Angalizo: Watu wa Mbeya mnaoishi Mbeya Mjitathimini mienendo yenu kinidhamu inalichafua Jiji, ipo siku jiji litafutwa

Hakika. Kwa asilimia kubwa wasanii wamechangia sana mmomonyoko wa maadili.

Nachukia nikisikia msanii kujiita kioo cha jamii wakati anaharibu jamii
Hayo matamasha ni ushnz mtupuuu tuu

Ova
 
Mbeya misingi yake ni hip hop kwenye burudani pia wagumu ni wengi na wastaarabu sana ila ukizingua sasa huo mtiti wake!
 
Sasa kwani likifutwa Jiji wao watapata shida Gani na Sasa linasemekana ni jiji kunafaida Gani waipatayo.
Zuchu tulia umeyataka mwenyewe
 
Poleni Mbeya sio mkoa wa kabila Moja,kuna makabila mbalimbali na wahamiaji Toka mikoa mingine.Ukienda Sehemu Moja inaitwa undalini na huko Sehemu za Mwakaleli,huwezi kusikia mwizi au wezi hata wa pini au sindano.Ni Bangi zinawashanganya hao walioko Mbeya mjini na ushamba wa kizamani kwamba u babe ndio maisha!
 
Jiji halifutwi kirahisi hivyo, punguza siasa nyepesi.

Badala ya kulaumu, shida imeanzia wapi? Mzizi wa tatizo ni nini?
Jiji limejaa watu wenye tabia za kihalmashauri ya wilaya Bora hata lifutwe tu, inakuwaje watu wa jiji wanaiba mpaka betr za sola za barabarani
 
unaposema sema watu mbeya am sure unakuwa umejumuisha kila mwana mbeya kwamba ndiyo tabia zao,???
Sisi wageni tunapopita Mbeya mjn na kuona taa usiku haiwaki kisa mtu kaiba betri ya solar tunasema watu wa Mbeya wanaiba hata betr za taa za barabarani
 
Jiji limejaa watu wenye tabia za kihalmashauri ya wilaya Bora hata lifutwe tu, inakuwaje watu wa jiji wanaiba mpaka betr za sola za barabarani
Basi halifutwi kwa hisia zako, wala halitofutwa kwa tabia za watu. Maana jiji lote haliko hivyo

So kaka ume fail, mbeya itabaki kuwa jiji, hapa ni kuangalia chuki imeanzia wapi? Je siasa zilihusika? Au kuna jambo lingine?
 
Tamasha lilikuwa linaendelea vizuri sana huku watu wakiendelea kupata burudani. Aliyekuja kuharibu hilo tamasha lao ni hako katoto tutakoless mnakokaita Zuchu.

Amepanda jukwaani anaanza kuwaambia watu mitano tena kwa mama, hapo watu waka mind, akaanza kuimba hamalizii wimbo anawawekea mike waimbe, hapo kelele zikaanza, wengine wakakumbushia kuwa mnatuona wajinga au? Tumetoa hela zetu mnakuja kutwambia mitano tena, nadala ya kuimba utuburudishe unatuwekea mike tuimbe, zikaanza kurushwa chupa za maji, mara viti.
Zuchu akaanza kujibishana na mashabiki, akawaonyeshea kidole cha kati, hapo watu mashetani yakawapanda, wakamwambia mnatuletea mambo mliyofanyiwa na PDiddy sisi? Watu wakapanda Jukwaani na kulivunja tamasha lisiendekee ikabidi mabaunsa wamkimbize Zuchu.
 
Bora wangempopoa mawe ya kutosha ww uwaoneshe dole la kati watu wakuache tu ...hako katoto hakana adabu kama kamekulia kwenye kilabu ya chibuku..Harafu sasa unakakuta mm mtoto wa kiislam siwezi tangaza pombe ila kuweka dole kati ni sawa ...
 
Jiji la Mbeya sidhani Kama watu wake wanajua kuwa wapo jiji wapo very primitive
Wanajielewa,msanii anaandaa event unalipia,unaenda kwenye tamasha usikilize na kuenjoy mziki halafu analeta kampeni za siasa, lazima upopolewe mawe!
Big up Mbeya ila hapo kwenye solar za barabarani wanakosea.
 
Sema ulitaka uongelee swala la zuchu tu
 
Hao wasanii wenu mnao waanzishia uzi hivi wamewapa nini cha maana?
ukusikiliza nyimbo zao matusi tu hakuna cha maana. vaa yao ovyo ovyo huwezi angalia hata kama una watoto wakiume wenzako huwezi.

Msanii wenu kawaonyesha mashabiki zake dole la kati clip na picha zimetumwa mitandaoni akionyesha dole la kati
lakini bado mnawaona watu wa mbeya ni washamba sasa kama ujanja ndo huo msanii kuwaonyesha dole la kati basi bakini na wasanii wnu.

Watu wa Dar mna matatizo sana vichwani mwenu, badala mfatilie kwann zuchu alifurushwa jukwaani yeye pekee yake na wasanii wengine hawakufanyiwa hivo yeye alikosea nini?

Badala yake mnakuja na lawama kwa watu wa mbeya.Ndo kafurushwa sasa hamna mtakacho fanya
 
Mnapochabikiaga Machadema mlidhani Huwa wanapandikiza nini?

Uhuni umehama kutoka Arusha na Sasa ni Mbeya.

Chadema ni watu wa hovyo,unganeni kuwakataa ndio chanzo Cha yote hayo.

Saizi Arusha imetulia Kwa sababu wameyakataa Machadema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…