
 
Wewe ndiyo unajitoa akili kwa makusudi, unaongelea mh Lema kutumia muda mwingi mahakamani? Huko mahakamani anajipeleka mwenyewe?

Kuitwa kichaa siyo lazima utembee uchi, naona wewe tayari ushakuwa kichaa tayari.

Sisi wana wa Arusha tupo na mh Lema hata mfanyeje hamuwezi kutubadilisha mawazo na mapenzi yetu kwa mh Lema.

Back
Top Bottom