Will Jr
JF-Expert Member
- Jul 21, 2018
- 4,897
- 7,074
Brighton ni timu nzuri, yenye kocha mdogo mwenye ambition, wachezaji wazuri super talented sio rahisi kutengeneza chances kwa kiwango unachodhani, baadhi ya mechi utashinda ushindi mwembamba, fine margin, mpira upo hivyo, inapotokea referee akaharibu ushindi huo ndipo watu wanalalamika.Dropped 4 points kwa Brighton.
Ukifanya kazi inayohitaji results hua tunajiuliza "When all else failed what was I doing?" Sawa game ya kwanza tulipata red and then what did we do?
Game ya pili sawa penati inaonekana ina upendeleo timu yetu ilifanya nini? Chances haziwi created na watu hawaendi mbele hilo ni kosa la refa?
Mpira wa kusema brighton au brentford au Forest ni timu ndogo umepitwa na wakati, kina Trossard, Ben white, cucurela hata Moises Caicedo walitoka brighton na walisajiliwa kwa mamillion ya pesa, leo tunahusishwa na wachezaji km Mbeumo, Semenyo n.k wanaotoka timu za aina hii tukidhani kwamba wanaweza kutuvusha kwenye daraja tulilokwama, wapo kina Baleba, Mitoma n.k wanahusishwa na timu kubwa kama Liverpool, kwa hiyo si rahisi kutengeza chances 20+ unapocheza na timu kama hizi. Unapopata goli hata moja unahitaji kulilinda ukicheza na timu za aina hii hasa ukiwa kwenye title race, ukipokonywa kwa makusudi lazima ulalamike.