Anthony Diallo aomba radhi kwa waliomuelewa vibaya kauli yake ya 'Viongozi waliopita walikuwa na Matatizo ya Akili'

Anthony Diallo aomba radhi kwa waliomuelewa vibaya kauli yake ya 'Viongozi waliopita walikuwa na Matatizo ya Akili'

Nawe kwa akili yako mbovu unaamini ameomba radhi. Ukweli ni aliousema mwanzo. Na wote tuliokuwepo 2015-20 tunakubaliana naye. Ilikuwa tunaongozwa na kichaa. Tuliona na wala Diallo hakusema lolote jipya kwa vile.
 
Hiki ni kipindi cha kila mtu kutaka kujulikana kwamba ni shujaa, hata kama ni kwa sababu za kuipuuzi. Naagalia maelezo ya Diallo, ni wazi kwamba hajitambui nafasi yake na hatambui matokeo na maelezo yake. Kwa kiasi kikubwa ni elimu ndogo aliyonayo ambayo haikuongezeka kwa miaka yote aliyoacha kazi yake ya RMA na kujiita daktari...
Tatizo lenu hamtaki kuambiwa ukweli...
 
Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mwanza, Dk. Anthony Diallo ameomba radhi ‘kiaina’ baada ya kauli yake kuzua mjadala ndani na nje ya chama chake.

Dk. Diallo amesema, ametafasiriwa vibaya na baadhi ya watu huku akiwataka wanachama wa chama hicho tawala nchini Tanzania kuwa makini kwani wapo wasiowatakia mema wanatumia mwanya huo kuwachonganisha...
Ahaa Dialo tumekusikia kwa masikio yetu Leo umeamua kikana kivuli chako.hadi watoto wamekusikia huo mda mbona wengi wao walikuwa hawajalala.leo baada ya kusakwama umeamua kupindua meza eti hujaongea ivo eti watu wametafasili vingine.simamia msimamo wako we sema ulichokiongea ndicho hicho hich .
 
Hiki ni kipindi cha kila mtu kutaka kujulikana kwamba ni shujaa, hata kama ni kwa sababu za kuipuuzi. Naagalia maelezo ya Diallo, ni wazi kwamba hajitambui nafasi yake na hatambui matokeo na maelezo yake. Kwa kiasi kikubwa ni elimu ndogo aliyonayo ambayo haikuongezeka kwa miaka yote aliyoacha kazi yake ya RMA na kujiita daktari...
Tatizo lenu hamtaki kuambiwa ukweli
 
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mwanza, Dk. Anthony Diallo ameomba radhi ‘kiaina’ baada ya kauli yake kuzua mjadala ndani na nje ya chama chake...

Ni hivi, aombe msamaha au la, ujumbe sahihi umefika kuwa dhalimu alikuwa na tatizo la akili, na alikuwa ni mlevi wa madaraka. Ukweli una tabia moja tu, hata ukitaka kuukanusha huwa haukanushiki.

Amesema ukweli ambao wanaccm na watanzania wote wanaujua, japo ukweli huu unalindwa na ccm kwa nguvu zote usisemwe hadharani.
 
Ni
Hiki ni kipindi cha kila mtu kutaka kujulikana kwamba ni shujaa, hata kama ni kwa sababu za kuipuuzi. Naagalia maelezo ya Diallo, ni wazi kwamba hajitambui nafasi yake na hatambui matokeo na maelezo yake. Kwa kiasi kikubwa ni elimu ndogo aliyonayo ambayo haikuongezeka kwa miaka yote aliyoacha kazi yake ya RMA na kujiita daktari.

Kama kweli alijitoa muhanga bila kujali nafasi yake, iweje siku moja tu unaomba radhi? Hii ni kutaka kujinyonga, kitendo ambacho ni cha kipuuzi, halafu pia ukashindwa kuchagua tawi zuri au kamba imara ya kukamata shingo yako, ambao ni upuuzi wa juu zaidi. Kwa mtindo huu CCM bado muna mbumbumbu wengi tu!
Ni hadi uwe na akili Ili kumuelewa
 
Unasumbuliwa na utoto.
Sasa mwenyekiti wa CCM wa mkoa, kakiri kwamba ccm ilituletea mtu mwenye ulemavu wa akili awe Rais wa nchi, UTOTO ubatoka wapi?

Hii ni uvunjaji wa katiba. Mojawapo ya masharti ya kugombea urais, ni uwe na AKILI TIMAMU. Ni wazi Magufuli hakuwa na AKILI TIMAMU. Sio ajabu aliweza kufanya ukatili wa kiwango kile. Kazi iendelee? Hapana, Tunahitaji kurekebisha rekodi zetu. Kwamba tuliwahi kufikia hatua mtu mgonjwa wa akili akawa Rais wetu
 
Ni hivi, aombe msamaha au la, ujumbe sahihi umefika kuwa dhalimu alikuwa na tatizo la akili, na alikuwa ni mlevi wa madaraka. Ukweli una tabia moja tu, hata ukitaka kuukanusha huwa haukanushiki. Amesema ukweli ambao wanaccm na watanzania wote wanaujua, japo ukweli huu unalindwa na ccm kwa nguvu zote usisemwe hadharani.
Ukweli ambao umewekwa wazi ni kuwa Diallo alidhania kufanya kampeni kupitia Star tv mwaka 2015 ndio loophole ya kutolipa kodi. Sasa alichobakiza ni hasira baada ya kulipishwa kodi.

