Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Eehh, "mpige na kibao" mtaani raha sana.

Zamani tulikuwa tunacheza soka bichi, mtu akipigwa kitu kizito tunaweza kuacha mpira tunaenda kujitosa baharini kwanza. πŸ˜‚πŸ€£
Mimi nilikua beki, kipindi hicho Emmanuel Eboue alikua ndiyo anakiwasha Arsenal. Jamaa nikawa napenda anavyocheza akaniinfluence kufocus na skills kuliko nguvu.

Kwahiyo mtu alikua akija vibaya nampiga body feints na ile chenga maarufu ya Zidane naipiga vizuri tu. Nilivyoanza chuo tu nikaanza ubishoo na mpira ukaishia hapo kuucheza
 
Kuna unconfirmed reports kwamba Leipzig wanataka ama tumnunue Sesko moja kwa moja au loan iwe na kipengele cha lazima kumnunua.

Arsenal inataka loan pekee.
 
Eboue, kitasa kimoja cha hatari sana, tulibahatika na Lauren etame mayer, kisha akaja Eboue.
 

Safi sana mkuu. Mimi niliacha kucheza mpira seriously nikiwa form 3. Muda wa mazoezi nikawa napendelea kuwa studio nikichora. Sasa nacheza kwa afya tu, na vijana wananipelekesha mbio balaa.

Ila mpirani nilikuwa ka Marc Overmars flani, au ka Martinelli hivi kwa sasa.
 
Kuna unconfirmed reports kwamba Leipzig wanataka ama tumnunue Sesko moja kwa moja au loan iwe na kipengele cha lazima kumnunua.

Arsenal inataka loan pekee.
Tunajichelewesha ama kuna chaguo jingine tofaut na Sesko Summer??
 
Kuna unconfirmed reports kwamba Leipzig wanataka ama tumnunue Sesko moja kwa moja au loan iwe na kipengele cha lazima kumnunua.

Arsenal inataka loan pekee.
Pia nilidhani Sesko atataka kwenda Unyumbuni kwa Amorim...?
 
Mtu anakwambia Arsenal tunategemea kona, you're right sababu tuna probability kubwa ya kufunga magoli ya kona ila Arsenal are xg miners, nioneshe ni lini mpinzani alitengeneza nafasi nyingi kutuzidi, kila timu tunayocheza dhidi yao lazima tuwazidi kwenye chance creation isipokuwa Brighton away, tatizo letu kubwa ni finishing sababu tunakosa clinical attacking, Liverpool ni timu yenye attacking bora kwenye premier league lakini nakuhakikishia tulitengeneza nafasi nyingi kuliko wao tulipokutana at emirates huku tukikosa baadhi ya wachezaji muhimu kama Odegaard, put some respect to Mikel Arteta
 
Nilijichanganya siku moja nikavaa six nikaingia.

Kwanza pumzi sina tena na control imekata. Akili inataka mwili unagoma.

Mi mpira haukua kipaji ni ilibidi nipractice daily ili nibaki palepale πŸ˜…
 
Unajua wabongo wengi hatujui mpira, nilimsikia mchambuzi wa clouds fm anasema anashangaa Arsenal kuhusishwa na usajili wa Zubimendi sababu tayari eneo la kiungo mkabaji ,DM, kwamba Arsenal ina wachezaji wengi kama Partey, Jorginho na Declan Rice, kwa hiyo haoni umuhimu wa Zubimendi to Arsenal, alichoshindwa kuelewa ni kwamba

kwanza, Partey & Jorginho wapo kwenye kipindi cha mwisho wa mikataba yao

pili, Zubimendi is the latest and better version of Jorginho

Tatu, profiles za Zubimendi + Rice zinacompliment kutumika kwenye double pivot kitu ambacho kinachange the team's dynamics, the most creative player ambaye ni Saka anaweza kuingia interior na kutumika km no.10 na kutatua tatizo kubwa tulilonalo la creativity, yaani timu inakuwa haina tena RCM role bali RCM inakuwa converted to no.10 ambaye mostly anakuwa kwenye Zone 14 na system inachange from 433 to 4231.
 
Kwetu wabongo beki ni beki na striker ni striker, yaani beki azuie, striker afunge, mpira tunauona hivyo, lakini kumbe unaweza kusajili beki na akatatua matatizo ya attack, mfano, usajili wa calafiori lengo lilikuwa, ok, ku stabilize defense lkn kubwa zaidi ni kuaffect our attacking dynamics, ndiyo maana Mikel arteta anasema after Timber's ACL injury last season kulizuia plan yake ya kuifanya Arsenal kuwa unpredictable force, leo ukimtoa Skelly lewis na kumtumia Kieran Tierney usitegemee kuwa na similar dynamics, mfano mzuri ni namna tulivyokuwa wazuri na fluid going forward baada ya usajili wa zinchenko, leo tupo sawasawa kwenye kutengeneza nafasi lkn tupo hovyo kwenye finishing, naamini tunahitaji usajili wa striker sababu ya finishing, na ieleweke kwamba finishing ni suala la mtu binafsi sio jambo la system
 
Kuna shabiki wa Chelsea aliwahi kunambia kwamba Arsenal tuna a lots of system plyers, leo naamini, baada ya hili tatizo la finishing, sio kai havertz tu, ila a lots of our players wana Miss hizo big chances, Rice, Merino, odegard, havertz etc hii ni kukosa individual brilliance level ya Mo Salah, tukumbuke plan A ilikuwa ni Dusan Vlahovic, Mykhalo Mudryk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…