DOKEZO Angalizo: Utapeli na wizi kwenye maduka ya Pharmacy/ biashara ya dawa za binadamu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mfano wako hauna Uhalisia....kutoka2500 hadi 30000?
 
Kabisa Sasa hivi Kuna upandaji holela wa Dawa
Mfano Kuna Dawa moja Wanaita Erythromycin Nilikuwa nikinunua 10 kwa Tsh 1000
Ajabu Ndani ya muda mfupi Imekuwa 2000
Sasa Inapandaje Ghafla kwa ×2
Sijui nchi hii tunakwemda wapi
Ndugu.....

Jitahidi sana kama una uhitaji wa dawa kwa muda ( Mungu aepushie mbali) utembelee maduka makubwa makubwa tofauti na haya ya mtaani......kidogo Yana unafuu....
 
Ndugu
Tumeshaangamia kwani wapo wengi wanaojifia kwa kukatishwa tamaa na bei za kubumba Hali ya kuwa ni bei za kitapeli
Mimi kaka yangu alikufa 2001 kwa kukosekana buku 5 ya sindano ya pumu. Zahanati ya mtaani kabisa ambapo tunajulikana ila mtu na roho yake mbaya alishindwa kufanya tendo la kibinadamu na kupelekea mapafu kubana hatimaye kukata moto. Ni story ambayo haiwez futika akilini mwangu.
 
Ni kawaida hiyo mkuu mbona. Wale ni machinga hivyo bei watakupga mara kadhaa. Hii ni kwa biashara zote si duka la dawa tu.
Hata bia kuna sehemu inauzwa buku 2 sehemu nyingine utanunua buku 7
 
Ni kweli kabisa, inashangaza sana sikuhizi Wauza madawa mpaka wanajitangaza sana kupitia WhatsApp, Tiktok, Instagram na kwingineko kama wauza nguo na bidhaa zingine
 
Pole sana ndugu yangu......

Kaka yako ni miongoni mwa wahanga wanaoangukia kwenye mikono ya hawa mashetani walioweka fedha mbele na kuwacha ubinadamu nyuma.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…