Hata wewe unahilo tatizo. Ulidhani kushiriki uchaguzi ndio kushinda. Sasa una machungu ya kupoteza pesa, bora ungejilipa na kilimo.
 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, bwana Anthony Diallo amewaomba radhi watanzania kwa kauli zake alizozitoa kuwa viongozi wa Serikali waliopita walikuwa na mafaili mirembe.
View attachment 1849688

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mwanza, Dk. Anthony Diallo ameomba radhi ‘kiaina’ baada ya kauli yake kuzua mjadala ndani na nje ya chama chake.

Dk. Diallo amesema, ametafasiriwa vibaya na baadhi ya watu huku akiwataka wanachama wa chama hicho tawala nchini Tanzania kuwa makini kwani wapo wasiowatakia mema wanatumia mwanya huo kuwachonganisha.

Ni baada ya jana Jumamosi, tarehe 10 Julai 2021, kuzungumza masuala mbalimbali yaliyojitokeza katika utawala wa awamu ya tano akigusia suala la nchi kuongozwa kwa matamko.

Dk. Diallo aliyewahi kuwa waziri, alizungumza hayo katika kipindi cha Ajenda, kinachorushwa na kituo chake cha televisheni cha Star TV, jijini Mwanza.

Akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kupata maoni yake juu ya nchi kuongozwa kwa matamko bila kufuata Katiba na sheria, Dk. Diallo alisema, kuna umuhimu wa kuangalia historia ya mtu kabla ya kupewa dhamana ya kuongoza.

Mimi nafikiri tuwe waangalifu tu katika kuchagua tuwe tuna ‘track record’ kwani huko nyuma tuliwahi kuchagua watu walikwisha kwenda hospitali za vichaa ‘milembe’ harafu unamwachia aongoze nchi, kwa hiyo tuwe makini,” alisema.

Kauli hiyo ilizua mjadala na leo Jumapili, tarehe 11 Julai 2021, akizungumza na waandishi wa habari amesema “nilifanya kosa kwa kutolea mfano wa wakati uliopita badala ya wakati ujao kuwa tusipokuwa waangalifu tunaweza kuchagua viongozi wenye matatizo ya akili.”

Na sijasema mtu kuwa aliyekuwa na tatizo ila nilikosea tu kwenye maelezo. Nawataka radhi wale ambao walinielewa vibaya kwani wapo waliotafasiri wanavyojua wao,” amesema Dk. Diallo.

Mwanasiasa huyo mkongwe nchini amsema “mimi nadhani tuwe waangalifu sana hasa wana CCM, tumeanza kuingiliwa sana.”

Dk. Diallo amekosoa kitendo cha baadhi ya viongozi wa chama hicho kuanza kutoa matamko kabla ya kumsikiliza au kumuuliza alikuwa ana maanisha nini.

“Unakuta ni kiongozi wa chama anatoa tamko na kunituhumu kama vile nimefanya kosa, bila hata kuniuliza. Lazima tuwe waangalifu sana wana CCM,” amesema Dk. Diallo.

Miongoni mwa viongozi waliomshtumu ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), Kenani Kihongosi alisema, viongozi walioaminiwa na “chama chetu, na wanakaa katika vikao vya maamuzi, tunawaomba wawe na nidhamu na chama hiki.”

“Chama hiki ni kikubwa kuliko mtu, kwa hiyo mwenyekiti na katibu mkuu wetu, niwaombe sisi kama UVCCM, kauli ile imetuudhi sana, mwenyekiti wa CCM anapozungumza hivyo hapaswi kuungwa mkono.”

Kihongosi aliongeza kwa kusema “kama yeye aliona wanapaswa kwenda milembe hapa anafanya nini, kama ni vikao vya maamuzi yeye ni miongoni na kauli zile kama sisi vijana zinatuvunja moyo.”

Mwanahalisi
Oooh masikini, too late ujumbe wa kwanza ndio umepokelewa pakubwa mno 🤣🤣🤣
 
Cdm mmebaki kuwa wacheza Ngoma za ccm tu kwa sasa, hakuna operation haki, maandamano Wala wabunge wa covid 19, kila sehemu mnaangukia pua.
Mchukueni sasa huyo Dialo wenu
Mbona povu mkuu 🤣🤣🤣
 
  • Thanks
Reactions: mmh
Back
Top Bottom