Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Yule mjinga hamis77 kawalisha ndimu kuhusu arsenal halafu kapotea. Kiukweli kama kuna msimu mlitutisha na mbio za ubingwa ni msimu wa 2022/23 na msimu wa 2023/24 ila sio msimu huu.

Yule mchele mliyesema muwaongezee westham pesa kidogo karudi kwenye default yake maana ule msimu aliluwa anatetea price tag yake.

Yule babu Partey mliyekuwa mnaonyesha dalili ya kumuuza anazima vizuri zaidi 6 kuliko Rice.

Hivi siku hizi hamna inverted fullback kama zamani au shida iko wapi?
 
Hoja dhaifu, kwa hiyo Majeruhi wanayo Arsenal pekee? Maamuzi mabovu ya marefa huwa yanakwenda kwa Arsenal pekee?? Hamna siku maamuzi yaliwanufaisha?? Au yakiwanufaisha sio shida zenu.

Kila timu inapitia vyote hivyo, jana tu Tot vs Newcastle mchezaji kaunawa mpira ikasababisha pasi ya goli lakini goli likawa halali. Lakini hata hawatoi milio kama nyie mazwa zwa.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Mashabiki wa Arsenyo wanapenda kudeka utafikiri Vitinda mimba(watoto wa mwisho)
Ukisikia wanavyolalamikia majeruhi utafikiri timu yao pekee ndio yenye majeruhi, ukija upande wa maamuzi ya marefa wanalalamika utafikiri ni wao pekee ndio wanaoonewa wakati takwimu zinaonyesha Arsenyo ndio timu inayoongoza kupata favor toka kwa waamuzi.
Mashabiki wa hii timu Masingeli amewaharibu sana kisaikolojia.
 
Majinga haya yanakuja na hoja dhaifu eti majeruhi, ooh wachezaji kupangwa out of position,, ondoeni baadhi ya useless players, sajilin kocha experienced,,,baada muda mtaona matunda!
 
Unapozungumzia injury kwenye timu, kuna vitu viwili vya kuzingatia

1. floor/ base ya timu inaundwa kupitia nini? mabeki au strikers? hivyo injury ya Calafiori kwa Arsenal ina madhara makubwa kuliko injury ya Lets say Jota kwa liverpool, cuz Arsenal's floor ni wachezaji wa nyuma

2. Injuries to key players, injury ya Saka au Ø pale Arsenal, the main creative force, ni sawa na injury ya De bruyne au Rodri pale City na ndio maana kama umenisoma vizuri nimesema City wame collapse sababu ya majeruhi, sikuitaja liverpool cuz wachezaji wao wazuri kama Salah, Trent n.k wepata muda mwimgi kuliko Saka, ø, Rodri na De bruyne.

Tunapolalamikia marefarii, tunalalamika point tulizopoteza sababu ya bad officiating, Brighton home and away, City at etihad, Bournemouth n.k hizo ni zaidi ya point sita zimepotea.

Mechi dhidi ya liverpool at home ilikuwa ni straight win, kuumia kwa Gabriel na timbertimber na kukosekana kwa saliba na Ø kuliwapa liverpool ahueni na kupata sare

Jana tumecheza bila Saka, havertz, Ø away to brighton baadae Nwaneri kaumia, so how do you expect us to compete kwa mazingira hayo?
 
Data zina support nachojua mimi, angalia liverpool ilipo, tukisema liverpool imekuwa na bahati kwenye suala la injury na bad officiating tunamaanisha hivi, haya ni mambo ya kisomi, ikiwa ulitoroka shule ukaenda kukaa milimani huwezi kuelewa, lazima ubishane sababu huoni wanachokiona wenye akili
 
Liver kasuluhu

Kaangalie nani anawalaumu 😅

Binafsi nipo jukwaa la nyumbu kuwapa pongezi.
 
Dakika 7 za nini kama sio agenda? mwisho wa picha wangefungwa wao sasa
 
Machawa yote yamelala, degree zao za uchambuzi zimeyeyuka paka pale Arsenal atapo draw tena, yaani unachojua ni kuchambua Arsenal inapodondosha point tu, get a job bro!
 
Dropped 4 points kwa Brighton.

Ukifanya kazi inayohitaji results hua tunajiuliza "When all else failed what was I doing?" Sawa game ya kwanza tulipata red and then what did we do?

Game ya pili sawa penati inaonekana ina upendeleo timu yetu ilifanya nini? Chances haziwi created na watu hawaendi mbele hilo ni kosa la refa?
 
Kuna mtandao nipo kuna hoja wameianzisha ambayo inaonyesha kwa msimu wa 23/24 katika games 20 tulikua na points 40 sawasawa na kipindi hichi.

Isipokua kwa msimu wa 23/24 tulikua nafasi ya 4 na msimu huu kwa points zile zile tupo nafasi ya 2. Wanasema inawezekana fans tunaoverreact ila kila kitu kipo under control.
 
Tulikuwa na tofauti ya points ngapi na anayeongoza?
 
Nwaneri anaumwa.

Baada ya game na Newcastle tuna game na nyumbu kwenye FA. Kuna page imetabiri kikosi cha kesho kinaweza kua hivi

Ingawa naona ni ngumu kiasi. Why?

Baada ya game ya kesho tarehe 12 tuna game na nyumbu kwenye FA. Kisha baada ya tarehe 12 unarudi mchaka mchaka wa kila baada ya siku 2 mechi.

Nahisi Arteta anaweza risk starters game ya kesho zaidi kuliko ya nyumbu labda waingie dakika za lala salama, ukizingatia sisi tupo CL na ligi wakati tunaokutana nao hawana cha kupoteza siyo kwenye ligi wala nje ya hapo so wao watakua full mkoko kutuzidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…