South Noma niliwahi kufata mkumbo mwaka 1990 nikashawishika kwenda South dah nilipofika nilijilaumu sana baada ya kuona maisha halisi waliokuwa wanaishi watz.... Baada ya kufika moja kwa moja tulienda kujitambuliza kwa home wetu kuwa tayar tumeingia basi home boy akatupeleka anakokaa kwenye mgorofa mmoja humo kuna wabongo kama wote.... Yaani sitokuja sahau aisee... Hilo gorofa kila muda ni milio ya risasi namuuliza mwanangu vip ananiambia kuna mtu kazingua kabigwa risasi mara wabongo wale wa kule wamevamia hapa wamepiga watu risasi kisa demu aisee maiti kila muda duh mbaya zaidi rafiki yangu alienitoa bongo kunileta kwa mkaburu asubuhi a naona watu wamejazana chini nauliza naambiwa mwanao kapigwa kisu na wazuru kafa yupo hapo chini polisi(kitenga) bado hawajafika... Nilishangaa sana yaani matukio ya mauwaji ni kitu cha kawaida maeneo hayo... nikaona hapa sio sio sehemu ya kuishi.... Nafanyaje na hela sina akili ikanijia nikajilipue polisi mimi mtanzania naishi South bila documents yoyote labda naeza kurudishwa home kirahis.....thubutu sijaamini nilichikutana nacho baada ya kujitambulisha mimi mtanzania sijui naishi bila kibali.... Picha linaanza nilifukuzwa hapo kituo cha polisi [emoji1787][emoji1787][emoji1787]... Huko sio kwa kwenda kama una Channel yoyote ya maana utaenda juta