"Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) inawataarifu wateja wake kuwa kumetokea hitilafu kwenye mfumo wa njia ya kusafirisha umeme ya gridi ya taifa kuanzia 8:22 hivyo kusababisha baadhi ya maeneo nchini kukosa huduma ya umeme.

"Wataalamu wetu wanaendelea na jitihada za kurejesha huduma.

"Shirika linawaomba uvumilivu wateja wake katika kipindi hiki ambacho huduma ya umeme imekosekana."
 
Eneo nililopo Mbagala umeme ulikatika usiku wa manane kabla ya saa nane usiku mpaka hivi sasa saa mbili na asubuhi umeme haujarudi.

Ni hivi karibuni mheshimiwa alisema mtambo mmoja mpya umewashwa huo ndio mwisho wa kukatika kwa umeme, umeme ndio huo umekatika.

Hivi hawa viongozi wa CCM kwanini wanakuwa na haraka ya kutatua matatizo kwa mdomo!
 
Na wewe ukamwamini? Sijawahi KAMWE kumwamini mwana CCM yoyote yule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…