Anna Tibaijuka: Dubai ni Mshindani Wetu kwenye kuendeleza Transhipment potential, tukimkabidhi Bandari zote ni sawa na Kujinyonga!

Anna Tibaijuka: Dubai ni Mshindani Wetu kwenye kuendeleza Transhipment potential, tukimkabidhi Bandari zote ni sawa na Kujinyonga!

Yaan point yako ninini. Kwamba sio kweli alichosema au kwasababu na yeye ni wale wale. Maana hapa ishu ni mkataba wa bandari.

Sasa naona umeanza kuelewa mkuu...

Alichokiongea hakina uhalisia wowote, kaongea kwa sababu kajisikia tu kutoa maoni lakini hata yeye angekuwa ni waziri mwenye dhamana au kwenye nafasi ya kuamua kama wenzake walivyoamua, uamuzi wake usingekuwa tofauti na kina Mbarawa...

Kwa sasa huo mkataba hauwezi badilishwa, rekebishwa au fanyiwa mageuzi ya aina yeyote...

Kwa sasa atulie tu aendeleze miradi yake ya mashamba ya miti ambayo usikute chanzo chake ni mihela ile ya kwenye sandarusi...
 
Sasa naona umeanza kuelewa mkuu...

Alichokiongea hakina uhalisia wowote, kaongea kwa sababu kajisikia tu kutoa maoni lakini hata yeye angekuwa ni waziri mwenye dhamana au kwenye nafasi ya kuamua kama wenzake walivyoamua, uamuzi wake usingekuwa tofauti na kina Mbarawa...

Kwa sasa atulie tu aendeleze miradi yake ya mashamba ya miti ambayo usikute chanzo chake ni mihela ile ya kwenye sandarusi...
Hakina uhalisia kivip? Hata kama angetekeleza Lakin hapa kasaidia kuchokonoa mjadala so usiishi kwa kujadili mtoa hoja jadili hoja yake. Je ni kweli asemayo? Je nini kifanyike. Africa tunafeli sana coz tunaishi kwa kukariri makosa ya watu tunasahau kila mtu ana kitu cha kumfaa mwingine. Mi nilifikiri umefanya utafiti ukaja na hoja pinzan kumbe hoja yako ni Tibaijuka. Suala la kuwa hata yeye angekuwepo angefanya hivyo hilo halina mantiki coz hata wewe ungekuwepo ungefanya hivyo pia. Lile ni suala la uwajibikaji wa pamoja huwez kupinga ukiwa ndani. Lakini mpaka mkataba unavujishwa inamaanisha hata walioko ndani hawakubaliani nao. Na huu ni mkataba mmoja Kati ya 17 aliyosaini Mama pale Dubai.
 
Kwa hiyo huko jikoni bado mmekubaliana kuwapa DPW??
Uamuzi wa kuwapa DPW, uliishafikiwa kitambo sana toka 2022 wakati hiyo IGA ilipo sainiwa, ile process ya kuridhiwa na Bunge ni just a due process, kinachopikwa sasa ndio mkataba wenyewe wa HGA, this is the real thing!.
P
 
Kutetea huu mkataba kazi sana, bora mnyamaze kimya tu.

Hayo maendeleo utayapataje wakati umeshawapa waarabu operation zote wafanye wao milele? kwani wao wajinga wasipeleke profit kwao wawape nyie?!
Kiukweli elimu ya mikataba inahitajika sana kwa Watanzania!, mkataba wa HGA na Mwarabu wa Dubai kutuendeshea Bandari zetu bado!, uko jikoni unapikwa!. Mwarabu wa Dubai hapewi operation zote, anapewa container terminal only na sio milele, ni within a specified period of time utaiona kwenye HGA
P
 
Prof Anna Tibaijuka anasema Dubai ni Mshindani Wetu kwenye kuendeleza Transhipment potential so tukimkabidhi Bandari zote ni sawa na Kujinyonga

Tibaijuka anasema kupitia Ukurasa wake wa twitter kwamba bado ana Imani Mkataba Huo wa DP World utarekebishwa kwa kutumia Wataalamu Wetu wa Uchumi

Mlale unono!

Kwa hiyo anataka tuendelee kumkabidhi muhaya mwenzake Nazir Karamagi wa tics?
 
Kiukweli elimu ya mikataba inahitajika sana kwa Watanzania!, mkataba wa HGA na Mwarabu wa Dubai kutuendeshea Bandari zetu bado!, uko jikoni unapikwa!. Mwarabu wa Dubai hapewi operation zote, anapewa container terminal only na sio milele, ni within a specified period of time utaiona kwenye HGA
P
Nonsense.

