Japo unajitaidi sana kuielimisha jamii kuhusu mikataba lakini watanzania walio wengi pamoja na wewe unazungumzia tu upande mmoja wa uhalali wa mikataba kutokana na nature ya mikataba ya kibiashara ilivyo kokote duniani hata hapa kwetu kwenye mabank na mikopo ya taasisi ndogondogo.
Kiualisia mkopo wa kibiashara lazima uwe na masharti, hakuna anayepinga hilo, Ila Shida kubwa inakuja kwenye ambavyo makampuni au taasisi tunazoingia nazo hiyo mikataba kutuzidi ujanja wa vipengele vya mkataba,uongo kwenye utekelezaji,uongo kwenye ukadiliaji,uongo wa kitaalamu.
Unakuta kampuni fulani inakuja Kwa staili ya utafiti inaleta wataalamu na wakishafanikisha ugunduzi wao wanaleta taarifa serikalini yenye chumvi au limao na ukishawapa Mladi hauleti matokeo yaliyotarajiwa au unatoa matarajio ya ziada lakini kwenye mikataba unakuta Hakuna hivyo vipengele.