Angalizo wababa: Mtoto wa kambo si wako, usitarajie haki zisizokuwa zako

Angalizo wababa: Mtoto wa kambo si wako, usitarajie haki zisizokuwa zako

Ukiwa na uhusiano na mwanamke mwenye mtoto, hasa wa kiume, siku zote yule mtoto anakuona kama mvamizi kwenye maisha yake na mama yake. Na akikua kidogo akajua unamnyandua mama yake, ujue atakuchukia kishenzi, wivu kabisa ule wivu wa kiume.

Atakuvumilia tu kwa kuwa unampa mama yake pesa, lakini hakupendi. Chochote utakachompa anakihesabu kama hongo kwa kuwa unamkula mama yake, usitegemee shukurani yoyote kwa sababu umeshaipata kwa mama yake na ujue hapendi unavyomkula.

Usitarajie kuwa ukija kumuoa huyo mama eti na huyo mtoto atakupenda, hilo nakuhakikishia halitatokea hata umfanyie nini. Na atakapopata mawasiliano na baba mzazi, basi hao watatu (mtoto, mama yake na baba yake) watakugeuza chumo, bwege mtozeni. Utalea mtoto wa mwenzio, akifikia kujimudu mwenyewe ataondoka kwako kama vile hakujui!

Ataanzisha makazi yake mapya na kuendeleza ule wimbo wa "nani kama mama", wewe utatelekezwa. Hata yule baba yake uliyekuwa unadanganywa kuwa hamjali mtoto utakuja kushangaa kujua kuwa kumbe alikuwa anamjali! Watakuwa wanakutana na mkeo kwenye shughuli za huyo mtoto wao! Ataitwa kuja kutoa jina la mjukuu, wewe utawekwa kando. Unahitaji kuwa na ngozi ngumu sana kuvumilia mambo kama haya uzeeni.
Point
 
Wewe bado hujaelewa somo.

Single mother hawana shida, shida ni wanaume mbumbumbu wanaotegemea Embe kwenye Mnazi.

Mtoto wa single mother sio wako na hatakuja kuwa wako Kivyovyote vile hata uwekeze vipi.
Jambo hili utaanza kuliona ukishaanza kuishiwa nguvu Kwa uzee.
Hakika
 
Ila humu JF watu huwa wanaji hype sana yani ukiwa ni mgeni humu ukasoma comments za wachangiaji unaweza kuzimia kwa pressure.

Kiuhalisia wengi hapa mnao support mada wala sio maisha yenu na wengi mtaoa tu singo bibiz au masingo bibiz wenu kuolewa na wanaume wengine.

Acheni kujimwambafai wakati mnafwafwanzika uswahilini.
 
Wengi wanaongea hawana experience na hiyo kitu.... kiukweli mwanzoni mtoto wa kiume lazima amchukie baba wa kambo ila...

Jambo unalotakiwa kufanya step-father ni ku earn imani na upendo wa dogo wa kiume, sisemi kama itakuwa kazi rahisi ila watoto wakufikia upendo wao una earn sio utapewa kirahis rahis tu
 
Dada yangu ni single mother aliolewa lakini mtoto alichukuliwa na akalelewa.na wajomba zake. Pale nyumbani anakuja kusalimia tu. Na ndoa yake imetatibiwa na wajomba mwanzo mwisho.
Mtoto wa kiume ni janga kwa wazazi walezi

Mtoto mpumbavu huvunja ndoa ya wazazi wake na mtoto muelevu huwaweka wazazi karibu zaidi
 
Diamond mwenyewe si ana baba wa kambo
Diamond ni ushahidi tosha wa madhila yanayowafika baba wa kambo. Mara tu alipofanikiwa, Diamond akajifungamanisha na mama yake, baba akatengwa, Diamond na mama yake wakaungana na watoto wa upande wa baba mzazi, ikawa hivyo.

Nimeona wengine wengi wa namna hiyo. Mtoto akishaanza kufanikiwa utaona anaanza safari za vikao vya huko anakoita kwa "ndugu zake", upande wa baba yake ambao miaka yote mama yake alikuaminisha eti hawakuwahi kuwa na "time" na huyo mtoto! Utashangaa kugundua anawafahamu wote kwa majina na mahali walipo, na kumbe tangu zamani zote aliwasiliana nao, na kumbe eti baba yake alikuwa anamsaidia hata wakati ule ulipodanganywa kuwa alimtelekeza.
 
Ukiwa na uhusiano na mwanamke mwenye mtoto, hasa wa kiume, siku zote yule mtoto anakuona kama mvamizi kwenye maisha yake na mama yake. Na akikua kidogo akajua unamnyandua mama yake, ujue atakuchukia kishenzi, wivu kabisa ule
Vijana wa siku hizi kweli hawana heshima kabisa,eti mwanamke mwenye mtoto ukimuoa unaambiwa umeoa MOJA BILA.
 
Back
Top Bottom