Mwarabu yuko field tangu October 2022.

Hapewi container terminal only, yale makubaliano ya mwanzo ambapo yanamfanya awe field sasa yanampa mamlaka ya kusimamia bandari zetu Tanganyika zote, za bahari na maziwa.
 
Nonsense.
Punguza hasira na kutukana watu bure
Mwarabu yuko field tangu October 2022.
Anachofanya ni kitu kinachoitwa mobilization, ni matayarisho tuu!.
Hapewi container terminal only, yale makubaliano ya mwanzo ambapo yanamfanya awe field sasa yanampa mamlaka ya kusimamia bandari zetu Tanganyika zote, za bahari na maziwa.
Nakushauri tusubirie mkataba wa HGA ndio utaona anapewa nini na muda gani.
P
 
DPW hatakabidhiwa Bandari zote, wala Bandari yoyote, watakabidhiwa tuu zile Beth za makontena zilizokuwa chini ya Ticks kwenye Bandari moja tuu ya Dar es Salaam, hivyo tutakuwa free kuendeleza Bandari yetu ya Bagamoyo na Mchina.
P
Hii scope ya ushirikiano umeitoa kwenye kifungu kipi cha mkataba tuliosoma? Unaniangusha baba paroko.
 
DPW hatakabidhiwa Bandari zote, wala Bandari yoyote, watakabidhiwa tuu zile Beth za makontena zilizokuwa chini ya Ticks kwenye Bandari moja tuu ya Dar es Salaam, hivyo tutakuwa free kuendeleza Bandari yetu ya Bagamoyo na Mchina.
P
Kwenye mkataba ipo aya ya ngapi? wekeni uzalendo mbele
 
Huyu Profesa...Milioni 10 pesa ya mboga.

Prof. Tibaijuka alipokuwa madarakani alitaka kuuza sehemu ya Kigamboni kwa mwekezaji, kwa ajili ya Mradi wa Kigamboni New City project.

Magufuli aliufuta mradi.
Sawa lakini kama ameamua kusisima na jamii kutetea maslahi ya nchi hatuna tatizo naye
 
Punguza hasira na kutukana watu bure

Anachofanya ni kitu kinachoitwa mobilization, ni matayarisho tuu!.

Nakushauri tusubirie mkataba wa HGA ndio utaona anapewa nini na muda gani.
P
Nonsense ndio tusi? kama sioni cha maana unachoendelea kunijibu ulitaka nitumie neno gani hebu niambie hapa niwe nalitumia??

Anafanya matayarisho ya nini? vipi tukibadili nia, huyo mwarabu atakuwa mjinga gani aanze kutupa pesa zake bure kwenye matayarisho?

Nonsense from you again.
 
Uamuzi wa kuwapa DPW, uliishafikiwa kitambo sana toka 2022 wakati hiyo IGA ilipo sainiwa, ile process ya kuridhiwa na Bunge ni just a due process, kinachopikwa sasa ndio mkataba wenyewe wa HGA, this is the real thing!.
P
Oooh kumbe!
Sasa hiyo Host Government Agreement (HGA) nayo mtaiweka wazi?
I hope DPW atalete tija... Watu wetu wapate ajira na ujuzi
 
Sidhani kama wanazidiwa ila ni mfumo wa chama dola wa kujitoa ufahamu, (unyumbu). Unyumbu nitabia ya watu wanao fikiri vizuri kuahirisha kufikiri kwasababu ya kulinda masilahi ya kundi fulani, (CCM), ama uoga wa kuwaogopa viongozi wao. kwakinyakyusa tunaita 'herding behavior'. Herding behavior is an occurrence of thoughtful people suspending their reasoning because of group objective or fearing their leaders
Njaa... Umaskini... Elimu duni! Vyote hivyo huzaa woga, njaa, umaskini na elimu duni!
 
nchi haina uelekeooo inaendaa kama imechanganyikiwaaa... suala la bandari unashindwa kuelewa tatizo ni MTAJI au USIMAMIZIII??? yani sehemu ambapo ni source kubwa ya mapatooo serikali inashindwaa kuwekaa mtaji sababu ya URASIMUUU??? serikalii imekubalii kuwa ufisadi wa bandari umefikisha taifa hapaa??? ni aibuu kubwa sanaaa kama taifaa kufika tupofikaaa ni UKICHAAA WA HALI YA JUUU.
 
Back
Top Bottom