Angalizo wababa: Mtoto wa kambo si wako, usitarajie haki zisizokuwa zako

Point
 
Hakika
 
Ila humu JF watu huwa wanaji hype sana yani ukiwa ni mgeni humu ukasoma comments za wachangiaji unaweza kuzimia kwa pressure.

Kiuhalisia wengi hapa mnao support mada wala sio maisha yenu na wengi mtaoa tu singo bibiz au masingo bibiz wenu kuolewa na wanaume wengine.

Acheni kujimwambafai wakati mnafwafwanzika uswahilini.
 
Wengi wanaongea hawana experience na hiyo kitu.... kiukweli mwanzoni mtoto wa kiume lazima amchukie baba wa kambo ila...

Jambo unalotakiwa kufanya step-father ni ku earn imani na upendo wa dogo wa kiume, sisemi kama itakuwa kazi rahisi ila watoto wakufikia upendo wao una earn sio utapewa kirahis rahis tu
 
Dada yangu ni single mother aliolewa lakini mtoto alichukuliwa na akalelewa.na wajomba zake. Pale nyumbani anakuja kusalimia tu. Na ndoa yake imetatibiwa na wajomba mwanzo mwisho.
Mtoto wa kiume ni janga kwa wazazi walezi

Mtoto mpumbavu huvunja ndoa ya wazazi wake na mtoto muelevu huwaweka wazazi karibu zaidi
 
Diamond mwenyewe si ana baba wa kambo
Diamond ni ushahidi tosha wa madhila yanayowafika baba wa kambo. Mara tu alipofanikiwa, Diamond akajifungamanisha na mama yake, baba akatengwa, Diamond na mama yake wakaungana na watoto wa upande wa baba mzazi, ikawa hivyo.

Nimeona wengine wengi wa namna hiyo. Mtoto akishaanza kufanikiwa utaona anaanza safari za vikao vya huko anakoita kwa "ndugu zake", upande wa baba yake ambao miaka yote mama yake alikuaminisha eti hawakuwahi kuwa na "time" na huyo mtoto! Utashangaa kugundua anawafahamu wote kwa majina na mahali walipo, na kumbe tangu zamani zote aliwasiliana nao, na kumbe eti baba yake alikuwa anamsaidia hata wakati ule ulipodanganywa kuwa alimtelekeza.
 
Ukiwa na uhusiano na mwanamke mwenye mtoto, hasa wa kiume, siku zote yule mtoto anakuona kama mvamizi kwenye maisha yake na mama yake. Na akikua kidogo akajua unamnyandua mama yake, ujue atakuchukia kishenzi, wivu kabisa ule
Vijana wa siku hizi kweli hawana heshima kabisa,eti mwanamke mwenye mtoto ukimuoa unaambiwa umeoa MOJA BILA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…